Hivi wali una nini cha mno?

Hivi wali una nini cha mno?

Kinapendwa sababu kile kingine kinamapungufu, wali una mafuta, chumvi nk. Wakati ugali unachemshwa tuuu bila kitu vitalinganaje? Wenzio wanaumiza vichwa kwa mambo ya maana we unawaza tofaut ya wali na ugali,,,,!!!??
[emoji13] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wali ni chakula pekee unaweza kula bila mboga bado kikawa poah tuuh.
 
Tangu utoto wangu nmeupenda wali mpaka leo,wali kwangu haujawahi kuisha utamu hata kidogo.
 
Tofaut ya wali na ugali unataka kujua!

Kwanza wali ni chakula chenye energy nyingi yaani protein, pia ukila wali una uwoze wa kukaa muda mrefu bila ya njaa hata ufanye kazi ngumu.

Ugali ni chakula chenye nguvu mwilini, tatizo lake huwezi kukaa muda mrefu, lazima utaona njaa, mie ugali naupenda ila ukipikwa huomba kiwepo chakula chengine ziada baada ya muda ni njaa
 
Mbona lugha zenu zinaleta ukakasi atii !, huo wali haubanikwi, bali unakuwa unapaliwa na makaa ya moto , kwa maana ukishaiva kabla ya kukauka, unachukua chombo cha kufunika juu yake unaweka makaa ya moto, ndiyo kupalia kwenyewe hukooo!
Shukrani kwa muongozo Bwana Mpunga.
 
umemshinda ndege huo swaiba mi binafsi naona chakula kawaida sana kama ugali tu
 
Wali ulianza kuliwaza akili zetu toka tukiwa wadogo,utaendelea kutuliwaza siku ya harusi,na utaendelea kutuliwaza mpaka siku ya msiba,udumu wali jana, leo,kesho na hata milele.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Wali ulianza kuliwaza akili zetu toka tukiwa wadogo,utaendelea kutuliwaza siku ya harusi,na utaendelea kutuliwaza mpaka siku ya msiba,udumu wali jana, leo,kesho na hata milele.
 
Ugali ni rizki,wali chakula,
uliona kwenye sherehe au misiba wanapika ugali? Kama umesoma shule za bweni siku ya kupikwa wali inakuaje?
Majibu mnayo tayari
 
Hii kitu ina majina meengi kweli kweli wala hujakosea na mengi ya majina hayo ni kuonesha sifa zake na aina za mapishi kwa mfano

Mpunga

Wali

Punje ( Ilitumika zaidi sehemu za Skuli)

Mpunyenye ( Hiii kwa wazee wetu waleee wa zamani)

Pilau ( Raha yake uwe na kachumbari na ndizi mbivu) na haswaa kwenye shughuli

Biriani ( Mapishi ya kihindi)

Ubwabwa ( Huu uliwe na maharage ) haki ya nani weka mbali na watoto !

Boko ( Hapa aidha mapishi yameenda doroo au uji wa mgonjwa)

Mchele ( kwa ndugu zetu wa Uganda na akina Omera pale za kanda ya ziwa)

Ubeche ! heee heee heee !
Halafu kwa kumalizia hata ID yako ni MPUNGA 😀😀
 
Acha kabisa. Umpate mpishi na hasa awe wa PWANI.
Mkuu wali upikwe na Myemeni, wao wanaita MANDI,
Pembeni kunakua na vitunguu vilivyokatwa katwa na kua vyembambaa kisha vikakamuliwa na limao,haki ya nani unaweza sahau hata jina lako kwa utamu wa Mandi.
 
Back
Top Bottom