Hivi Wasafi FM hamna program manager?

Hivi Wasafi FM hamna program manager?

Kesho ya mtondogoo anakuja hamisa kusema jinsi alivyopigwa mimba na diamond mara tatu mfululizo....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ntakufa mie uwiiiih
 
Wasafi ina kipindi kimoja tu cha Sport Arena asubh baada ya hapo ni utopolo[emoji28][emoji28]
 
Ukitaka kujua haiwezi kufa na inabamba, angalia idadi kubwa ya sponsors wanaodhamini vipindi. Hii ndio tanzania ya ajabu kama ilivo ccm tuu
Inatembelea nyota ya umaarufu kunuka wa Diamond, lakini kimsingi hamna kitu cha kumvutia msikilizaji. Imagine siku ya Jumamosi kama wao wanapiga muziki tu kuanzia jana usiku hadi usiku badala ya kuendesha vipindi vya elimu ya umma na muziki hapa na pale
 
Ndo raha ya kuwa na CHAKO.
dawa yao ndogo tu msisikilize redio yao
Kinachonishangaza wao ikipigwa nyimbo ya mondi ikiisha ni kuanza kusifu na kuabudu tu na mapambio juu kumuhusu mondi......
Weledi ni kitu muhimu sana kwenye izi kazi....
Anaemuelewa dida anijuze anamuelewaje mie nimeshindwa kabisa kumuelewa naona ni mpiga makelele tu.....
 
Wasafi ndio habari ya mjini kama maji vile. Mtake msitake mtaiongelea tu.
Yes ni habari ya mjini, but inatokana na wanaosikiliza wanataka nn hasa. Wapo watu wanakaa pembeni ya radio ili mradi tu anaisikiliza. But in reality, kwa msikilizaji makini wa radio angependa sana kusikiliza content na pia kumsikiliza mtangazaji anayejua anachokiongea.

Though, hatutaki Wasafi itangaze kama Rtd, lakini tungetamani kuona mtiririko mzuri wa maongezi baina ya wafanyakazi, mada nzuri (japo hizo hizo za kijingajinga lakini zipangike basi), pia watangazaji waachie zamu ya kuongea na kuacha kubishana studio as if wanatangaza vituo tofauti.

Lakini kingine muhimu kupunguza kumsifia sana Diamond. Mimi sidhani kama hicho kituo kilianzishwa kama sehemu ya propaganda ya Diamond, ila kilianzishwa kwa ajili ya wasikilizaji. Then yanatoka wapi mambo ya kumfagilia tu Diamond mwanzo mwisho, kama siyo ushamba flani uliochanganyika na upimbi na ulimbukeni.
 
Cha ajabu kuna huyo mtangazaji Adela Tillya yaani sauti ya ki-radio Tanzania kabisa lakini kajiweka FM radio. Mtangazaji wa FM Station eti anacheka ha ha ha ha ha haaaaaaaaaa, kweli? Halafu sijui nani alimdanganya kuwa kubishana na baba levo kwenye kipindi ndiyo kuvutia wasikilizaji.
Unamaanisha Nini mkuu wangu
 
Achana na hizo redio za kihuni, TBC FM wana vipindi vingi vizuri tu, kuna makala mbali mbali zinazoenda na wakati kwenye upande wa burudani wana mchanganyiko wa nyimbo zenye ujumbe mzuri.
View attachment 1641696
View attachment 1641697
Linavyokuja swala la makala achana kabisa naa UTV wale watu wapo vizurii mnoo... hua naakaa na daftari kabisa nachukua notes
 
Hicho ki redio kina wasikilizaji wengi ni boda boda na bajaj wengi wanapenda hizo maujinga ujinga
Nadhani wanalipwa hela ndogo sana. Na mimi natabiri hiki kiredio kitaweka rekodi ya kupoteza umaarufu mapema sana kuliko redio nyingine yoyote kutokea kama wakiendelea hivi. Yaani hawana content kabisa hawa vilaza
 
Yaani vipindi watangazaji wanapiga kelele, hamna hata mpangilio. Halafu hakuna ubunifu kabisa. Yaani mtangazaji anakuja studio hajui hata ataongelea nn. Unakuta mtangazaji anasubiri upigwe wimbo wa Diamond halafu mada inaanza hapohapo ili mradi tu
Wasafi FM ni redio ya hovyo kabisa, sijuwi kwanini serikali hawaifungii. Nakiri kusema kuwa HAWANA watangazaji hata mmoja anayejitambua, kama si wote basi wengi wao ni mazezeta wasiojuwa kanuni za utangazaji.
 
Back
Top Bottom