Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Sawa ila mbona wanaume mnakubali tuingilie majukumu yenu huku hamtaki kuingilia majukumu yetu (simaanishi kubeba mimba, kuzaa watoto wala kunyonyesha watoto)? Kwanini?
kwa mfano jukumu kama lipi ambalo mwanaume anapenda aingiliwe na lipi mwanaume hapendi majukumu yenu
 
Unajua kwanini wanasema hivyo? Kwa sababu wameshaaminishwa kuwa wanaume hamtakiwi kufanya hayo majukumu ila wanaume mngeonyesha nia ya kuyabeba hayo majukumu na kuyafanya kama ya kwenu hakika jamii ingezoea tu

Take this from me hakuna mwanamke asiyependa kusaidiwa ikiwa yeye anasaidia hao wanaosema mume bwege sijui kawekwa kiganjani ni exceptions chache tu ni sawa na uwepo wa wanaume ambao hawataki kabisa wake zao watafute pesa (ambapo wanaume wa hivyo siku hizi wapo wachache ukilinganisha na wanaotaka)
Ubaya ni kuwa hata wanawake mnaamini hicho
 
Ndo maana %kubwa ya wanawake mnabaki kuwa single mom kwasababu ya kutaka usawa,,,usitake kufanana na mwaume hata siku moja mwanaume anaweza kupanga kuoa mwaka fulani lakini mwanamke hilo huwezi!mwanamke jitambue baki kwenye nafasi yako na mwanaume abaki kwenye ufalme wake.
Nadhani haujanielewa na kama umenielewa basi haujajibu swali langu nimeuliza mnaposema tunataka usawa huwa mnamaanisha tunataka usawa kwenye mambo yepi?
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ukisaidia kazi ndio inakuwa yako. Frankly speaking hata feminists hawawezi kuwashauri watoto wao kuoa wanawake wenye Tabia Kama zao
Mkuu mbona zipo ndoa ambazo mwanamke ndo anahudumia familia kwa kiasi kikubwa kuliko mwanaume na inakuwa ni kama kazi yake wakati kiuhalisia na kiutamaduni siyo kazi yake?
 
Sio wanaume wote wanaofanya udhalilishaji, japo kiafrika afrika haki za wanawake zinaminywa na kufika safari ni ndefu sana.

Sababu zipo nyingi za kimazingira, malezi, hata kiwango cha ustaarabu. Anaeweza kumdhalilisha mwanamke anaweza kumdhalilisha pia mwanamme mwenzie lakini pia itasaidia kama baadhi ya wanawake hawatojitengenezea mazingira ya kudhalilishwa.
Sawa mkuu
 
Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
Hawaitaki nafasi ya usaidizi.Wanataka na wao wawe viongozi wa familia.
 
Kama umemuelewa vizuri hoja yake na umeipenda kwanini basi wanaume hamtaki kufanya majukumu ya wake zenu ikiwa yapo ndani ya uwezo wenu?
Shida nyingine ni kuwa wanawake wengi hudhani wao wanafanya kazi kubwa sana kwenye familia kuliko waume zao, wengine hufikia hatua ya KUTAKA kuwaaminisha Jambo hilo watoto. Sasa Kwa ugumu wanaoamini wanaupata, wanaamini ni haki na ni lazima mwanaume asaidie majukumu ya mwanamke...!! Msaada unaotafutwa Kwa namna hii lazima upate upinzani
 
Jibu ni simple HAMJIELEWI, mmezidi kujiweka cheap na hamuielewi thamani yenu kabisaa. Wengi hamjui kuwa katika hii life mnatakiwa kuwa na mipaka Kama watoto wa kike ila nyie mnaona kutokuwa na mipaka ndio usasa na kustaarabika, kumbe mnaonekana wapuuzi na msiojielewa na hizo hizo kampani zenu za kiume.

Yaani sisy utakuta ni mzuri ila asifungue mdomo. Unaondoa credits zote
Sidhani kama swala la kutokujielewa ndo sababu hapo naona unatumia ule msemo wa samaki mmoja akioza wote wameoza yaani maovu ya baadhi ya wanawake unajumuisha wanawake wote?

Kumbuka siyo wanawake wote hawajielewi na unataka kumaanisha kwamba wanaume wote wanajielewa? Au wanaume wasipojielewa ni sawa tu? Je na sisi wanawake tujumuishe wanaume wote kwenye maovu ya baadhi ya wanaume? Inafaa kweli?
 
Habari za usiku huu wana JF?

Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.

Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?

Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?

Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
Hivi wewe kati ya mume na mke unataka nani akorome.
 
Binafsi ukinisikia nasema wanawake mnapenda hali sawa namaanisha MNATAKA wanaume tufanye majukumu yote, YENU na YETU.... yaani ingewezekana MNATAKA hata mimba tubebe...
Hapana huwa tunamaanisha kwamba kama tunafanya majukumu yenu basi na ninyi mfanye ya kwetu ila kama hatufanyi majukumu yenu basi na ninyi msifanye ya kwetu

Yaani hapa suluhisho lilikuwa ni kubadilisha mtazamo kama jamii yaani tuamue moja kwamba kama tumeamua kuwa kutafuta pesa ni jukumu la wote basi hata kufanya kazi za ndani pia liwe jukumu la wote

Ila kama tumeamua kuwa kutafuta pesa ni jukumu la wanaume tu basi kufanya kazi za ndani liwe ni jukumu la wanawake tu yaani wenzetu wazungu kwa asilimia kubwa wameshafanya sheria kuwa kutafuta pesa ni jukumu la wote na vivyo hivyo kufanya kazi za ndani pia ni jukumu la wote

Yaani kwa wazungu siyo ajabu mwanaume kuamka asubuhi kuandaa chai ya familia wakati mkewe kalala na wala haumwi ila kwa wabongo ni ngumu hata kama mwanamke naye anatafuta pesa na anachangia maendeleo ya familia ila bado yeye kila siku ndo awe wa kufanya kazi za ndani tu mume akifanya ni mara moja kwa mwezi tena anasema eti siyo jukumu lake anasaidia tu
 
Dearest one. Movement ya kudai haki sawa haikusababishwa na mtu yoyote kutokutimiza majibu yake Bali ni ile Hali ya kunyanyapaliwa au kunyimwa fursa kutokana na jinsia ya muhusika.

Wanawake zamani hawakupewa fursa ya elimu, umiliki wa mali Kama ardhi au hata Haki ya kurithi mirathi ya waume zao . Pia kulikuwa na mifumo ambayo inahalalisha kunyanyasa wanawake Kama mifumo ya sheria na physical abuse. Hivi ndivyo vitu vya mwanzo kabisaa kupiganiwa

Mliokidaka hiki kitu juu juu bila kuielewa ndio mnaona Ni movement ya kutaka usawa na wanaume badala ya FURSA NA HAKI SAWA.
Sawa nashukuru umeona pia kuwa wanawake zamani tulikuwa tunanyanyasika na kuteseka je ule mfumo ulikuwa ni sahihi ukilinganisha na wa sasa?
 
Ipo hivi; wanawake mnaiga mambo ya magharibi.

Hamfundwi yaani mnakiuka wajibu wenu na mnavuka kipaka kimajukumu.

Yaani, Yale yatarajiwayo yafanywe na ninyi hamfanyi yaani wajibu wenu kifupi mmesahau.

Usiniulize wajibu upi maana mambo ni mengi kiujumla kifamilia wanawake wengi hamko sawa.

Utandawazi umewaharibu
Nadhani labda ungefafanua ni wajibu upi unaomaanisha ingekuwa vizuri zaidi kuliko kuandika juu juu ila labda nikuulize tu hili swali ndugu yangu je wanaume wanaotaka wanawake wenye pesa au wenye akili ya maisha hawajaiga kutoka magharibi?
 
Mkuu mbona zipo ndoa ambazo mwanamke ndo anahudumia familia kwa kiasi kikubwa kuliko mwanaume na inakuwa ni kama kazi yake wakati kiuhalisia na kiutamaduni siyo kazi yake?
Mwanamke kufanya kazi ya kulea familia ni kweli ipo ila Mara nyingi hutegemeana na kwa Nini mwanaume sio muwezesuaji na lMungu asaidie mwanamke ajae ufahamu wa kuiheshimu nafasi yake Kama mwanamke ila akinyimwa kinachofuata ni maumivu kwa mwanaume.

Mimi Sina ndoa hivyo huwa sipendi kuzungumzia kitu nisicho na experience nacho japokuwa Nina uhakika roho itakuuma ukimkuta mtoto wako wa kiume anapiga deki , kuosha vyombo na kukuna nazi na mkweo akiwepo.
 
uko sawa ila ukweli ni kwamba wanawake wanashindwa kutofautisha kati ya haki na ubinadamu wanachokosa wanawake ni ule upendo wa kuhurumiana na kusaidian ila wao wanadhani ni haki ndio maana utasikia leo hii wanaseam tutafute pesa ila kiukweli pesa haisolve chochote kama hakuna mtu karibu yako wa kukuonesha ubinadamu na utu utakuta atatafuta pesa ila moyoni anahis bado kuna kitu kina pwaya...mfano mzuri angalia zari ni mwanamke mwenye pesa ila utakuta na yeey kila kukicha anakimbizana na wanaume mara wanaitana eti king bae...kwnye kusalitiana na kupigana kote huko ni kukosa ubinadamu amabao uliutegemea kutoka kwa mwanaume wake na akaukosa sasa badala ya kujua kinacho takiwa ni ubinadamu wao wanasema haki...its misconception kuna wanawake hapa hapa tanzania ukisema wanawake wananyanysaw atakushangaa maana ana mtu anayemjali na kumuheshimu...halafu pia ukija katika hali nyingine mwanamke n kiumbe anayependa kutukuzwa hata katika majukumu yake mwenyewe still bado atataka apewe compliments..na psychology yake na mind yake iko very complicated mfano kuna wanawke wengi tuu nilishasikia wanasema eti mwaume ambaye hamkoromie au kumtisha tisha maana ake church boy eti wanaboa sasa hapo ndio utagundua wanawake wako very complicated
Yeah hao wanawake wa hivyo wapo ila ni exceptions chache tu kama ambavyo wapo wanaume wanaopenda wanawake waongeaji kupitiliza yaani wapayukaji sana (ambapo wanaume wa hivyo wapo wachache pia)
 
Sawa ila mbona wanaume mnakubali tuingilie majukumu yenu huku hamtaki kuingilia majukumu yetu (simaanishi kubeba mimba, kuzaa watoto wala kunyonyesha watoto)? Kwanini?
Hatukatai muingilie majukumu yetu na hatuwafosi au kuwalazimisha muyafanye ni nyinyi wenyewe ndo maana tunawapeleka shule mnasoma mnaajiriwa hatuwakatazi kama zamaani na kuwaacha mfanye majukumu ya nyumban tu na nyie mnapata pesa baadhi tunawaona mnakuwa ma providers kweny baadhi ya familia zenu zpo hzo ambazo mwanamke ndo mlishaj .


Ila sisi kama wanaume hatuwezi Fanya majukumu yenu sjui kupika, kuosha vyombo kulea sisi hayatuhusu mwanamke upo kwa ajilii ya kuangalia nyumba na makuzi ya watoto kiujumla pale ambapo mwanaume npo ktk shughuli za utafutaj hata kama sina kazi inajulikana mwanamke wake ni ulezi

Usawa wenu mnataka na sisi tufanye hzo kazi yaani tuoshe vyombo sjui tupike na nyie mpo huo ni uzwazwa

Mnataka muwe sawa kimaamuzi na kikauli ndani ya nyumba sasa Nani kamuoa mwenzake embu tambueni nafasi zenu na tutavuruga hadi akili zikae sawa
 
Wanataka tufanye majukumu yao kama yapi?

Mie nachoona kiko fair ni kila mtu haijalishi ni mwanaume ama mwanamke kufanya anachoweza kufanya ambacho kiko ndani ya uwezo wake....sio eti kusubiri ooh hiki kitu anatakiwa afanye mwanamke ama kile afanye mwanaume
Kwamba mmoja akijisikia hawezi au hajisikii kufanya kitu anaacha sio??Mambo hayataenda labda mmoja ajifanye mjinga.Hii haina tofauti sana na kauli ya mwanamke mvivu anayejaribu kukataa majukumu yake kwa kauli/mbinu za kuzunguka.

Kwa mtazamo wangu inabidi mwanaume asimame kama kiongozi kwa busara kuhakikisha mambo yanaenda ipasavyo.
 
Unajua kwanini wanasema hivyo? Kwa sababu wameshaaminishwa kuwa wanaume hamtakiwi kufanya hayo majukumu ila wanaume mngeonyesha nia ya kuyabeba hayo majukumu na kuyafanya kama ya kwenu hakika jamii ingezoea tu

Take this from me hakuna mwanamke asiyependa kusaidiwa ikiwa yeye anasaidia hao wanaosema mume bwege sijui kawekwa kiganjani ni exceptions chache tu ni sawa na uwepo wa wanaume ambao hawataki kabisa wake zao watafute pesa (ambapo wanaume wa hivyo siku hizi wapo wachache ukilinganisha na wanaotaka)
Huo ndo ubwege tena hao ndo wanakaa jikoni na wake zao mapoyoyo
 
kwa mfano jukumu kama lipi ambalo mwanaume anapenda aingiliwe na lipi mwanaume hapendi majukumu yenu
Wanaume wa leo mnataka mpate wanawake wenye akili ya maisha na wanaojua kutafuta pesa ili wawasaidie katika kuhudumia watoto na mahitaji ya nyumbani lakini ninyi hamko tayari kusaidia kufanya kazi za ndani na kulea watoto sasa hapo hamuoni kuwa wanawake ndo wanakuwa wanafanya majukumu mengi kuliko wanaume? Kitu ambacho hakitakiwi maana mwanamke aliumbwa kama msaidizi tu kwa mwanaume
 
Back
Top Bottom