Hivi Walimu ni mishahara ndio inawapa hasira?

Hivi Walimu ni mishahara ndio inawapa hasira?

Wewe endelea kupongeza maana ufahamu wako umeishia kwenye kupiga makofi.

Mimi nazungumza vitu vikubwa hapa! Kwahiyo endelea kupiga makofi!
Duh! Kuwatetea wanafunzi wanaovunja sheria za shule kwako ndivyo vitu vikubwa?
 
Suala la mishahara linaingiaje hapo? Watu wote wanaotekeleza wajibu wao kwa uaminifu ndiyo wanatafsiriwa kuwa wana hasira kwa kuwa kuna shida kwenye mishahara yao? Hata utumbuaji unaofanywa wa watu wanaoboronga serikalini tuseme kuwa mtumbuaji ana hasira kwa kuwa kuna shida kwenye mshahara wake?
 
Sawa nikosa! Waonyeni ili wamalizie, kuwafukuza hamuoni ndo mnawaua kabisa?
Kumbukeni hao ni watoto, nashauli shule zingebuni mbinu mbadala hata kuweka didector machine siku wanapo report shuleni.

Nyie waalimu huwa hamjiulizi kwamba kama simu inaingia gerezani sehemu yenye mabunduki na ulinzi mkubwa sembuse na shuleni?

Inamaana na askari magereza wawe wanafukuzwa pale wafungwa wanapokutwa na simu?
Kumbukeni hao niwatoto

Hizo zitakuwa nihasira za kunyimwa michango ya michele🤣🤣🤣☝

Wanazimalizia kwa watoto.

Wewe nawe tangu uje na mada yako ya kulialia ukiwalaumu hao walimu wa huko kijijini kwako kukutaka uchangie mchele kidogo tu ili mtoto wako asome vizuri, basi ndiyo hatunywi maji!

Ulichosahau ni kwamba tupo wazazi wengi tu humu jukwaani tunatoa hiyo michango ya chakula kila mwezi na watoto wetu wanapata elimu mpaka saa 11 jioni wakati huu wanapojiandaa na mitihani yao ya darasa la 7, na wala hutuoni tukilialia humu mana tunafahamu umuhimu wa elimu kwa watoto wetu! tofauti kabisa na wewe ambaye umetanguliza zaidi ULAFI.
 
Kipindi cha mitihani wapo na simu?? Ikitokea kumbe wanatumia kusambaza maswali na majibu ya NECTA, halafu wakaingia nazo kwenye vyumba vya mtihani na baadaye wakakamatwa na wasimamizi je mkuu wa shule, wasimamizi wenyewe na kituo cha mtihani kwa ujumla kitakuwaje? Yaani ajira za watu na maisha ya watu yapo hatarini!
 
Hivi sababu za msingi za kuzuia simu ni zipi??

Afrika kuja kuendelea tutasubiri sana!
Kwamba simu zikiruhusiwa mashuleni italeta maendeleo zaidi barani Africa au unamanaisha nini?

Kila taasisi ina sheria zake na sheria za shule haziruhusu simu hilo linajulikana wazi, kujiunga na hizo shule means umekubaliana na sheria na taratibu zake na endapo utakiuka basi sheria itafata mkondo wake.
 
mlikaa na matoto yenu majumbani miezi mitatu mkaona kama mwaka mkaadha kupiga kelele bora warudi shule haya wamerudi shule wazazi walimu wanasimamia kile kilichokuwa kinawashinda majumbani mnaanza kelele
Kuna mazazi mengine sijui yana akili gani! Ubawalaumu walimu kwa kosa gani? Ukute hili lim-mama lina mtoto amefukuzwa! Tena hao watoto wasirudishwe shule kabisa!
 
Kuna habari nimeona kwa wanafunzi wa form six wamefukuzwa shule siku chache kabla ya mitihani yao ya kuhitimu
Chanzo kabisa ni wanafunzi hao kukutwa na simu
Nimejiuliza inakuwaje mwalimu unahangaika kukagua wanafunzi amabaye hama hata zaidi ya mwezi kuendelea kuwepo hapo shuleni kama wana simu tena ni usiku ingekuwa hata ni muda wala hata sio muda wa kipindi na simu zenyewe walikuwa wanatumia kwa kunificha
Mngewaacha tu wamalizie mitihani yao
Kama wewe sio mwalimu huwezi kumfundisha mwalimu jinsi ya kufanya kazi yake, kama wewe sio daktari, hauwezi kumfundisha daktari jinsi ya kukutibu. Ualimu ni professional kama zilivyo zingine. Itachukua juda sana kukuelewesha kwa vile inaonekana una hasira na walimu. Kwanza nikusahihishe tu. Sio kweli kwamba walimu wana mishahara midogo. Hilo ulijue kuanzia leo. Shida ya walimu ni matumizi, wanatumia fedha zao bila mpangilio. Na shida ingine ni kukopa mikopo ya riba kubwa kubwa. Na hili ndo linawafanya kuonekana hawana hela. Ila kwa walimu wa degree wakiajiriwa wanaanzia lake 7 na diploma laki 5.5 huu sio mshahara mdogo sababu ushavuka kima cha chini.
Nije kwenye point yako sasa. Ni sheria mwanafunzi haruhusiwi kjmiliki simu. Na kosa kama hilo ni kufukuzwa shule wala sio suspension kama walivofanyiwa hawa.
 
Hao vijana walishindwa kuvumilia mwezi mmoja kweli
 
hao watoto wasirudishwe shule kabisa!
Hapa hatuwazungumzii tu "hao watoto" waliofukuzwa (japo sina uhakika kama ni watoto).

Tunazungumza katika muktadha mpana wa matumizi ya gadgets mashuleni.

Humu wanapita watu wengi wanasoma na wanaelewa. Watachukua linalowezekana.

Hivyo vijisheria koko vilivyoandikwa kwa penseli ni subsidiary mno tena mno! Vinaweza kufutwa kwa wino mweupe just within a matter of seconds!

Kwahiyo usishupaze sana shingo!
 
Kuna habari nimeona kwa wanafunzi wa form six wamefukuzwa shule siku chache kabla ya mitihani yao ya kuhitimu
Chanzo kabisa ni wanafunzi hao kukutwa na simu
Nimejiuliza inakuwaje mwalimu unahangaika kukagua wanafunzi amabaye hama hata zaidi ya mwezi kuendelea kuwepo hapo shuleni kama wana simu tena ni usiku ingekuwa hata ni muda wala hata sio muda wa kipindi na simu zenyewe walikuwa wanatumia kwa kunificha
Mngewaacha tu wamalizie mitihani yao
Pole Sana ila iyo Habari haijakamilika Bora ungetuletea yote bila ukamilifu wa Habari utawalaumu Sana walimu,,Sijui mishahara yao na kukamatwa simu kwa wanafunzi kunauhusiano gani?
Naomba nikukumbushe kuwa mwalimu Hana mamlaka ya kumfukuza mwanafunzi shule ila Bodi ya shule ndio yenye mamlaka ya kumfukuza mwanafunzi shule. kwa iyo Habari yako haijakamilika.
Pili bodi ya shule haina mamlaka ya kumzuia mwanafunzi wa kidato cha mitihani kufanya mtihani akiwa ameshasajiliwa na Baraza la mitihani labda mpaka akutwe na kosa la jinai na liwe limethibitishwa na mahakama,, Ila wanamamlaka ya kumfukuza shule ambapo mwanafunzi husika kama ni wa boarding atakuwa akitokea nyumbani kuja kufanya mtihani na kurudi nyumbani na sio kukaa tena shule.
Tofauti na miaka ya nyumba ambapo ulikuwa ukifukuzwa basi na haki yako ya kufanya mtihani unakuwa umepoteza.
Mleta mada tunaomba utueleze je hao wanafunzi wamefanya mtihani au hawajafanya Mana mwanangu amemaliza mtihani jana
Tuache kuwalaumu walimu kwa bila sababu tulipofikia Kama nchi tukiwa tunaona simu Ni muhimu basi sheria za nchi zibadilishwe na sio kila kitu mwalimu ndio anamakosa.
Mtanisamehe nilipokosea kuandika.
 
Hivi sababu za msingi za kuzuia simu ni zipi??

Afrika kuja kuendelea tutasubiri sana!
Huwezi kuvunja sheria kwa kuwa tu hukubaliani nayo !.

Kwa mazingira ya ki Africa ukiruhusu simu mashuleni . Utakuwa umeleta kesi nyingi za uwizi, na wanafunzi kupoteza muda mwingi kutumia simu, badala ya kuelekeza akili zao kwa kilichowapereka shuleni.
 
Hapa hatuwazungumzii tu "hao watoto" waliofukuzwa (japo sina uhakika kama ni watoto).

Tunazungumza katika muktadha mpana wa matumizi ya gadgets mashuleni.

Humu wanapita watu wengi wanasoma na wanaelewa. Watachukua linalowezekana.

Hivyo vijisheria koko vilivyoandikwa kwa penseli ni subsidiary mno tena mno! Vinaweza kufutwa kwa wino mweupe just within a matter of seconds!

Kwahiyo usishupaze sana shingo!
Ni upumbavu kushabikia wanafunzi kuwa na simu shuleni! Kama shule yako imeandika sheria hizo kwa penseli in upumbavu wa shule yako. Sheria hizo zinatoka wizarani wala siyo sheria za kujitungia walimu, hivyo watoto hao wafukuzwe moja kwa moja!
 
Daah umenikumbusha tulivyodakwa na simu wiki tatu before mtihani, tulikula fimbo na adhabu ya kufa mtu ila hatukufukuzwa
adhabu ya kufa mtu ila haukufa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna habari nimeona kwa wanafunzi wa form six wamefukuzwa shule siku chache kabla ya mitihani yao ya kuhitimu
Chanzo kabisa ni wanafunzi hao kukutwa na simu
Nimejiuliza inakuwaje mwalimu unahangaika kukagua wanafunzi amabaye hama hata zaidi ya mwezi kuendelea kuwepo hapo shuleni kama wana simu tena ni usiku ingekuwa hata ni muda wala hata sio muda wa kipindi na simu zenyewe walikuwa wanatumia kwa kunificha
Mngewaacha tu wamalizie mitihani yao
Simple anzisha shule yako watoto waje na simu
 
Back
Top Bottom