Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 16
- 16
OSHA ni Wakala wa Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu. Wajibu wake ni kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vilivyopo au vinavyojitokeza katika sehemu za kazi ambavyo vinaweza kusababisha Magonjwa, Ajali na hata Vifo. OSHA inatekeleza majukumu yake chini ya Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 pamoja na Kanuni zilizoanzishwa chini ya Sheria hiyo.
Sheria imetafsiri mahali pa kazi "workplace" kama mahali popote au mazingira mtu anapofanyia kazi ikihusisha watu walioajiriwa na waliojiari. Pia Sheria hii inatakiwa kufatwa na Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Binafsi katika kuhakikisha wanazingatia Masharti yaliyowekwa chini ya Sheria na Kanuni zake kwa kuwa wote ni waajiri katika nyanja tofauti.
Swali langu ni je, kiuhalisia, ni kweli kwamba Taasisi hii inasimamia kwa ukamilifu Taasisi na Mashirika ya Umma katika kutekeleza masharti yaliyowekwa na Sheria kama wanavyofanya kwa Taasisi Binafsi au ndio huwezi kuukata mkono unaokulisha?