Hivi waliosema "i you want to sell your freedom get married" waliwaza nini ?

Hivi waliosema "i you want to sell your freedom get married" waliwaza nini ?

Wengi wakiingia kwenye ndoa uhuru unapungua.kwa baadhi lakini asilimia kubwa.
Mfano Binti upo free kwenda kokote,kulala Kwa rafiki yako,kusafiri,kuhudhuria matamasha,hata ukirudi saa SITA usiku Ukute unaishi kwako.ila Sasa ukiolewa Kila pa kwenda utoe taarifa uombe ruhusa Kwa mume.ukichelewa tatizo.atahisi ukienda kuchepuka huko.
Kwa mwanaume pia kama uko free kwenda unapotaka,kuelewa na marafiki,kuhudhuria hata birthday ya rafiki wa kike,kusafiri nk..itabidi umjuze mkeo in details,ajue unaenda wapi na kufanya Nini Kwa mda gani.
Kuna mambo mengi kUyafanya lazima mwenzio ajue.
Na Kuna ruhusa ama kukokupewa ruhusa hasa Kwa upande wa mke maana Yuko chini ya mume.akisema hakuna kwenda ni hakuna.🤣🤣

Mwenzangu alikua kaondoka nyumbani,ana Maisha huru,kurukaruka sijui kwenye matamasha,taarab za akina Mzee Yusuf,kushindia bar wanaokunywa bia na nyama Hadi saa SITA,weekend ikifikia full midadi..na ndoa aliitaka akaolewa na mwanaume ambae Yuko kinyume kabisa na hayo Maisha.hakuna kutoka ama kuzurura labda uwe na safari inayoeleweka,huna tuliza tako hapo.
Kuna siku kaomba ruhusa aende club akacheze mziki..akaambiwa redio Hilo hapo kiwango fungulia mziki ucheze humuhumu🤣🤣🤣
 
Ukioa au kuolewa kuna possibility kubwa ya kupoteza.uhuru wa kufanya mambo ya kijinga jinga.

NB:Hii ni kwawalio oa au kuolewa na watu waliokomaa akili
 
IF YOU WANT TO SELL YOUR FREEDOM GET MARRIED
Je ni kweli kuna uhuru unapungua ukioa au kuolewa ?

Ni uhuru upi huo ?

Kuna wengine husema "no matter how boring life gets, never get married"

Kuna nini ndani ya ndoa ?

Kuna haja ya somo la umuhimu wa ndoa na familia kufundishwa vyuoni .
Kataa ndoa. Ndoa ni utapeli mamboleo.
 
Nafikiri hizi itakadi hasi kuhusu ndoa zinatokana na uwoga wa majukumu kwa vijana na roho ya ubinafsi. Ukiwa kwenye ndoa na mtu sahihi kwako na ukawa tayari kubeba majukumu,hakuna uhuru utakaokosa.
Mwisho wa siku huu ni wito ambao sio lazima uuingie,ila ni muhimu kuwa na ndoa katika wakati sahihi.
 
Back
Top Bottom