Hivi wali una nini cha mno?

jmapunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
731
Reaction score
2,923
Wandugu,nimekuwa nikijiuliza na kushangaa hiki chakula chenye majina mengi kwanini kinapendwa sana na watu karibu wa rika zote?Labda walevi ndio hawakifagilii sana.

Nipo ugenini kwa ndugu zangu,huku zao kuu ni mpunga.Ndugu zangu hawa waliniomba nije na unga wa mahindi kwani wanaumiss ugali.Ajabu ni kwamba wiki ya tatu sasa hawajapika ugali labda ni uji tu wa mtoto.

Nauliza tena chakula hiki kina nini cha mno?
 
samahani, wewe ni mtu wa pwani?
 
ungeuliza mchele una nini cha zaidi........? labda ningekuelewa
 
Cha ajabu ukifululiza wiki moja, unatamani ugali, ila ugali hata mwaka fresh tu.
 
Wali ni mzuri ila kula wiki nzima unakinai tofauti na ugali.
Pole mana hata mimi siwezi kaa wiki tatu nakula tu wali.
 
Aaah! Hapana chezea ugali wewe!
 
Chakula hakiwez kuwa ugali bhana wee..

1. Chakula gani kinabagua mboga
2. Mahindi huko wanafanya msosi wa ng'ombe...
3. Chakula cha shida, ushawah kuona kwenye matatzo kama somalia au wapi huko wanaangushiwa viroba vya mchele ni unga tuu..

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Jokes..
 
Ha ha kwa wale wa enzi zileeee. Nakumbuka siku ukipikwa ubwabwa
1. Unawahi kuoga maana hiyo ndio pswd ya kula.
2. Hupendi kabisa wenzako waje kucheza kwenu. Na wakija wakagundua kuna ubwabwa hawaondoki mpaka wanakula unaisha.
3. Ukiacha kiporo unawahi kurudi nyumbani ili bro asije akakipiga chote ukaambiwa songa ugali[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…