Hivi walimu tuna akili timamu kweli?

kajaga88

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2013
Posts
228
Reaction score
31
Habari wana jamvi.

kuna kipindi najiuliza maswali kama kweli walimu tuna akili ya kutosha.

Hivi inaingia akilini tangu mwaka jana mwezi wa 6, watu wamepanda daraja lakini mpaka sasa hawajabadilishiwa mishahara. Hivi kama ni idara nyingine inawezekana?

Uchaguzi umekaribia, utawaona walimu wanaenda kulala nje kwa kulipwa elfu 80, tu. hebu tudai haki zetu jamani, kwann tusigome ktk mambo kama haya?

Kwann cc waoga kiasi hicho? Mimi naomba niwe wa kwanza kufukuzwa kazi kwa kudai pesa yetu ya madaraja tangu kupandishwa mwaka jana.
 
msigome kula isue ya kuandikisha daftali la wapiga kura na usimamiaji wa kura
 
Wale wa kinondoni walitaka kumuotesha manundu mwenyekiti wao wa c.w.t.kwa mambo hayo hayo !! Je mnasubiri nini? Hawa watu hawana adabu!
 
walimu tuna halingumu,tutazua kitimutimu,hadi wizara ya elimu....
 
msigome kula isue ya kuandikisha daftali la wapiga kura na usimamiaji wa kura

Mwalimu wache wagome ni haki yao
Hayo unayoyasema mwaka huu uchaguz utakuwa tofauti na miaka mengine inahitajika watu makin km ww ni wa rushwa na kuyumbishwa na maneno huwez
 
Ki ufupi mwalim ndo kila kitu Tanyaoia, lakn bado serikal haimthamini.
 
Duh! Walimu wajanja sana mwaka huu watoto wamefaulu mtihani darasa la saba na kuchaguliwa kwenda sekondari. LAKINI HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA. WAZAZI WENYEWE WANAANGAIKA WATOTO KURUDIA LA TATU NA LA NNE???? CHEZEA WALIMU WEYE!!!!
 
Mimi nawapongeza kwa kiasi fulani wali wa msingi. Ila walimu wa sek umoja =0 unafki tu na woga
 
Hivi cwt wameshindwa kushughulikia matatizo ya wazi kama haya mpaka mtafutane kiasi hiki? [emoji35]
 
Dah! Namm Mda Wangu Wakupanda Daraja Ukifikia Cjui Itakuwa Ivyoivyo Au Rais Atakae Chaguliwa Atabadilisha Mifumo Ya Uongoz,.
 
kajaga88, kwanza nakupa big up kwa kutambua haki yako inayopotea.

Ila nakupa mbinu moja ya maisha yakutoka kama wewe ni mwalimu mpenda mafanikio.

Kama wewe ni mwalimu na unadiploma,fanya mpango wakusoma kitu kingne, mfano wewe una diploma ya mathematics, nenda kale degree ya accounting au computer sc, IT, economics au course yoyote!

Then rudi kituoni uombe kufanyiwa recategorization

tumia akiri zako zooote mpaka ufanikiwe na ukiona halmashauri yako wanabana tafuta halmashauri nyingine nzuri uhamie uko..


Hii ndio njia rahisi kufanikisha malengo yako...ila ukipambana kwenye ualimu wa bongo utajikuta peke yako na utachoka akili bure!

Tatizo kubwa la walimu wengi ni waoga,wanafiki na zaidi wajinga,kwahiyo ningumu kupambana ukiwa umezungukwa na wajinga...jitenge nao upambane uone mambo yako yatakavyonyooka fasta.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja kwanza sisi tuajiriwe inaonesha mlioko kwenye game wengi mnambwela kukinukishaaaaa coz mshakuaaa mababuu tulia watu wenye hasira kali tuje
 
Ngoja kwanza sisi tuajiriwe inaonesha mlioko kwenye game wengi mnambwela kukinukishaaaaa coz mshakuaaa mababuu tulia watu wenye hasira kali tuje

Kibaya utajikuta umezungukwa na walimu wajinga,itakuwiya vigumu kupambana ukiwa na wafuasi wajinga na utashindwa vita hiyo saa 12 asubuhi.
 
walimu tumekuwa na madai mengi sana serikalini na ambayo mengi yao yamekuwa yakipuuzwa ipo haja ya kuhimizana na kuweka malengo yetu na mahitaji yetu wazi zaidi na kuhakikisha yanatatuliwa bila kupuuzwa,naamin serikali ina uwezo mkubwa wa kuya tatua haya na yakaisha,angalizo cwt sidhani kama ni chombo huru kinacho weza kutatua matatizo yote ya walimu pamoja na kusimamia haki za walimu
 
Hakika baadhi ya waalimu ni waoga kupindukia,Mimi nimeshaanza kupambana kimya kimya,nimegoma kufundisha practicals za biology, coz utaalamu wa maabara ni taaluma inayojitegemea na wanapaswa kuajiriwa kwa shughuli za maabara tu,sasa leo wananitaka nifundishe darasani,na practicals niwafundishe kwa mshahara ule ule!!!!hii haikubaliki hata kidogo,waalimu wenzangu popote mlipo,kataeni upuuzi na uonevu wa jinsi hii,kwani tunaonewa na hii serikali kiasi kwamba hata serikali yenyewe inatushangaa na kutudharau kwa ukimya wetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…