Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Hii tabia ipo kwa vidada vya kimasikini vinavyolipwa 100k , na buku 2 ya chipsi na juice mchana, mi nikishaona mdada kwenye duka anaperuzi simu yake yaani nikishasogea nageuka hata bila kuuliza natafuta duka la watu wazima WANAJUA wanatafuta nini. Ni vijana wa kiume wachache sana yaani 5 percent wenye tabia hizi.



Nilikakuta kengine duka la dawa kubwa sana lakini kanaangalia dj mavi kwenye simu unakauliza dawa flani ipo kanajibu uku kako bize kwenye simu pale mezani wakati mwingi huelewi kanajibu nini yaani hakakuangalii kanaangalia dj mavi na matafsiri ya uongo uongo hakajali mteja ikabidi niende kwingine nikakuta mdada kajiinamia alivyo niona akaamka kunihudumia.
 
Wewe endelea kumuona mteja ni mfungwa, mtumwa, au mwizi.
Utafika mbali na biashara yako !!!
hao wengi wao ni hawa hapa
👇
 
Wahudumu kama hao ndio chanzo cha kuharibu biashara za watu.

Wenye biashara wanakwenda kwa masangoma kutafuta dawa za kuvutia wateja huku waajiriwa wanakazana kuwafukuza.
 
simple tu mteja sio mfalme umekuja dukani kwangu shida zako mwenyewe,kama huduma yangu mbovu fungua huduma yako
 
Naelewa mteja ndiyo anae toa faida ila mhudumu sio mtumwa wa mteja Hivyo tu.

Wajibu Wangu mm Kama mfanya biashara ni kuhakikisha nakupa huduma Bora iliyo ndani ya uwezo Wangu Nita jali mda wako ila Kama nimepgiwa simu na mtu wa maana usitegemee nikate simu. As if nakuogopa ntamsikiliza muongeaji Kisha Nita mplease kwanza atulie ili niuhudumie. Kwaio ni wewe Sasa mteja usubiri kidgo ni mplease huyu Alie nipigia au uende kwingine ni juu yako.

Tatzo wabongo walalamishi mno, mnakera Sana Kama vip fungueni na nyie biashara Sasa Kama ni rahisi hivyo.
 
Tunacho ongelea Sio kujibiwa vibaya binafsi siungi mkono mhudumu yoyote kujibu vibaya mteja ila kumbuka mteja sio mfalme na mhudumu / mfanya biashara sio mtumwa wa mteja.

Ukipga Simu voda ukaanza kulalamika watakusikiliza Kisha wanakukataa ki aina.
 
Wewe umeona hiyo ni busara, nimekuja unaongea na simu kata, hudumia mteja!
Heshimu kazi yako, heshimu wateja.
Sio lazima kukata Kama unaona nakuchelewesha nenda kwingine. Kwangu mm itachukua sekunde Karibu 10 za kumstop Alie nipigia ili nikuhudumie Kama itaweza vumilia ni sawa.
 
Kuna wateja wanaweka order zao kwa kutumia simu alafu unataka akatiwe usikilizwe wewe na umemkuta…
Wateja wengine wapuuuzi Sana. Haka ka usemi ka meja ni mfalme kamewapa ujinga watu wengi.
 
Naungana na wewe mkuu.
 
Wewe endelea kumuona mteja ni mfungwa, mtumwa, au mwizi.
Utafika mbali na biashara yako !!!
Wewe mdo umetaja hayo majina ya wizi,utumwa na mfungwa ila mteja ni mteja basi . Ana haki ya kuondoka na kuhudumiwa kwingine Kama anaona kwangu hapati huduma Bora Kama atakavyo yeye.
 
Upo sawa na misimamo yako lakini kwangu mm naona ni ujinga tu yaani nimekuja dukani nakuta mdada anaperuzi sijaongea nae ata kumwambia nataka Nini afu nageuka.! nianze kutafuta duka au huduma ambapo mtu mzima atanihudumia huo mda wa kupoteza Sina.
 
Hata wamiliki ni hivyo hivyo.

Hata wale wafanyabiashara wanaotegemea kabisa mapato ya leo ili akale.

Juzi tumeita bolt ya bajaji. Akawa hafiki, ramani haisomi kwamba anakuja. Tukampigia simu. Akasema anamalizia kula na kuomba tumngoje kwanza.
 
Kuna wateja ni kero, Wengi wanaolalamika hapa hawajawai kuhudumia wateja,... angalia wadada wa migahawani, bar au grocery wanavyoteseka na wateja, mtu na kielfu tano chake anajiona mfalme full kufoka na kumpelekesha dada wa watu,....ukishakuwa na experience ya kutosha kwenye biashara waweza mtambua mteja kwa muonekano wake tu anavyoingia dukani,....wateja wa bongo hela hawana kutwa kutanga tanga kwenye biashara za watu kuleta majaribu, akuulize bei aseme una bei sana kwa fulani tunanunua hivi, utamwambia kanunue huko, kesho atarudi tena atakwambia nipe tu hivyo hivyo japo una bei weeeh!, Mara alete mazoea ya kishamba shamba hasa wanawake na vinjaa njaa vyao, mara mteja aanze kukupa darasa la biashara unayoifahamu kwa miaka nenda rudi, hapa ungefanya vile hapa ungeweka hiki,...kwa ufupi kwenye biashara yangu sibembelezi mteja NEVER,....anapotoa kihela chake anaona amekupa msaada saaaana, kana kwamba yeye hakuwa na shida na bidhaa aliyochukua....wateja wa kibongo ni pasua kichwa tu,..... kwenye biashara yangu unakuta utaratibu na wewe mteja fuata utaratibu, ukiona sieleweki baada ya kulalamika nenda kwingine, ukishindwa huko waweza itumia hiyo kama fursa ya wewe kupiga hela kwa kufungua biashara yako yenye utaratibu mzuri uonavyo wewe,..hutaki sikukuita uje, waweza kwenda kwingine....all in all, good customer care ni number one priority kwangu,..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…