Hivi wakina dada mnaposafiri, hayo mabegi makubwa mnaweka nini?

Hivi wakina dada mnaposafiri, hayo mabegi makubwa mnaweka nini?

Mkuu,,,nadhani nikupe jibu simple ambalo utapatiamo jibu la swali lako,,,NGUO ZAO NI CHEAP.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahahahaaa wee acha uchokozi..... ni kweli nguo za kike ni bei nyepesi kidogo ukilingabisha na nguo za kiume. Mfano kiatu cha kiume unaweza kuta kinauzwa laki 2 na nusu ila cha kike ukakipata kwa laki na nusu. Vivo hivyo suti ya kiume laki 5 hadi saba zile suti quality akati suti quality ya kike laki tatu na nusu unapata.

Ila hiyo sio sababu ya kubeba mabega mengi.

Sema wanawake tuna mambo mengi kama maji hehehehheee.
 
Hahahahaaa wee acha uchokozi..... ni kweli nguo za kike ni bei nyepesi kidogo ukilingabisha na nguo za kiume. Mfano kiatu cha kiume unaweza kuta kinauzwa laki 2 na nusu ila cha kike ukakipata kwa laki na nusu. Vivo hivyo suti ya kiume laki 5 hadi saba zile suti quality akati suti quality ya kike laki tatu na nusu unapata.

Ila hiyo sio sababu ya kubeba mabega mengi.

Sema wanawake tuna mambo mengi kama maji hehehehheee.
[emoji23] mambo kasie,,,mi naona kwa kua nguo za kike ni cheap ndo mana mnasafiri nazo nyingi coz mmenunua nyingi,,,zetu expensive si rahisi kusafiri na mitoko yote kuna kuibiwa au gari kuwaka moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada naomba nijiongelee mimi binafsi....

Nikisafiri kama ni siku 4 hadi wiki moja zamani nilikuwa nabeba beginning kubwa moja yale ya ku check in. Ila siku hizi safari ya wiki 1 cabin bag aka hand luggage inahusika.

Kama ni safari ya kikazi na ntatakiwa kuwa formal nikiwa kazini huko niendako badi ntabeba sketi na blouse ya kuvaa kika moja siku yake. Sirudiagi kuvaa nguo bila kuifua hata iwe suti. Hapohapo jioni baada ya muda wa kazi ntatoka kwenda kula au kula bata, ntabeba nguo ya kuvaa usiku baada ya kuoga. Na nikirudi chumbani kulala ntalala na night dress hivo lazima nibebe night dress 2 au 3 hii ni kwa safari ya wiki 1.
Nguo ya kuendea ingine ya kurudia ingine. Kwa manikin hiyo safari ya siku 7 nguo ntabeba kama 20 hivi.... hapo nimebeba kamili kamili yaani siweki hata extra moja.

Nikisema nguo ya ziada ni pale inaweza tokea kitu ukahitaji kuvaa nguo halafu zote chafu, au ukakuta nguo uliyobeba kumbe zipi iliachia au hukuivaa siku nyingi kumbe imekuwa kubwa kiasi baada ya kupungua hivo haikukai vizuri tena au imekuwa inakubana sana baada ya kuongezeka kidogo. Si unajua miili ya kike mara uongezeke kidogo mara upungue basi burudani tuu.

Hapo kwenye viatu tarajia ntabeba viatu pea hata 4 hapo sijaweka pea 2 za emergency ikitokea ulichopanga kuvaa ukifika huko ukaona hakikai vizuri mguuni hivo pea 6 za viatu zinahusika. Begi lazima lijae.

Hapo sijaweka chupi brazia mtandio kitenge saa za kubadilisha hereni mkufu vibanio vya nywele kama sijasuka mtindo. Na chupi na brazia mie huwa napenda kubeba kila siku chupi yake na huwa sizifui kwa sababu zangu binafsi. Ntarudi kufua nikirudi nyumbani na huwa nakuwa na kibegi kidogo cha kuwekea chupi chafu nahakikisha hata Begi likichanika au kufunguka kwa bahati mbaya hazionekani hadharani.

Mie sinaga makorokoro ya kujipodoa zaidi ya perfume mafuta ya majina mwilini mafuta ya nywele wanja na lips shine.

Sasa ili kuwezesha begi lisiwe kubwa nguo nnazobeba ni zile laini laini ambazo nazikunja kina kuwa kidogoo kama ki wallet hivo kupunguza nafasi na ukubwa wa begi.

Kama ukikuta mwanamke ana mtoto ndo kabisaaa safari ya siku mbili mabega 6.... aahahahahahahaaa mvumilie tuu.

Ila na nyie safari ya siku 7 unabeba suruali 2 mashati 3 na t-shirt 2..... hapo kama hutoi oda zifuliwe ina maana wanaume huwa mnarudia kuvaa nguo chafu..... mke siwezi hiyo. Am comfortable when I have everything I need with me.

It's like having money all the time, am comfortable ila nikiwa sina hela.... comfortability inapotea. Same way nikiwa na nguo.... anytime mtu akaniambia tutoke navaa nguo ingine sirudii nguo hata kidogo. Nnachofanya tuu huwa sinunui nguo kwa ajili ya safari, ntabeba nguo zangu hizo hizo za kabatini. Hii imenifanya kila baada ya miezi 6 natoa nguo ambazo sizivai na zimechakaa ili wakati wowote niweze kuwa na nguo tayari tayari kwa safari na inayovalika. Japo saa ingine nachemka kufanya hivo naweza pitisha mwaka sijachambua nguo.
 
Nguo za mitoko za kukomeshea mtaa anapofikia. Yaan ni ile pania na funga kazi asifiwe yeye tu kwa kuvaa nguo bila kurudia.
 
Hapo hapo Hata nyie mtuambie nyie ..."me" haswa vijana age ya 18-25 hivi hizi bag pack mnajibebesha siku hizi mnazunguka nayo kutwa huwa mnaweka nini ? View attachment 785236
Huu mtindo wa kila mtu siku hizi bag mgongoni unatuharibia sana sisi tunaotembea nayo yakiwa na zana za msingi za kazi zetu za kila siku,siku hiyo jamaa mmoja tunaheshimiana sana naye ananiuliza "kila siku na bag mgongoni au hirizi?",nikamwangaliaaa sema nikabadilisha maongezi.

Mkuu kweli siyo wote wenye kazi nayo ni ubishoo tu ila baadhi huwa wana kazi nayo tena muhimu sana,sisi wengine bila bag siku hiyo hesabu haingii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana tukawa wa kike
Nikivaa nguo sirudii na niko ugenini
Nianze kuhangaishana na kufua wapi na wapi
Mm nabebaga mbegi mkubwaa hata kama safar ya siku tatu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kidogo unaeleweka. Lakini ndo mabegi mawili?

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using Tapatalk
 
Wanaume hata kama anenda kukaa mwezi hana hata wasiwasi.
Why-do-you-need-a-vacation-218x150.jpg
mm chuo huwa begi kama hilo tu linanitosha humo naweka suruali, shati, tsheti,viatu na nguo za ndani, suka na blanget hapo semister ni miezi 4
 
Halaf unakuta kadada kenyewe kembamba tu bora angekuwa mneneee tungesema anavaa majeans kama ya pepe kale
 
Back
Top Bottom