Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Wanaume wa leo mnataka mpate wanawake wenye akili ya maisha na wanaojua kutafuta pesa ili wawasaidie katika kuhudumia watoto na mahitaji ya nyumbani lakini ninyi hamko tayari kusaidia kufanya kazi za ndani na kulea watoto sasa hapo hamuoni kuwa wanawake ndo wanakuwa wanafanya majukumu mengi kuliko wanaume? Kitu ambacho hakitakiwi maana mwanamke aliumbwa kama msaidizi tu kwa mwanaume
Mimi kama kiongozi ukifanya shughuli nyingi ni sawa tu lazima kuwe na utofauti Kati ya kiongozi na mfuasi
 
Sawa nashukuru umeona pia kuwa wanawake zamani tulikuwa tunanyanyasika na kuteseka je ule mfumo ulikuwa ni sahihi ukilinganisha na wa sasa?
Mfumo wa zamani sikujua ulikuwa sahihi kwa wakati ule ingawa kwa mazingira ya Sasa sio mzuri.

Kwa mfumo uliopo Sasa, Wanawake mna fursa kubwa ya kufanikiwa kutokana na fursa nyingi tu ambazo hutolewa na serikali au hata mashirika binafsi kwa ajili ya kumuinua mwanamke. Ila ukija kijamii naona hakuna tatizo Sana hasa mijini zaidi ya nyinyi kulitengeneza. Mwanamke kupigania kazi za ndani ili zifanywe na wote naona Kama halina mantiki kubwa kama waliyoyapigania mama zetu
 
Shida nyingine ni kuwa wanawake wengi hudhani wao wanafanya kazi kubwa sana kwenye familia kuliko waume zao, wengine hufikia hatua ya KUTAKA kuwaaminisha Jambo hilo watoto. Sasa Kwa ugumu wanaoamini wanaupata, wanaamini ni haki na ni lazima mwanaume asaidie majukumu ya mwanamke...!! Msaada unaotafutwa Kwa namna hii lazima upate upinzani
Kama hayo majukumu ni mepesi mbona wanaume wengi huwa mnayachukia? Tunasema umsaidie mkeo hayo majukumu endapo na yeye anakusaidia majukumu yako ila kama yeye hakusaidii majukumu yako basi haina haja ya wewe kumsaidia majukumu yake
 
Ni kwa sababu mmewatwisha majukumu yenu na wakati ninyi majukumu yao hamtaki kuyafanya
Hapana, Edelyn sio hivyo mara zote.

Naomba unikubalie kuwa kuna watu ni wavivu au hawakulelewa kujituma kufanya vitu wenyewe.Mtu wa hivi hata kama akifanya kitu kidogo tuu anaweza akasema umetwisha majukumu yote.
 
Wanaume wa leo mnataka mpate wanawake wenye akili ya maisha na wanaojua kutafuta pesa ili wawasaidie katika kuhudumia watoto na mahitaji ya nyumbani lakini ninyi hamko tayari kusaidia kufanya kazi za ndani na kulea watoto sasa hapo hamuoni kuwa wanawake ndo wanakuwa wanafanya majukumu mengi kuliko wanaume? Kitu ambacho hakitakiwi maana mwanamke aliumbwa kama msaidizi tu kwa mwanaume
basi kumbe hapo ndo huwa mnakosea mwanaume sio kwamba akisema akili ya maisha ni kutafuat pesa akisema akili ya maisha ni mwamke anayelewa kwamba kuna kupata kuna kukosa na kuna mihangaiko mingi katika maisha na pengine kutokupata kabisa na uwezo wa kukubaliana na hali hiyo ndio akili ya maisha anayitaja mwanaume kwa sababu kwa mwanaume anayejielewa mwanamke kwake ni investment katika familia...japokua sikatai kuna wanaume ambao wanajifany awao ndio wanaolewa lia sio kwamba hawajui kutunza familoa ni jukumu lao ila ni ujinga tuu walionao...kuhusu kuosha vyombo ni kwamba hebu assume wewe ni ma awa nyumbani kazi yako ni kuweka mji safi na watoto waonekane ni wenye afya halafu unakaa mpaka jioni hujaosha vyombo mtu kaja amechoka kaleta pesa ya kula unamuambia aodhhe vyombo we unaona hiyo ni haki....ukija hoj y apili system ya maisha huku africa imabedilika sana unakuta wadada pia wanaenda shule wanasoma masters degree sasa mtu keshasoma je nikimuambia akae home aache kazi alee familia atakubal jibu ni hapana ...kwa au hata wewe assume mama kawapikia halafu kaondoka anakuta hamjaosha vyombo je alikua anaachekea?
 
Mwanamke kufanya kazi ya kulea familia ni kweli ipo ila Mara nyingi hutegemeana na kwa Nini mwanaume sio muwezesuaji na lMungu asaidie mwanamke ajae ufahamu wa kuiheshimu nafasi yake Kama mwanamke ila akinyimwa kinachofuata ni maumivu kwa mwanaume.

Mimi Sina ndoa hivyo huwa sipendi kuzungumzia kitu nisicho na experience nacho japokuwa Nina uhakika roho itakuuma ukimkuta mtoto wako wa kiume anapiga deki , kuosha vyombo na kukuna nazi na mkweo akiwepo.
Roho itaniuma kama anafanya peke yake na mkwe wangu amekaa tu ila kama wanafanya wote wanasaidiana wala sina shida kwani hata kusaidiana tu napo ni taabu?
 
Hatukatai muingilie majukumu yetu na hatuwafosi au kuwalazimisha muyafanye ni nyinyi wenyewe ndo maana tunawapeleka shule mnasoma mnaajiriwa hatuwakatazi kama zamaani na kuwaacha mfanye majukumu ya nyumban tu na nyie mnapata pesa baadhi tunawaona mnakuwa ma providers kweny baadhi ya familia zenu zpo hzo ambazo mwanamke ndo mlishaj .

Ila sisi kama wanaume hatuwezi Fanya majukumu yenu sjui kupika, kuosha vyombo kulea sisi hayatuhusu mwanamke upo kwa ajilii ya kuangalia nyumba na makuzi ya watoto kiujumla pale ambapo mwanaume npo ktk shughuli za utafutaj hata kama sina kazi inajulikana mwanamke wake ni ulezi

Usawa wenu mnataka na sisi tufanye hzo kazi yaani tuoshe vyombo sjui tupike na nyie mpo huo ni uzwazwa

Mnataka muwe sawa kimaamuzi na kikauli ndani ya nyumba sasa Nani kamuoa mwenzake embu tambueni nafasi zenu na tutavuruga hadi akili zikae sawa
Sawa kwahiyo unataka mwanamke ndo afanye majukumu mengi kuliko mwanaume?
 
Mnadai isawa wakati huo mnatutegemea tuwawezeshe na kuwahudumia.

Mmekuwa na katabia cha kupenda kushindana. Yaani nikifanya hivi na wewe ufanye vile.
 
Unaweza kuchimba kaburi?[emoji3]
Ni sawa ila mimi naona kama mara nyingi wanawake ndo tunaweza kufanya majukumu yote ambayo yapo ndani ya uwezo wetu ila wanaume kuna baadhi ya majukumu hawawezi kufanya hata kama yapo ndani ya uwezo wao eti kwa sababu tu kwenye jamii yamezoeleka kuwa ni majukumu ya kike na inaonekana ni aibu kwa mwanaume kuyafanya hii imekaaje?
 
Mimi kama kiongozi ukifanya shughuli nyingi ni sawa tu lazima kuwe na utofauti Kati ya kiongozi na mfuasi
Uliona wapi makamu wa rais anafanya majukumu mengi kuliko rais? Mwanamke ukishataka afanye majukumu yako lazima atachukua nafasi yako tu utake usitake hizo nafasi wanaume hamkupewa bure bali mlipewa kwa masharti ya kutimiza majukumu yenu kwa wake zenu

Ndo maana Mungu alimwambia mwanaume atamtawala mwanamke na pia akamwambia mwanaume atakula kwa jasho lake sasa cha kushangaza wanaume wa siku hizi wengi wanataka kula hadi kwa jasho la wake zao halafu bado wanataka wawatawale wake zao hiyo haipo hata Mungu mwenyewe hakutaka iwe hivyo sasa sijui sisi binadamu ni kina nani hadi tupinge
 
Mfumo wa zamani sikujua ulikuwa sahihi kwa wakati ule ingawa kwa mazingira ya Sasa sio mzuri.

Kwa mfumo uliopo Sasa, Wanawake mna fursa kubwa ya kufanikiwa kutokana na fursa nyingi tu ambazo hutolewa na serikali au hata mashirika binafsi kwa ajili ya kumuinua mwanamke. Ila ukija kijamii naona hakuna tatizo Sana hasa mijini zaidi ya nyinyi kulitengeneza. Mwanamke kupigania kazi za ndani ili zifanywe na wote naona Kama halina mantiki kubwa kama waliyoyapigania mama zetu
Mkuu sijui kama umenielewa nimesema mwanaume amsaidie mke wake kufanya kazi za ndani ikiwa huyo mwanamke anamsaidia mumewe kutafuta pesa ila kama hamsaidii basi na yeye asimsaidie? Hivi kwani wanaume ni kipi kinachowawia vigumu kufanya hizo kazi? Mtabadilika jinsia?
 
Hapana, Edelyn sio hivyo mara zote.

Naomba unikubalie kuwa kuna watu ni wavivu au hawakulelewa kujituma kufanya vitu wenyewe.Mtu wa hivi hata kama akifanya kitu kidogo tuu anaweza akasema umetwisha majukumu yote.
Vitu vidogo kama vipi hivyo?
 
Back
Top Bottom