First Lady 1, please forgive me kwa urefu wa post
.
Inasikitisha sana mambo ambayo yanatokea katika jamii na hasa katika ndoa
Imekua ni mtihani kwa kweli
Sijui kama nitakua natoka off topic (sorry kueleweka nataka nidadafue the way naelewa).
Kutokana na ukweli kua maisha yamebadilika sana in every level hivyo kupanda kwa gharama kila sehemu ugusayo hasa ukitaka kitu quality ili kupata huduma ya uhakika iwe education, malazi/makazi, matibabu, chakula, - facts zinazofanya wenza wote wawili mujishulishe hivyo kama mna watoto mnamtafuta binti wa kuwasaidia
Tatizo ndo linakuja hapo.. NDIO akina dada tuko busy saaana lakini jamani are we so busy to the extent huwezi nyanyua kidole hata kidogo??? Nauliza/nasema hivi in the sense kua NDIO Msichana wako anakupa support katika kuendesha/kuangalia nyumba lakini je kuna haja ya kumpa full access kwa mumeo
kwa mtazamo wangu wadada/mama wengine huyataka mambo kama haya ya kwenye thread hii kuwatokea tokana na the way anendesha mambo yao katika ndoa yake
.
Kwanini umpe msichana wako FULL ACCESS kwa mumeo???? Ladies if you love your man and proud of him at all cost minimize vitu/mambo yawezao kumshawishi (akina mama tuna njia tofauti hii ni kwa wale wataoona I am right)
Kama Speaker alivyosema katika moja ya post.. Never let your mans mind wander .... Hivyo akina dada/mama tujiulize je wewe personaly umempa msichana wako (maarufu kwa house girl) Full Acces OR No Access kwa mumeo???
FULL ACCESS
Anaingia chumbani kwenu (eti kufanya usafi
lol!) na worse enough yeye ndo anatandika kitanda ambacho wewe na hubby mnajimwaya; Anapika mwenyewe (si mbaya sana) but worse enough yeye ndo anaandaa chakula na kumkaribisha hubby mezani..; Anampokea mizigo akifika in other words mumeo anatangulia kufika kabla yako kila siku (bad news - kwa wale ambao iko nje ya uwezo
); Ndio afue nguo (for maybe you have no time) but ziwahi hakuna haja ya hubby kuulizia soksi ikowapi which at the end of the day atamfuata binti kumuuliza mana anajua wazi hufui wewe
. Etc.
NO ACCESS
Huna nafasi ya kupika, but unahakikisha umekagua chakula, umeandaa mwenyewe na umemkaribisha mwenyewe mezani, Ndio nguo hafui but at least anahakiki zimetakata zimenyoshwa vizuri na zinarudishwa room kabla hubby hajazimiss..; Ana hakikisha kila mumewe anpokuwepo nyumbani yupo tayari home' labda in rare cases plus kujitahidi kurudi kabla ya the hubby
etc. Kwa ufupi kutojenga mazingira ya wao kuwa karibu
. House girl awe karibu na watoto
. BUT not the husband
Note; Wanaume hawalindiki hasa akiwa na nia but at least ikitokea utasema "I tried my best but he is just a Ba****"