Hivi Walimu ni mishahara ndio inawapa hasira?

Hivi Walimu ni mishahara ndio inawapa hasira?

we utakua mmoja wa hao wanafunzi,

sheria hairuhusu kuingia na simu, kama unaona walimu hawako sahihi, kawashitaki
 
hivi mwanafunzi wa f6 naye ni mtoto? hajui jema na baya? hakuna sheria za shule? hongereni walimu, mungu awabariki maana kupitia hao wachache wengine wamejifunza. mmewalinda vyema!
 
Hivi sababu za msingi za kuzuia simu ni zipi??

Afrika kuja kuendelea tutasubiri sana!
Watoto nao bwana !!. Kwanini walazimishe kuwa na simu wakati wakijua shule zote zimekataza kuwa na simu shuleni ?!. Na hili zaidi ni kwa shule za serikali . Huwezi kuona upuuzi ktk shule za masista
 
Hizi sheria ziangaliwe upya!

Wanafunzi wanaweza kumiliki simu na gadgets kwa ajili ya masomo katika nyakati hizi za teknolojia.

Swala sio tu kuzisimamia sheria kama roboti.....Utashi unahitajika pia.

Utambuzi wa nyakati na mazingira husika!
 
Nenda kasome sheria za shule uone adhabu ya kutumia simu

Nadhani hujasoma boarding ndio maana, Laiti ungeona sehemu wanazochajia (local connections) usingesema,

In case ikija kutokea bweni limeungua na wanafunzi wamekufa ww ndio utakuwa was kwanza kuwalauni walimu walikuwa wazembe hawafuatilii

NB
Ualimu ni kama ukocha tu katika mafanikio watasifiwa wengine kikiharibika kitu lawama kwao
Kwanini wasiwekewe socket za kutosha ili wasihangaike na hizo local connections!?
Mi nakumbuka nikiwa A level kuchaji simu library ilikuwa ruksa tu, na hakukuwa na tatizo lolote!
 
Hizi sheria ziangaliwe upya!

Wanafunzi wanaweza kumiliki simu na gadgets kwa ajili ya masomo katika nyakati hizi za teknolojia.

Swala sio tu kuzisimamia sheria kama roboti.....Utashi unahitajika pia.

Utambuzi wa nyakati na mazingira husika!
Kweli mkuu, sasa watu wamekazana tu simu marufuku, yan ujinga ujinga tu!
 
Hivi sababu za msingi za kuzuia simu ni zipi??

Afrika kuna kuendelea tutasubiri sana!
Hili ni Taifa la watu "waliosomea ujinga". Wengi wao hawana utambuzi wa maswala hata ya ufahamu wa kawaida tu.

Nyakati hizi za sasa simu ni kifaa muhimu sana katika masomo na mazingira yoyote ya kujifunzia.

YouTube tutorials, google, e-learning platforms, Telegram, whatsapp-sharing materials and documents nk.... huko pana kila nyenzo ya kujifunzia.

Naona bado sana watu kulitambua hili. Tuko miaka ya 1960's huko!
 
Kweli mkuu, sasa watu wamekazana tu simu marufuku, yan ujinga ujinga tu!
Binafsi sioni ubaya wa simu hasa kwa mwanafunzi wa A level ambaye ameshajitambua.

Au hata hao wanafunzi wa ngazi za chini, madhali tu kuwe na utaratibu maalumu.

Simu sio kifaa cha anasa kama inavyotafsiriwa.

Kuna shida mahali.
 
Wamekosea lakini walimu wamekosea sana
Walimu hawana makosa,wamefuata sheria za shule,Kama kufuata sheria ni makosa,basi hata askari wanaowakamata wavunja sheria wanafanya makosa,na mahakama zinazowahukumu zina makosa pia. Mimi nawapongeza walimu hao.
 
Kuna mwaka wanafunzi kadhaa walifutiwa matokeo kwa sababu ya simu..

Walikuwa na simu wakapata baadhi ya mitihani,wakasolve wakaandika summary zao,muda wa kuingia kwenye mtihani ukafika;wakaingia na huo ulikuwa mtihani wao wa mwisho.
Kuna wasimamizi kutoka baraza nadhani wakaanza kupita mashuleni,wakakagua yale mabegi na wakagundua summary zao zinafanana na kile kilichopo ndicho hichohicho wamo ndani kuandika.
Walibebwa na kupelekwa polisi.
Watoto takribani 15 walifutiwa matokeo Yao.

Mtoa mada hujui madhara ya simu wewe.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu Wapo Vema Sana, Wagosi Wa Kaya
Wana Song Lao Zuri Kuhusu Walimu
 
Walimu Wapo Vema Sana, Wagosi Wa Kaya
Wana Song Lao Zuri Kuhusu Walimu
 
Hizi sheria ziangaliwe upya!

Wanafunzi wanaweza kumiliki simu na gadgets kwa ajili ya masomo katika nyakati hizi za teknolojia.

Swala sio tu kuzisimamia sheria kama roboti.....Utashi unahitajika pia.

Utambuzi wa nyakati na mazingira husika!
Bahati mbaya asilimia kubwa ya wanafunzi wetu hawatumii simu kwa ajili ya kujisomea.
Wengi wao ni mapenzi na kuwasiliana na wazazi kidogo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sioni ubaya wa simu hasa kwa mwanafunzi wa A level ambaye ameshajimbua.

Au hata hao wanafunzi wa ngazi za chini, madhali tu kuwe na utaratibu maalumu.

Simu sio kifaa cha anasa kama inavyotafsiriwa.

Kuna shida mahali.
Hizi ni sheria za shule,walimu wamefuata sheria zilizowekwa na serikali au shule husika kwa shule binafsi, wanafunzi wanamakosa, hii tabia ya kuwatetea wanafunzi wanaovunja sheria ni mbaya, haina afya kwa wanafunzi. Nawapongeza walimu hao
 
Kuna habari nimeona kwa wanafunzi wa form six wamefukuzwa shule siku chache kabla ya mitihani yao ya kuhitimu
Chanzo kabisa ni wanafunzi hao kukutwa na simu
Nimejiuliza inakuwaje mwalimu unahangaika kukagua wanafunzi amabaye hama hata zaidi ya mwezi kuendelea kuwepo hapo shuleni kama wana simu tena ni usiku ingekuwa hata ni muda wala hata sio muda wa kipindi na simu zenyewe walikuwa wanatumia kwa kunificha
Mngewaacha tu wamalizie mitihani yao
Unaambiwa hutakiwi kuwa na simu shuleni, na adhabu yake ni kufukuzwa tatizo ni nini...wamekutwa na simu na wakafukuzwa baasi. Wanafunzi wana makosa halafu ukiwasikiliza ni wajeuri sana
 
Wamekosea lakini walimu wamekosea sana

Walimu wamekosea sana kwenye nini sasa! Kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na serikali yako!

Na wasinge chungukua hatua, ungekuja tena kulialia hapa kwa nini hao hao walimu wanawaacha wanafunzi wamiliki simu shuleni kinyume na utaratibu uliowekwa na serikali.

Ushauri wa bure: Fuata sheria za nchi na taasisi zake. Utaishi maisha mazuri na hutakuja tena hapa kuwalaumu watu wanaotekeleza wajibu wao.
 
Shida sio kufuata tu sheria, maana hizo sheria ni tatizo pia.

Hata Hilter alipoua mamilioni ya waisrael aliwaua kwa kufuata sheria.

Lazima uelewe muktadha. Usiwe kama roboti lililowekwa betri.

Katiba ya nchi inabadilishwa, seuze hivyo vijisheria koko vya shule vilivoandikwa kwa penseli?

THEY ARE VERY SUBSIDIARY. DON'T BE STUPID.

Sio ninyi mnaolia lia kila siku kwamba elimu imeshuka? Kuna ubaya gani wanafunzi wakitumia simu na gadgets kwa ajili ya kujifunza?
Jambo hili inaonekana limekukera sana Mkuu,usiharibu siku yako. Hata hivyo kuna Jambo la msingi umeligusia kwamba sheria zinaweza kubadilishwa,pambania hilo. Kwa kuwa zikibadilishwa walimu watazifuata hizo sheria mpya.
 
Back
Top Bottom