Hivi wakina dada mnaposafiri, hayo mabegi makubwa mnaweka nini?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Heshima kwenu wakuu,

Mimi nashangaa, unakuta mdada anatoka Arusha anaenda Mwanza kukaa siku nne au wiki moja, lakini atabeba begi kubwa ukipishana naye utafikiri anaenda Mbinguni na Mizigo yake.

Begi litawekwa kwenye buti, hapo hapo ana mkoba mkubwa, ndani ya mkoba kuna mkoba mdogo na ndani ya mkoba ndogo kuna pochi na ndani ya Pochi kuna kamfuko anawekea simu au simu anaifunika na kitambaa ndo anaweka kwenye hiyo pochi ndogo kiasi kwamba akiwa Safarini hata hata ukimpigia simu hasikii, muwe mnawasamehe bure.

Swali langu kwenye begi Mnaweka nini?

Dunia simama nishuke



 
Wanakera sana yaani utadhani wanahama!wakati mwanaume ki begi cha mgongoni na laptop tuu kinatosha kwa safari
 
Mwanaume kwa safari za wiki moja huwa tunaenda na USB mfukoni tu..

Lakini wanawake unakuta safari ya week 1 ana mabegi makubwa mawili na mkoba mkubwa ndani....sijui huwa kuna siri gani mnabeba...au mkitembea huwa mnahamisha hadi vioo vya chumbani na pair zote za viatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…