Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari zenu wana Jf. Naomba ushauri wenu great thinkers.. Mimi nimeolewa yapata miaka 9 sasa nina watoto watatu. Mume amenizidi umri kwa miaka mitano. Ana watoto wa nje ya ndoa wawili ambao aliwazaa kabla hajaoa. Miaka minne baada ya ndoa yetu mume wangu alipata kesi ya kumpa mimba mwanafunzi. Mama wa mwanafunzi huyo aliwahi kuwa mpenzi wa mume wangu kabla hajaoa. Hapo kesi ilikua kubwa balaa. Baada ya denti kujifungua mtoto DNA ikagoma kusoma. Kesi ikamuepuka. Ilibidi tuhame ule mji. Mume wangu akapata kazi mkoa mwingine tukaishi kwa muda wa mwaka mmoja. Kwasababu za kikazi ilibidi mimi nihamie mji mwingine na watoto wakaanza shule. Yapata miaka miwili sasa tangu nihamie mji huu na wanangu, mume wangu hataki kabisa niende kumtembelea japo kwa siku mbili. Watoto wakifunga shule wanamuomba kwenda kumtembelea. Anakataa katakata. Kwakweli nashindwa kumuelewa. Mwanzo alikua anakuja kututembelea na hela za matumizi anatuma. Sasa hata hela hataki kutuma. Nikimuuliza anasema hana. Nashindwa kumuelewa kwa kweli. Nimevumilia mengi sana ukiwemo usaliti wa waziwazi. Nimeshafuma mesej za mapenzi mara kibao tu. Zikiwa na majina yao halisi. Sasa naona uvumilivu unafikia kikomo. Nafikiria kudai talaka. Washauri wameniambia eti wanaume wote ndivyo walivyo. Nisaidieni ushauri jamani.
Hata kama wana cheat lakini wana cheat responsibly. Bila mke kuumia wala kugundua. Bila watoto kuteseka. Siyo wanaume wote, huyo ni mwanaume malaya.Usitake kujitetea, wanaume ndivyo mlivyo. Kuna posti moja humu JF tulihakikishiwa na wanaume wenyewe kwamba 99.9% ya wanaume wanacheat!
Pole sana dada kwa yalio kukuta kabla hujachukua uamuzi wowote jiulize unampenda bado au la? Kisha jiulize utawaleaje watoto wako na ulikua unawatunza vipi kipindi chote ambacho hayupo? Then fikiria uzima wako kwani mwanaume unaempenda hata afanyeje akikuhitaji kimwili unaweza ukajikuta unakubali kitu ambacho ni hatari sana kwako kiafya kisha chukua hatua za kumuacha kama unamuacha mm ushauri wangu kwako muache inauma sana ila utasahau watu wanafiwa na waume zao wanasahautena wanaowapenda sembuse hiyo takataka tupa kule ni aibu kubwa kwako hasa watoto wako wakikua na kumuona baba yao alivyo mchafu kaambali nae watoto wakikuuliza waambie inshort mlishindwana tabia waambie aliondoka rabda hakurudi that's all kingine usijaribu kuwaruhusu watoto wakamuone baba yao peke yao wanawake sisi ni makatili mno wasije wakauliwa au kuharibiwa tabia bure
Pole sanaHabari zenu wana Jf. Naomba ushauri wenu great thinkers.. Mimi nimeolewa yapata miaka 9 sasa nina watoto watatu. Mume amenizidi umri kwa miaka mitano. Ana watoto wa nje ya ndoa wawili ambao aliwazaa kabla hajaoa. Miaka minne baada ya ndoa yetu mume wangu alipata kesi ya kumpa mimba mwanafunzi. Mama wa mwanafunzi huyo aliwahi kuwa mpenzi wa mume wangu kabla hajaoa. Hapo kesi ilikua kubwa balaa. Baada ya denti kujifungua mtoto DNA ikagoma kusoma. Kesi ikamuepuka. Ilibidi tuhame ule mji. Mume wangu akapata kazi mkoa mwingine tukaishi kwa muda wa mwaka mmoja. Kwasababu za kikazi ilibidi mimi nihamie mji mwingine na watoto wakaanza shule. Yapata miaka miwili sasa tangu nihamie mji huu na wanangu, mume wangu hataki kabisa niende kumtembelea japo kwa siku mbili. Watoto wakifunga shule wanamuomba kwenda kumtembelea. Anakataa katakata. Kwakweli nashindwa kumuelewa. Mwanzo alikua anakuja kututembelea na hela za matumizi anatuma. Sasa hata hela hataki kutuma. Nikimuuliza anasema hana. Nashindwa kumuelewa kwa kweli. Nimevumilia mengi sana ukiwemo usaliti wa waziwazi. Nimeshafuma mesej za mapenzi mara kibao tu. Zikiwa na majina yao halisi. Sasa naona uvumilivu unafikia kikomo. Nafikiria kudai talaka. Washauri wameniambia eti wanaume wote ndivyo walivyo. Nisaidieni ushauri jamani.
Huna mume hapo dada (pole kwa makavu ya uso, ndo dawa itakayokuponya).
1 huruhusiwi kumtembelea wewe wala watoto
2 haji tena kuwaona
3 hatoi matumizi.
Ni nini kinachowafanya muendelee kuwa mke na mume?
Hatua ya kwanza ya divorce process ni kuishirikisha familia, then viongozi wa dini. Waeleze wazazi, kuwa hamna ushirikiano wowote, sio wa kihali wala wa kimali. Na muongee kuhusu child support. Weka mguu chini haswa, atakuwa.kawekwa kwenye rambo huyo. Akisikia unataka kumuacha ataanza kukimbizana na wewe utashangaa.
Kujibu swali lako, sio wanaume wote wako hivyo. Huyo wako tu mwenye kichwa kama doughnut tu.
Ingawa mmeo ni msiba na mbwaa usiwahukumu wanaume wote. Kama unayosema ni kweli basi mmeo ni mtu wa kuogopwa kuliko hata ukoma na ukimwi. Amelewa chupi kiasi cha kushindwa hata kujijua kama usemayo ni kweli. Kazi ni kwako kuchagua kusuka au kunyoa maana ameishatenda mengi yanayohitaji adhabu ambayo binadamu hawezi kuibuni. Kama unaona ana kuzuia kwenda kumtembelea kwanini usichukue watoto wake ukaenda kule kwa nguvu tena bila kumtaarifu ili ugundue kinachomfanya akuzuie. Uhitaji kuomba ruhusa kwenda kumuona mumeo wala watoto kwenda kumuona baba yao. Nadhani heshima na upole wako anavichukulia kama ujinga na woga kiasi cha kukuwekea masharti ya kipumbavu.Wewe naye ni mwili mmoja. Pia jitahidi uende mahakamani kutetea haki za watoto wako. Maana kama anazaa hovyo hovyo kama panya siku ya kufa utajikuta una utitiri wa watoto walio wake na wasio wake. Na kama utasema utumie kipimo cha DNA bado ni upotezaji pesa. Chukua hatua mapema. Kama utaona migongano haifai unaweza kuamua kuanza maisha yako na watoto wako na Mungu atakubarikini.
KHEE!
mamii cha kufia nini?
cha kufia nini mpenzi wangu!
hebu endelea na maisha yako kwanza bora kama mpo miji tofauti na anavokukataza usiende anakuepusha na mengi sana mpenzi wangu!AKUWACHE UPUMUWEE!
mume wa aina hii hapaswi kujumuisha wanaume wote kuwa wanafanana!
kimsingi baki mwenyewe lea watoto wako,wawili tuuu na una kazi!FUNGA MKANDA JIKAZE NYANYUKA PIGANIA FUTURE YA WANAO!
mume mjaa laana hvo si mume ati!