figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Heshima kwenu wakuu,
Mimi nashangaa, unakuta mdada anatoka Arusha anaenda Mwanza kukaa siku nne au wiki moja, lakini atabeba begi kubwa ukipishana naye utafikiri anaenda Mbinguni na Mizigo yake.
Begi litawekwa kwenye buti, hapo hapo ana mkoba mkubwa, ndani ya mkoba kuna mkoba mdogo na ndani ya mkoba ndogo kuna pochi na ndani ya Pochi kuna kamfuko anawekea simu au simu anaifunika na kitambaa ndo anaweka kwenye hiyo pochi ndogo kiasi kwamba akiwa Safarini hata hata ukimpigia simu hasikii, muwe mnawasamehe bure.
Swali langu kwenye begi Mnaweka nini?
Dunia simama nishuke
Mimi nashangaa, unakuta mdada anatoka Arusha anaenda Mwanza kukaa siku nne au wiki moja, lakini atabeba begi kubwa ukipishana naye utafikiri anaenda Mbinguni na Mizigo yake.
Begi litawekwa kwenye buti, hapo hapo ana mkoba mkubwa, ndani ya mkoba kuna mkoba mdogo na ndani ya mkoba ndogo kuna pochi na ndani ya Pochi kuna kamfuko anawekea simu au simu anaifunika na kitambaa ndo anaweka kwenye hiyo pochi ndogo kiasi kwamba akiwa Safarini hata hata ukimpigia simu hasikii, muwe mnawasamehe bure.
Swali langu kwenye begi Mnaweka nini?
Dunia simama nishuke
Mtoa mada naomba nijiongelee mimi binafsi....
Nikisafiri kama ni siku 4 hadi wiki moja zamani nilikuwa nabeba beginning kubwa moja yale ya ku check in. Ila siku hizi safari ya wiki 1 cabin bag aka hand luggage inahusika.
Kama ni safari ya kikazi na ntatakiwa kuwa formal nikiwa kazini huko niendako badi ntabeba sketi na blouse ya kuvaa kika moja siku yake. Sirudiagi kuvaa nguo bila kuifua hata iwe suti. Hapohapo jioni baada ya muda wa kazi ntatoka kwenda kula au kula bata, ntabeba nguo ya kuvaa usiku baada ya kuoga. Na nikirudi chumbani kulala ntalala na night dress hivo lazima nibebe night dress 2 au 3 hii ni kwa safari ya wiki 1.
Nguo ya kuendea ingine ya kurudia ingine. Kwa manikin hiyo safari ya siku 7 nguo ntabeba kama 20 hivi.... hapo nimebeba kamili kamili yaani siweki hata extra moja.
Nikisema nguo ya ziada ni pale inaweza tokea kitu ukahitaji kuvaa nguo halafu zote chafu, au ukakuta nguo uliyobeba kumbe zipi iliachia au hukuivaa siku nyingi kumbe imekuwa kubwa kiasi baada ya kupungua hivo haikukai vizuri tena au imekuwa inakubana sana baada ya kuongezeka kidogo. Si unajua miili ya kike mara uongezeke kidogo mara upungue basi burudani tuu.
Hapo kwenye viatu tarajia ntabeba viatu pea hata 4 hapo sijaweka pea 2 za emergency ikitokea ulichopanga kuvaa ukifika huko ukaona hakikai vizuri mguuni hivo pea 6 za viatu zinahusika. Begi lazima lijae.
Hapo sijaweka chupi brazia mtandio kitenge saa za kubadilisha hereni mkufu vibanio vya nywele kama sijasuka mtindo. Na chupi na brazia mie huwa napenda kubeba kila siku chupi yake na huwa sizifui kwa sababu zangu binafsi. Ntarudi kufua nikirudi nyumbani na huwa nakuwa na kibegi kidogo cha kuwekea chupi chafu nahakikisha hata Begi likichanika au kufunguka kwa bahati mbaya hazionekani hadharani.
Mie sinaga makorokoro ya kujipodoa zaidi ya perfume mafuta ya majina mwilini mafuta ya nywele wanja na lips shine.
Sasa ili kuwezesha begi lisiwe kubwa nguo nnazobeba ni zile laini laini ambazo nazikunja kina kuwa kidogoo kama ki wallet hivo kupunguza nafasi na ukubwa wa begi.
Kama ukikuta mwanamke ana mtoto ndo kabisaaa safari ya siku mbili mabega 6.... aahahahahahahaaa mvumilie tuu.
Ila na nyie safari ya siku 7 unabeba suruali 2 mashati 3 na t-shirt 2..... hapo kama hutoi oda zifuliwe ina maana wanaume huwa mnarudia kuvaa nguo chafu..... mke siwezi hiyo. Am comfortable when I have everything I need with me.
It's like having money all the time, am comfortable ila nikiwa sina hela.... comfortability inapotea. Same way nikiwa na nguo.... anytime mtu akaniambia tutoke navaa nguo ingine sirudii nguo hata kidogo. Nnachofanya tuu huwa sinunui nguo kwa ajili ya safari, ntabeba nguo zangu hizo hizo za kabatini. Hii imenifanya kila baada ya miezi 6 natoa nguo ambazo sizivai na zimechakaa ili wakati wowote niweze kuwa na nguo tayari tayari kwa safari na inayovalika. Japo saa ingine nachemka kufanya hivo naweza pitisha mwaka sijachambua nguo.