Mnajua nini Tanzani siyo masikini kiasi tunachoaminishwa. Ni vile tumeshakaririshwa basi wimbo ni Tz masikini.
Hii nchi akipatikana kiongozi ambaye kashiba, mwenye utu wa kujali binadamu wengine. Tutakuwa na masikini wachache sana.
Pesa zinavyotumbuliwa kwenye Serikali, zingethibitiwa hata hawa vijana wanaomaliza vyuo, wangeweza kupata mitaji ama aina nyingine ya kujikimu.
Humo maofisini safari meneja wa Idara anaenda kukaa nje ya nchi mwezi, pesa yake ndefu, bado Mkurugenzi wa Idara DG ndiyo usiseme na tuna Mamlaka kibao.
Tuje wenyeviti wa bodi ni kufuru, hela yake anahudumiwa kama mtoto. Hapo alishakuwa kiongozi fulani mkubwa na kastaafu ana kila kitu.
Wizi kuisha mpaka Watanzania wenyewe waamke, keki ya Taifa ni kubwa ila wanaoila ni wachache.
Kwa kodi yako, kuna watu wanaishi kama wafalme na kuna mtu ni kodi yake anaishi kwenye lindi la umasikini. Kupanga ni kuchagua....