Hivi wanaume wengine mnawezaje hivi vitu Mimi binafsi siwezi na sitaweza kamwe

Loh, eti kipigo cha mbwa koko, hahaaaaa. Yani hapo kwa mfano utajiita mume au bwana jela?
Wanaume, wapendeni/waheshimuni na kuwathamini wake zenu. Tambueni wajibu wenu, waongozeni nao watambue wajibu wao. Ubabe hausaidii kitu.
Mwanamke anaweza kupiga goti mdomoni akasema shikamoo (moyoni anakufyonya ebu liangalie)
Hakuna jambo LA kheri kama mke kukupikia, kukufulia nk huku moyo wake ukiwa na furaha. Yani unakwenda kazini nguo zimepasiwa, kiatu kiwi inang'aa mkeo kakuandaa kwa upendo.
Maisha hayana kufokeana wala kupigana. si kwa mume wala mke, maisha ni kuelekezana na kurekebishana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…