Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hiyo ni sababu ya mgawanyo wa majukumu yaani pesa tutafute wote ila kazi za nyumbani nifanye mimi peke yangu inakuja kweli hiyo? Ukielewa hilo utaelewa kwanini bado wanawake tunawategemea wanaume kiuchumi
Mpenzi, hivi umeshawahi jiuliza sehemu kubwa ya bajeti ya mwanamke kimatumizi huwa inaenda wapi?!
 
Uwongo hadi aliyekuumba anakushangaa unavyohalalisha unafki kuwa ukweli
Uongo uko wapi hapo mkuu? Kwani siku hizi wanaume si ndo mnawaita wanawake majina ya ajabu mara sijui wadangaji sijui wauzaji eti kwa sababu wanapenda pesa hivyo mnataka wajitafutie wenyewe siyo nyie?
 
Kama mwanamke ni mama wa nyumbani hatafuti pesa basi hastahili kusaidiwa majukumu yake na mumewe ila kama anatafuta pesa kwanini mumewe asimsaidie? Hivi wanaume mmeshajaribu kuvaa viatu vyetu na kujiuliza kuwa kama mngekuwa nyie mngeweza?

Imagine wote mnatoka alfajiri mnaenda kazini halafu wote mnarudi usiku lakini mume akirudi anakaa sebuleni miguu juu halafu mke anapitiliza moja kwa moja jikoni anaandaa chakula akimaliza anaosha vyombo halafu ndo mnaenda kulala hivi hiyo ni sawa kweli?
Hivi akatokea kaka jambazi ghafla hapo unadhani nani atacheza nae twist?!

Je, mfano nyumba ni ya kupanga, unadhani nani kodi atalipia?!

Je wadhani asilimia kubwa ya mshahara wa mwanaume huenda wapi?!
 
Ni suala la kupima tu, kwanini siku hizi ambapo haki sawa inapiganiwa sana, ndoa nyingi zinavurugika na watu wanaachana sana kuliko zamani ambapo wanawake hawakuwa na elimu, kumiliki mali na wanaume walikuwa wanaoa wake wengi lakini kuachika ilikuwa ni nadra sana.

Jibu ni moja tu, hakuna nyumba inayoweza kuendeshwa na viongozi wawili na ikafanikiwa, labda mmoja awe msaidizi.
 
Edelyn kazi gani hizo za nyumbani mnazofanya siku hizi!? Asilimia 70 za nyumba zetu za mjini zina wadada wa kazi.. kama mwanamke anafanya kazi ni wajibu wake pia kuitunza familia, hapa hakuna ubishi.. na mara nyingi wanaume hutangulia kufariki kabla ya wake zao hasa huku africa sasa mama hapo utaendeshaje familia kama uliweka akilini kwamba hiyo ilikua kazi ya mwanamme!?
 
Haki saw inawezekn kwa wazungu especially Western counties lkin huku Africa asia icho kitu n ngum Sana
Pia nahic tamaduni tu tulizo zikuta mwanamke yupo responsible San n Kaz za nyumbn kulea watto n kadharika

Pia hi sio kwa binadamu t hata wanyama females animals are the ones provide foods for their children male are created to rule
Binadamu tumeshawekewa sheria na amri na Mungu aliyetuumba tuzifuate rejea maandiko usitake kuanza kutolea mifano ya wanyama kwa sababu tu inawafaidisha wanaume hilo siyo lengo la Mungu binadamu na wanyama ni aina mbili tofauti ya viumbe
 
Dearest one. Movement ya kudai haki sawa haikusababishwa na mtu yoyote kutokutimiza majibu yake Bali ni ile Hali ya kunyanyapaliwa au kunyimwa fursa kutokana na jinsia ya muhusika.

Wanawake zamani hawakupewa fursa ya elimu, umiliki wa mali Kama ardhi au hata Haki ya kurithi mirathi ya waume zao . Pia kulikuwa na mifumo ambayo inahalalisha kunyanyasa wanawake Kama mifumo ya sheria na physical abuse. Hivi ndivyo vitu vya mwanzo kabisaa kupiganiwa

Mliokidaka hiki kitu juu juu bila kuielewa ndio mnaona Ni movement ya kutaka usawa na wanaume badala ya FURSA NA HAKI SAWA.
Hiyo hali imehatarisha sana ndoa za Watu hadi kufikia hatua Wanaume tunaogopa sana Ke wenye kazi zao, elimu 7bu hujawa na viburi na hata hawajali Waume zaidi ya kuangalia mahitaji yao wenyewe.

So kwanini walilie kufanya kazi ilihali hiyo kazi yenyewe hazina tija yoyote ktk ndoa zaidi ya kuwapumbaza kutwaa nzima kushinda kwenye mitandao, kujipodoa na kununulia viwalo vyao tu [emoji848]
 
Ndiyomaana kila kukicha yanabaki kulia lia kuachika ktk ndoa 7bu yameiga utamaduni wa kipumbavu toka nchi za magharibi nakati Bibi na Mama zetu hawakuwa hivyo ndiyomaana wadumu sana ktk mahusiano ya mapenzi na ndoa.
Kwahiyo wewe ulitaka tuweje mkuu? Mbona wanawake tukitafuta pesa hamlalamiki ila tukifanya mambo mengine ndo mnalalamika?
 
Mkuu sijui kama umenielewa nimesema mwanaume amsaidie mke wake kufanya kazi za ndani ikiwa huyo mwanamke anamsaidia mumewe kutafuta pesa ila kama hamsaidii basi na yeye asimsaidie? Hivi kwani wanaume ni kipi kinachowawia vigumu kufanya hizo kazi? Mtabadilika jinsia?
Mmmmmmhmn hapa sasa utakuwa unalenga kuachieve nini zaidi yaani?! Kama ni kuelemewa na kazi tafuta msaidizi mzee atalipia mshahara wake.

Ila sio tu kutaka kupima kama mwanaume ukiamua kumpelekesha atapelekesheka huku ni kumkosea adabu mumeo na utomvu wa nidhamu.

Mwanaume unatakiwa utazame kwa jicho la provider na protector na si vinginevyo. Atakusaidia pale inapobidi, labda ni mgonjwa, mjaumzito, umejifungua mtoto na dharula zingine ila sio kwa lengo la kupimana nae ubavu wakati akitokea nyoka hapo chumbani unarukia mgongoni kwake.... Wakija majambazi unataka yeye atoke akawavimbie, mimi kama unakuja na hizo itikadi nawalipa watu siku watuvamie halafu nione reaction yako, utakavyoweza pambana nao
...... Kama haujaingia uvungu wa kitanda....
 
Katika maelezo yako nahisi umeshatambua kwamba wanawake waliumbwa "kua wasaidizi" vice versa is never true
Ndiyo na kwa maana hiyo mfanye juu chini muhakikishe wake zenu hawafanyi majukumu mengi kuliko nyie yaani eti wewe utafute pesa tu ila mke wako atafute pesa na bado afanye kazi za ndani ni haki hiyo kweli?
 
Kwaio mama, kua msaidizi mzuri & enjoy the duty! Ndo mungu alikusudia iwe ivo,

Dont put much struggles kma vle kna mtu amekuonea. Thats nature.
Ndiyo kuwa wasaidizi na siyo kuwazidi majukumu
 
Jie ndo mnajipendekeza kuingilia mambo yetu sio Kama tunataka na hatuwakatazi mkifanya msipofanya hio ni juu yenu kama nlvyoelezea hapo awali
Wewe mke wako hata kama anatafuta pesa bado utamhudumia kama kawaida?
 
Nahisi nipo nje ya mada kidogo lakini sometimes wanawake tunajichanganya

Tunataka haki sawa kwa wote wakati huo huo tuna ile kauli mbiu yetu eti wanawake tukiwezeshwa tunaweza...SMH!😔😔

Kwanini tuhitaji kuwezeshwa wakati tuko na mikono na miguu miwili mixer ubongo kama wanaume
👍...
 
Me naomba niwaulizeni nyote. Kwani mwanamke ukapata elimu yako, ukamaliza na kutafuta kazi na ukatapata,ukasave mshahara kwenye account yako, ukafanya usafi wa nyumba kila wakati, ukafua nguo za mume wako weekend, ukamheshimu mume wako kwa kusikilizana nae na kuongea nae kwa adabu na heshima na kumpa moyo wa kutafuta na hata akikwama ukatumia pesa yako uliyosave kulipia utility za familia, na ukawa muaminifu bila kujihusisha na mtu mwingine yoyote nje ya mume wako, hivi ukafanya yote haya unapungukiwa kitu gani....
Hahahaha uko sawa mkuu hatupungukiwi kitu ila kwani na wanaume nao wakitafuta pesa na bado wakasaidia wake zao kazi za nyumbani wanapungukiwa kitu gani?
 
Izo ni sifa za wanaume wa dar,

Huku mikoani wanaume tunalima mashamba, tunapasua mbao, tunafanya kazi ngumungumu ambazo mwanamke hawezigusa!

Ndomaana uku heshima bado ipo
Ndiyo na kwa maana hiyo mfanye juu chini muhakikishe wake zenu hawafanyi majukumu mengi kuliko nyie yaani eti wewe utafute pesa tu ila mke wako atafute pesa na bado afanye kazi za ndani ni haki hiyo kweli?
 
Kwa hyo mkuu unataka tushinde jikoni, tufue, tudeki si ndio?


Daah wanawake mnaanza kutupanda vichwani
Kwani hauwezi? Unaweza ila kwanini unataka ufanyiwe? Basi kama hautaki kuyafanya tafuta pesa hudumia mkeo hata kama yeye anaweza kutafuta pesa na anatafuta pesa wewe achana na pesa zake mhudumie kama jukumu lako na uache kulalamika kuwa wanawake wanapenda pesa wewe hudumia tu
 
Tatizo ni mgawanyo wa majukumu wanaume hawataki kufanya majukumu yetu ila wanataka wanawake tufanye majukumu yao na matokeo yake wanawake tunajikuta tunafanya majukumu mengi kuliko wanaume something which is not fair I think.
But at the same time you want us to take care of you especially in the financial matters. hapa ndo nliposhindwaga kuwaelewa ni 50/50 gani mnayoitaka!
 
Sawa kwahiyo mwanamke kukusaidia wewe kutafuta pesa ndo sawa?
Unajua mimi sidhani kama kuna wanaume waliokamilika wanatafuta wanawake kwaajiri ya kutafuta nao pesa. Bali wanaume waliokamili wanataka wanawake wenye uelewa na hali ya maisha aidha awe na kipato ama la.

Sio mwanamke unafika nyumbani tu hata haujashusha pumzi anakupokea na list ya bili za utility za nyumba, sijui hakuna mafuta, hakuna mchele, umeme unaisha, frji imeharibika, tunadaiwa pesa ya maji na takataka, mtoto anadaiwa ada,nahitaji pesa ya salooni, sijui vitu gani.

Na haya mambo yote anakwambia bila kujali unatafutaje pesa au kipato chako kipoje. Ila mwanamke mwenye busara atajitahidi kusoma nyakati na kujua mume wake kwa kipato kidogo alichonacho ni mambo gani ambayo anatakiwa kumsaidia kuyamudu. Anaweza hata kufanya biashara ndogo ndogo. Mwisho wa siku hata kipato cha mume wako kama utaongea nae vizuri anawezq hata kukupatia elfu hamsini ama laki kila mwezi uweke na kuhifadhi kwajiri ya dharula.....

Ni swala mtoto wa kike kufahamu obligation zako tu haitakusumbua hata kidogo kuwa mwanamke kwa mwanaume wako.
 
Unajua kwanini wanasema hivyo? Kwa sababu wameshaaminishwa kuwa wanaume hamtakiwi kufanya hayo majukumu ila wanaume mngeonyesha nia ya kuyabeba hayo majukumu na kuyafanya kama ya kwenu hakika jamii ingezoea tu

Take this from me hakuna mwanamke asiyependa kusaidiwa ikiwa yeye anasaidia hao wanaosema mume bwege sijui kawekwa kiganjani ni exceptions chache tu ni sawa na uwepo wa wanaume ambao hawataki kabisa wake zao watafute pesa (ambapo wanaume wa hivyo siku hizi wapo wachache ukilinganisha na wanaotaka)
Hao wachache ndiyo wanaokula mema ya wake sasa.

Kuna limama flani hivi Mumewe alikopa 8,00,000/= kalifungulia Mkewe mradi wa TIGO PESA, M-PESA & AIRTEL MONEY.

baada ya miezi 6 hv, Jamaa aliuguliwa Mama Mzazi(Mama Mkwe kwa Mke) akaenda kumwomba Mkewe 50,000/= ili amtibie Mgonjwa na ndipo ndoa ilipovunjikia hapo hapo baada ya Mkewe kumjibu Mume pumba eti "Hata nami wazazi wangu wana shida kibao lkn siwasaidii hivyo basi sina hela ya kukupa" ilihali pesa ipo kibandani.

Me alienda home kujipamba aliporudi kibandani alibomoa kibanda na kichapo juu kuchukua pesa, kesi ilisuluhishwa na Wazazi wote wa pande 2 lkn Jamaa alitwanga talaka papo hapo.

Ke ni Mama wa nyumbani na Me ni Mtafutaji kwa jinsi Mungu alivyotuumba kiuhalisia kabisa.
 
Back
Top Bottom