Hivi wanaotoa elimu za Ujasiriamali wao wametajirika?

Hivi wanaotoa elimu za Ujasiriamali wao wametajirika?

hawa jamaa wanaInspire sana watu unapata hamu kweli ya kufanikiwa lakin jana yeye alipata mlo kwa taabu sana.

mwanafunzi akuja na Ranger mwalimu anakuja na toyo
 
Don't take advice from someone who don't have the results that you want..[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Wapo waliotajirika na ambao hawajatajirika !! Ila kazi yao ni kukujenga ujitambue, ujue ni fursa gani inakufaa ulivyo,na kukumbusha kuwa unaweza fanya kitu ukithubutu.
Wao wenyewe kwanini hawana uthubutu huo?
 
Wengi wao hata kushika jembe hawajui,Mimi nitafundishwa na MTU niliyeshuhudia analima has a,sii hawa wa kufunga tai halafu ana kufundisha ujasiriamali
 
wale wanakufundisha njia mbadala za kuweza kutoka ulipo ukithubutu
 
Watakwambia mganga hajigangi.....

Hua nashangaa pia mganga wa kienyeji (mpiga ramli) anawapa watu utajiri ila yy ni masikini
 
Midomo yao ndo Ajira ambayo huwaingizia kipato ila anaefundishwa ndo mwenye Mali...kisa cha mchuuzi na mlanguzi kumuibia mkulima asiyeelevuka..
 
Hivi hawa wanaotoa elimu ya ujasiriamali wanautajiri kiasi gani?
na hawa wanaosema kilimo kinalipa tena mpaka wanatoa gharama zake na faida wao nao wana utajiri kiasi gani toka waanze.

ASante

Niliwauliza wauza Green House waliponitembelea hilo swali? hawakurudi
 
fundi hujenga kwa wenzake kwake kuna vuja! hata hivyo makungwi wengi ndoa zao zimevunjika
 
wanaishi kwa kuuza vitabu vyenye theory za kuokoteza na kutoza viingilio vya semina
Shigongo unamfahamu?
Lunyungu Unamfahamu?

Hawa ni watu ambao nimehudhuria semina zao, wanatoa ushuhuda namna walivyoanza.

Jambo jingine vipawa tunapewa tofauti, yupo alopewa kipawa cha kufundisha - anatumia mdomo, mwingine kapewa kipawa cha kutenda - anatumia mikono yake kufanya kazi, wote hawa wanapata kadri Mungu alivyowapangia.
 
Naamini ni vizuri kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa na sio wanaojua kuongea sana.

Hawa wakufunzi wengi wao wanaongelea nadharia za ujasiriamali ambao hawaujui. Mtu hawezi kukupa mbinu za kweli za kuingiza milioni 3 kwa mwezi huku yeye anaishia kupata laki 4 za ada za viingilio kwenye semina anazowapa. Wachumia tumbo hawa
 
Wapo waliotajirika na ambao hawajatajirika !! Ila kazi yao ni kukujenga ujitambue, ujue ni fursa gani inakufaa ulivyo,na kukumbusha kuwa unaweza fanya kitu ukithubutu.
My friend...atanifundishaje kujitambua ilhali hajitambui?
Is he earning enough....NO
Does he like to be poor...NO
Sasa iweje aniambie napoteza muda kuajiriwa utajiri uko shambani ilhali na yeye yuko huku mjini analalama kila unapochelewa kupeleka ada ya semina?

Maneno matupu ni illusions.
 
Naamini ni vizuri kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa na sio wanaojua kuongea sana.

Hawa wakufunzi wengi wao wanaongelea nadharia za ujasiriamali ambao hawaujui. Mtu hawezi kukupa mbinu za kweli za kuingiza milioni 3 kwa mwezi huku yeye anaishia kupata laki 4 za ada za viingilio kwenye semina anazowapa. Wachumia tumbo hawa
Yawezekana ikawa kweli na yawezekana ikawa si kweli ...
Mosi, tanguliza Imani Moyoni ...
Pili: Weka maarifa kichwani
Tatu: Weka pesa Mfukoni.
Pesa ni hatua ya mwisho baada ya hatua mbili za awali, Ya kwanza ni ya muhimu sana - kama unaamini kwamba inawezekana - ITAWEZEKANA TU! Kama unaamini kwamba haiwezekani - HAITAWEKANA KAMWE.

BADALA YA KUKATISHANA TAMAA TUTIANE MOYO!

Binafsi naamini yale yanayoongelewa ni ya kweli kabisa! Kabla hujajaribu usiwakatishe wenzio tamaa.
 
Back
Top Bottom