Hivi wanyama walimfanya nini Mungu?

Hivi wanyama walimfanya nini Mungu?

February Makamba

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2020
Posts
2,151
Reaction score
2,983
Bahamas!

Kwasisi binadamu hapa duniani, chanzo cha kuteseka na maumivu yote tutamlaumu babu yetu Adam ambaye alikosea kula apple kule bustanini.

Sasa kwa wanyama, wao kosa lao ni nini?

Kwanini swala aliwe na chui?
Kwanini Nyumbu aliwe na Simba?
Kwanini Pundamilia wakose majani?
Kwanini Kuku wachinjwe na binadamu?

Makosa yao hasa ni nini?
Kwanini wateseke hapa duniani?
Kwanini Mungu aliwaumba waje wateseke?
Is god all merciful and Loving?

Kwa binadamu kuteseka, watu huwa wanasema, ni kipimo hapa duniani na Mungu akatupa free will ili tushinde majaribu ya hapa duniani na kwenda kula neema zote mbinguni.

Wanyama wataenda mbinguni?
Wanyama wana free will kwamba na wao wana mitihani hapa duniani?
Wanyama walimfanya nini Mungu?
 
Imeandikwa,enendeni mkavitawale ndege wanyama na wadudu.hivyo binadamu hivyo vyoote viko chini yake.wanyama kutafunana ni tamaa tuu na uroho
Kwahyo binadamu kuwa juu ya wanyama ndio riketi ya wanyama wote kuteseka?
Mungu alishindwa kuweka system binadamu akawatawala lakini hawateseki?

Hiyo tamaa na uroho inatokana na nini?
Mnyama ana tamaa au anafanya vile ili aishi?
Mungu kwanini aliruhusu wanyama wateseke?
 
Imeandikwa,enendeni mkavitawale ndege wanyama na wadudu.hivyo binadamu hivyo vyoote viko chini yake.wanyama kutafunana ni tamaa tuu na uroho
Kwanini kunguru haliwi?
Kwanini kicheche haliwi
Kwanini nungunungu haliwi
Kwanini minyoo haibanikwi na kuliwa?
 
Watakuambia na sisi wanatutesa ...si unaona wanachotufanyia tembo, simba, chui, mamba nk
Sisi kuteswa na wanyama wanaweza kusema ni kwasababu adam alikuka tunda, hivyo hiyo ni mitihani ya hapa duniani ili watakaovumilia na kumfuata mungu wakapate neema zote mbinguni....
Je wanyama nao walikula tunda? Nao wataenda mbinguni? Na wao wana mitihani hapa duniani?
 
Kwa kulingana na Biblia utaona kuwa, viumbe vyote vilitiishwa kwa Adabu wakati wa uumbaji. Mwanzo 1:26-28.

Kwa kuwa vilivyotiishwa kwako ametenda dhambi, navyo vilianguka kwenye kundi la dhambi kama imavyosema katika RUMI 8:19-22 "19. KWA MAANA VIUMBE VYOTE PIA VINATAZAMIA KWA SHAUKU KUBWA KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU. 20. KWA MAANA VIUMBE VYOTE PIA VILITIISHWA KATIKA UBATILI SI KWA HIARI YAKE, ILA KWA SABABU YEYE ALIYEVITIISHA KATIKA TUMAINI. 21. KWA KUWA VIUMBE VYENYEWE NAVYO VITAWEKWA HURU NA KUTOLEWA KWTIKA UTUMWA WA UHARIBIFU HATA VIINGIE KATIKA UHURU WA UTUKUFU WA WATOTO WA MUNGU. 22. KWA MAANA TWAJUA YA KUWA VIUMBE VYOTE PIA VINAUGUA NAVYO VINA UTUNGU PAMOJA HATA SASA.
 
Dunia ina mambo mengi sana mkuu, kuna binaadamu wanaishi kama wanyama au zaidi kwa kutumikishwa, kingono, kikazi, kiuchawi/miujiza wewe acha tu mkuu
 
Kwanini kunguru haliwi?
Kwanini kicheche haliwi
Kwanini nungunungu haliwi
Kwanini minyoo haibanikwi na kuliwa?
Mhh. Mimi nakula Nungunungu (porcupine). Kwa uhakika nyama yake ni tamu kuliko nyama ya kuku wa kienyeji.
1671036057078.jpeg
 
Hailiwi na nani? Wewe mbwa unakula? Una uhakika mbwa haliwapgi popote hapa duniani?
Huyu jamaa kama akikubali kutoka nje ya box, huenda ataacha maswali yake hayo eti mbwa haliwi, kicheche haliwi, nungunungu haliwi n.k.
 
Kwa kulingana na Biblia utaona kuwa, viumbe vyote vilitiishwa kwa Adabu wakati wa uumbaji. Mwanzo 1:26-28.

Kwa kuwa vilivyotiishwa kwako ametenda dhambi, navyo vilianguka kwenye kundi la dhambi kama imavyosema katika RUMI 8:19-22 "19. KWA MAANA VIUMBE VYOTE PIA VINATAZAMIA KWA SHAUKU KUBWA KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU. 20. KWA MAANA VIUMBE VYOTE PIA VILITIISHWA KATIKA UBATILI SI KWA HIARI YAKE, ILA KWA SABABU YEYE ALIYEVITIISHA KATIKA TUMAINI. 21. KWA KUWA VIUMBE VYENYEWE NAVYO VITAWEKWA HURU NA KUTOLEWA KWTIKA UTUMWA WA UHARIBIFU HATA VIINGIE KATIKA UHURU WA UTUKUFU WA WATOTO WA MUNGU. 22. KWA MAANA TWAJUA YA KUWA VIUMBE VYOTE PIA VINAUGUA NAVYO VINA UTUNGU PAMOJA HATA SASA.
Viumbe hawana free will wala utashi wa kuelewa chochote...Kwanini Mungu awaingize kwenye hii dhahama?
 
Back
Top Bottom