Jamani kuna wanawake huwa kwao kuwa waaminfu kwenye ndoa ni ndoto,na pia leo narudia hili 'HAKUNA TABIA MPYA ITAKAYOONEKANA KWENYE NDOA KAMA HAIKUWEPO TOKA ENZI MTU AKIWA SINGLE' Ni kwamba huyo mwanamke tangu zamana alikua na tabia yaku-cheat na ndo maana imeendelea hata alipoolewa,wako wengi tu wenye hizo tabia,kuna dada namfahamu alikuwa ana uhusiano na mume wa mtu na huku pembeni ana serengeti boy,yule mume wa mtu alipojua akampa masharti akamryhusu aolewe lakini hakuna kuzaa na huyo aliyemwoa,ikatokea kapata mimba alipopata mimba mume wa mtu akamwambia toa nilishakwambia sihitaji uzae na huyo aliyekuoa dada wa watu akatoa mimba akasingizia kwa mumewe kuwa ni dawa alizokua anatumia wakati akiumwa malaria ndo zimesababisha itoke,hivi tunavyoongea amebeba mimba ya mume wa mtu.sasa hapo jamani utasema huyo kabadilikia ndani ya ndoa? Si ni tabia ambayo aliingia nayo na ameshindwa kuirekebisha.