Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Nahisi nipo nje ya mada kidogo lakini sometimes wanawake tunajichanganya

Tunataka haki sawa kwa wote wakati huo huo tuna ile kauli mbiu yetu eti wanawake tukiwezeshwa tunaweza...SMH!πŸ˜”πŸ˜”

Kwanini tuhitaji kuwezeshwa wakati tuko na mikono na miguu miwili mixer ubongo kama wanaume
 

Mara nyingi mambo ya mitandaoni yanakuwa tofauti na maisha halisi
 
Mimi siyo mjuzi ila ninaeleza kile ninacho elewa mimi.

Tunapoongelea usawa tunamaanisha tuondoe ule mnaouita mfumo dume kwamba binadamu wote ni sawa kitu ambacho si kweli. Mnaouita mfumo dume ni ule unaom favor mwanaume zaidi katika nafasi mbalimbali. Lakini kiukweli huo usawa mnaoulilia hauwezi kuja kutokea kwa sababu hata mkipewa nafasi bado hamtaweza kufanya vitu ambavyo mwanaume anafanya.

Mwanaume kaumbiwa roho ya ukakamavu, uvumilivu, na kujitoa muhanga katika hatari wakati huo mwanamke ana hali ya unyonge, kulia lia kila kitu na mwepesi kukata tamaa. Sasa mtu kama huyu anataka usawa na mwanaume.

Usawa tunaoulalamikia sisi ni ule wa kuingilia mipaka yetu achana hiyo uliyoongelea hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…