Mimi naona hii haki sawa ilitokana na baadhi ya wanaume kutokutimiza majukumu yao kwa wake zao maana majukumu ya mwanaume ni kutafuta pesa na kuhudumia mke na watoto na majukumu ya mwanamke ni kufanya kazi za ndani na kulea mume na watoto ila kuna wanaume waliwanyanyasa wake zao kwa sababu walijua kuwa wake zao waliwategemea wao kwa kila kitu
Ndipo sasa wanawake wakaona kwanini wanyanyaswe wakati sisi wote ni binadamu basi na wao wakaona waanze kujitafutia pesa zao wenyewe ili wasinyanyaswe tena na ndipo haki sawa ilipoanzia sasa hii ni kwa upande wa kiuchumi
Haki sawa nyingine inayoongelewa ni ile ya kupendana, kuvumiliana, kusameheana na kuheshimiana na hii ilitokana na kwamba wanaume wengi hasa wa kiafrika wanataka wao tu ndo wapendwe, wavumiliwe, wasamehewe na waheshimiwe na wake zao ila wao hawana muda wa kufanya hayo kwa wake zao
Na wake zao wakikosea basi hao hao wanaume aidha watawapiga watawasaliti watawapa talaka au watawaongezea wake kwa kisingizio cha kuwa wao ndo wanatoa mahari kwahiyo wanaona wakishatoa tu hizo mahari kazi yao imekwisha kazi inabaki kwa mwanamke sasa kuhakikisha anafanya mengine yote kulinda ndoa je hiyo ni sawa?