Hivi wakihubiri kwa kuchanganya Kiswahili na Kingereza ndio neno linaingia zaidi?

Hivi wakihubiri kwa kuchanganya Kiswahili na Kingereza ndio neno linaingia zaidi?

Imezuka tabia ya wahubiri vijana kuhubiri kwa kuchanganya kiswahili na kingereza (broken English) na tabia hii mimi binafsi inanifikirisha sana. Kiufupi nikishajua muhubiri huyu ni mchanganyaji wa lugha huwa siwezi kumsikiliza hata nusu dakika. Sijui ndio ujanja au ndio waumini wanaelewa zaidi sijaelewa.
Ukweli ni kwamba mnaboa. Afadhali makanisa yenye wakalimani, angalau mtu unaelewa wanasema nini. Sasa unakuta mtu kingereza chenyewe cha huko Nyumbigwa halafu bado anakilazimisha mwe😭😭
Ushauri wangu, kama mnalenga waumini waelewe mnachofundisha ongeeni lugha moja, either kiswahili au kingereza, na kukiwa na ulazima basi tumieni wakalimani.
Asante sana.
Wanafabnya hivyo kuwavuruga akili
 
Humu mtandaoni mtu asipoandika neno la kiingereza, utasikia fulani kaishia la ngapi aisee.
Jieleze kadri uwezavyo, usiogope kashfa za watu.

Kisa hujui kiingereza ndo huna haki ya kujieleza?

Na ukiona mtu anakushambulia, ujue hana hoja.

"Where we dare to talk openly."
 
Nilimkuta muuza dawa za asili mahali akiitambulisha dawa inaitwa "besila lagos small snake kutoka canada" baada ya kusema hivyo watu waliipapatikia mpaka ikaisha
 
Kiingereza kinahamashisha Shekhe na Sadaka zinatoka.
Wewe jaribu hata kupata dem anaye gugumia kwa kiingereza kitandani kitandani utaona hamasa yake😂😂.
Kamuulize🗝️
 
Jieleze kadri uwezavyo, usiogope kashfa za watu.

Kisa hujui kiingereza ndo huna haki ya kujieleza?

Na ukiona mtu anakushambulia, ujue hana hoja.

"Where we dare to talk openly."
Hapa jf hata Kama ukiandika uzi wa kiingereza huwezi kupata wachangiaji wengi.

Unakuta uzi umeandikwa kizungu ila mtu anarusha comment ya kiswahili

Au nimeandika uongo?

Tatizo humu kuna watu tu wa ajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom