Hivi watu wanapataga wapi ujasiri wa kuiba Mali (Fedha) za umma?. Mimi siwezi hata kuiba TSh 50/=, Not to mention billions of Tanzanians

Hivi watu wanapataga wapi ujasiri wa kuiba Mali (Fedha) za umma?. Mimi siwezi hata kuiba TSh 50/=, Not to mention billions of Tanzanians

Kama wee huwezi wengine wanaweza ndio maana binadam wote sio sawa
 
Nauliza watu wanapata wapi huu ujasiri?
Je, ni kutokuwa na hofu ya mungu?
(but, viongozi huwa wanaapa kwa Qur'an/biblia)
Kichekesho zaidi ni pale hawachukuliwi hatua zozote hata wakibainika

M/mungu yupo na anawaona, ibeni lakini mwisho wa siku mtaadhibiwa na mamlaka yake

Ramadhaan kareem
Wewe unaishi nchi gani watu wanaiba makanisani na misikitini sebuse hizi za TRA.........
 
Hawa wezi wa mali za umma hawakuanzia hapo tu, walianza kuiba mitihani wafaulu wapate ajira. Ni ishara tosha elimu zao walizipata kwa staili hii hii ya wizi anzia mitihani ya elimu ya msingi, sekondari na vyuo, wame advance kuiba tangu wakiwa elimu ya chini huu ndio ukweli. Huwezi kuwa gwiji wa kukwapua mali za umma kama huna uzoefu tangu chini kwenye msingi
 
Mnajua nini Tanzani siyo masikini kiasi tunachoaminishwa. Ni vile tumeshakaririshwa basi wimbo ni Tz masikini.

Hii nchi akipatikana kiongozi ambaye kashiba, mwenye utu wa kujali binadamu wengine. Tutakuwa na masikini wachache sana.

Pesa zinavyotumbuliwa kwenye Serikali, zingethibitiwa hata hawa vijana wanaomaliza vyuo, wangeweza kupata mitaji ama aina nyingine ya kujikimu.

Humo maofisini safari meneja wa Idara anaenda kukaa nje ya nchi mwezi, pesa yake ndefu, bado Mkurugenzi wa Idara DG ndiyo usiseme na tuna Mamlaka kibao.

Tuje wenyeviti wa bodi ni kufuru, hela yake anahudumiwa kama mtoto. Hapo alishakuwa kiongozi fulani mkubwa na kastaafu ana kila kitu.

Wizi kuisha mpaka Watanzania wenyewe waamke, keki ya Taifa ni kubwa ila wanaoila ni wachache.
Kwa kodi yako, kuna watu wanaishi kama wafalme na kuna mtu ni kodi yake anaishi kwenye lindi la umasikini. Kupanga ni kuchagua....
 
Hawa wezi wa mali za umma hawakuanzia hapo tu, walianza kuiba mitihani wafaulu wapate ajira. Ni ishara tosha elimu zao walizipata kwa staili hii hii ya wizi anzia mitihani ya elimu ya msingi, sekondari na vyuo, wame advance kuiba tangu wakiwa elimu ya chini huu ndio ukweli. Huwezi kuwa gwiji wa kukwapua mali za umma kama huna uzoefu tangu chini kwenye msingi
Kwa nini unaanzia kwenye mitihani usianzie kuwa walianza kuiba nyumbani vitu vidogo kama sukari. Au ukichukua kitu nyumbani umedokoa na hujaiba?
 
Back
Top Bottom