Hivi Watanzania tunasubiri hadi labda Kiungo bora wa Ukabaji Jonas Gerald Mkude astaafu au afe ndiyo tumtunuku Tuzo kwa Kipaji chake Kikubwa?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Ndani ya miaka 12 na tokea nianze Kumuona akiwa Simba SC B ( aliyokuwa nayo Kocha Matola ) na Kupandishwa Timu ya Wakubwa mwaka 2012 mpaka leo ( 2022 ) bado sijamuona Kiungo Mkabaji wa ama Kushindana nae au hata Kumzidi.

Sishangai ndiyo maana wakiwa katika Ndege wakitokea nchini Algeria kucheza na Club Setif Kiungo Mkabaji Marehemu Patrick Mutesa Petit Mafisango akiwa amekaa Siti Moja na Mchezaji Juma Kaseja ( Kipa ) na Kiongozi wa Msafara Kassim Dewji ( KD ) aliwaambia kuwa Simba SC imtunze na imlee vyema Jonas Gerald Mkude kwani ni Mchezaji mwenye Kipaji Kikubwa na ni Hazina kwa Klabu ya Simba na hata kwa Timu yetu ya Taifa.

Najua mtakuja hapa Kumlinganisha na Vichezaji vyenu vya hovyo ( hasa Yule Mrembuaji wa Kisiwani Zanzibar ) ila bado nawaambia kuwa hajatokea Kiungo bora wa Ukabaji kwa Tanzania ndani ya miaka hii Kumi ( 10 ) kama Jonas Mkude.

MINOCYCLINE nikikisifia Kitu sikikosei.
 
Mkude Hana uwezo wa kukaba,hawezi kusogea na mpira, haluki mipira ya vichwa, Hana maamuzi ya haraka 60% ya pasi zake ni za nyuma. Hana sifa ya kucheza kiungo wa chini.
Mbaya zaidi Hana uwezo wa kupora mipira. Ni mambo ya kiswahili tu yanayo mfanya awe pale Simba mbaka leo
 
Nakubaliana Na Wewe Kabisa.
 
Kama mambo ya kiswahili wengine nao wafanye wacheze basi
 
Kama mambo ya kiswahili wengine nao wafanye wacheze basiView attachment 2193664
Inonga pekeyake anaweza kuwa alimzidi Mkude kwenye takwimu zote japokua inonga ni Beki wa Kati. Orlando ukiacha dakika 20 za mwisho muda mwingi wali plan kuzuia, maanayake viungo wote wa Simba walikua huru kuchezea mpira wanavyo taka.
Upo uwezekano zile dk 20 za mwisho wakati Orlando Wana tafuta goli Mkude ata pasi Tano hakufikisha. Zile dk za Orlando wamefunguka Mimi Mkude sikumuona kabisa zaidi ya Inonga, Wawa na mzamiru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…