ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Kuna kitu kinanichekesha sana kwa baadhi ya watu wanaomsifia Elon Musk. Yaani SpaceX ikirusha rocket, Tesla ikitengeneza gari la kisasa au kampuni zake zikileta teknolojia mpya, utasikia Elon Musk ni genius, Elon Musk katengeneza hiki, Elon Musk kabuni kile! 😂
Hivi watu wanaelewa kweli namna miradi mikubwa ya kisayansi inavyofanyika? Hiyo miradi ina timu za Aeronautical Engineers, Aerospace Engineers, Mechanical Engineers, Electrical Engineers, Software Engineers, Robotics Engineers na wanasayansi wa kada mbalimbali. Kuna watu wanakesha maabara, wengine wanafanya calculations, wengine wanadesign mifumo, wengine wanapima vifaa na wengine wanatatua matatizo ya kiufundi kila siku.
Elon Musk anaweza kuwa mwekezaji, kiongozi, mfadhili wa mradi na hata kushiriki kwenye maamuzi muhimu ya kiufundi, lakini haimaanishi kwamba yeye ndiye anayekaa na kudesign kila kitu peke yake. Cha ajabu, rocket ikifanikiwa kuruka, sifa zote zinakwenda kwa Elon Musk kana kwamba hao maelfu ya wataalamu hawapo.
Mimi simnyimi Elon Musk sifa zake za uongozi, ubunifu wa kibiashara na uwekezaji, lakini tujifunze kutofautisha mtu anayesimamia mradi na wataalamu wanaoufanya mradi huo kuwa halisi.
Wakati mwingine tunakuwa na tabia ya kumtukuza mwenye kampuni na kuwasahau watu wenye maarifa wanaofanya kazi kubwa nyuma ya pazia.