Hivi Watanzania mnaamini uamuzi wa kupandisha bei ya vifurushi ni ya Waziri peke yake?

Hivi Watanzania mnaamini uamuzi wa kupandisha bei ya vifurushi ni ya Waziri peke yake?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Naomba niseme nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa uamuzi wa kupandisha vifurushi ulikuwa ni wa Waziri labda na TCRA tu kwasababu hili ni jambo kubwa ambalo siamini kama Waziri anaweza kulifanyia maamuzi peke yake.

Hili jambo halina tofauti na lile la kikokotoo ila tatizo watanzania ni wasahaulifu sana au ni watu wa kujitoa akili kwa malengo fulani na si kweli kwamba hawajui.

Kwa mtazamo wangu, inawezekana swala hili lilipita na kujadiliwa hata kwenye baraza la mawaziri au kuna mtu/watu wachache walikaa na kuamua hivyo huku Ndugulile akiwajibika kulitekeleza kutokana na nafasi yake.

Naamini Ndugulile anashindwa tu kusema ukweli labda kutokana na viapo vya kutunza siri au vinginevyo.

Lingekuwa ni jambo la kupata sifa, Ndugulile wale asingetajwa, bali sifa zote zingeelekezwa kwa mtu fulani, ila kwakuwa limepingwa na umma, basi zigo lote la lawama anabebeshwa waziri- hii ndio Tanzania ya leo.

Aliewaita wadanganyika hakukosea.
 
Precisely non sense. Ni ukweli mtupu ulichoandika.

Lakini ujinga wako ni kushindwa kuelewa anayefaa kuwajibishwa ni kiongozi wa kisiasa ambaye tatizo limepitishwa chini yake.
Usitegemee katibu mkuu ndiye apigiwe kelele.
 
Mpango ulikuwa kudhibiti criticism za Wazalendo dhidi ya Serikali inayojiita ya Wanyonge.
 
Precisely non sense. Ni ukweli mtupu ulichoandika.

Lakini ujinga wako ni kushindwa kuelewa anayefaa kuwajibishwa ni kiongozi wa kisiasa ambaye tatizo limepitishwa chini yake.
Usitegemee katibu mkuu ndiye apigiwe kelele.
Mnafiki na wewe ndio wale wale.

Mnamtaka awajibike huku wengine hamtaki hata wausishwe na huu uamuzi.

CCM must go.
 
Back
Top Bottom