Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Hata wamiliki ni hivyo hivyo.

Hata wale wafanyabiashara wanaotegemea kabisa mapato ya leo ili akale.

Juzi tumeita bolt ya bajaji. Akawa hafiki, ramani haisomi kwamba anakuja. Tukampigia simu. Akasema anamalizia kula na kuomba tumngoje kwanza.
Kwaio ulitaka aache kula aje wabebe nyie. Hujui Kama njaa ingeweza kua chanzo Cha yeye / nyie kupata ajali.
 
Naungana na wewe mkuu.
 
Huku kusini ndio mtashangaa yan wafanyabiashara hawajali wateja kabisa.
HUku wafanyabiashara wanadharau wateja asee Lindi kiboko
 
Wateja wengine wapuuuzi Sana. Haka ka usemi ka meja ni mfalme kamewapa ujinga watu wengi.
kufanya biashara zetu hizi za uchuuzi kwenye nchi ilyojaa maskini ni taabu sana, yaani wateja ni maskini wa pesa mpaka akili,...🚮🚮
 
Upo sawa na misimamo yako lakini kwangu mm naona ni ujinga tu yaani nimekuja dukani nakuta mdada anaperuzi sijaongea nae ata kumwambia nataka Nini afu nageuka.! nianze kutafuta duka au huduma ambapo mtu mzima atanihudumia huo mda wa kupoteza Sina.
Wewe ni mpumbavu
 
Kuna wateja wanaweka order zao kwa kutumia simu alafu unataka akatiwe usikilizwe wewe na umemkuta…
Swali moja. Kati ya mteja aliyepiga Simu kuweka oda na aliyekuja dukani physically kuweka oda yupi wa kumpa kipaumbele cha kwanza???
 
Mkuu hio ya kurukwa huwa tunaepusha kelele ofisini,
Anakuja mtu anaropoka mafuta ya buku mafuta ya buku hadi anapoteza usikivu, unampimia tu kisha unaendelea kuhudumia wengine kwa ustaarabu,

Point zingine tutaendelea kujirekebisha
 
Funga duka uongee na shangazi yako ukimaliza fungua utuhudumie, mwanangu huniambia samahani mama kata simu Nina.mteja nitakutafuta baadae au samahani mama kuna mteja ananipigia na hata akipiga hamuongei maana yuko busy kweli.na wateja. Lowasa (rip) alisema elimu tukaona katudharau, ukiwa na mwangaza hata wa certificate huwezi kumfanyia mteja hicho ulichokiandika, yaani nisubiri mtu amalize kuongea hapana bora nikose kabisa hicho kitu kuliko kukusubiri umalize kuongea
 
Kuondoka ni maamuzi, pia kumbuka humpunguzii Wala kumuongozea chochote.
[emoji44][emoji44][emoji44] baada ya muda unaanza kutuwekea misukule kwenye biashara wakati wewe ndio uliyefukuza wateja kwa taarifa yako akiondoka mmoja kaondoka na wateja zaidi ya kumi na je wameondoka wangapi ulioacha wakaondoka?, zidisha mara kumi
 
Mkuu hio ya kurukwa huwa tunaepusha kelele ofisini,
Anakuja mtu anaropoka mafuta ya buku mafuta ya buku hadi anapoteza usikivu, unampimia tu kisha unaendelea kuhudumia wengine kwa ustaarabu,

Point zingine tutaendelea kujirekebisha
😉😉😉😉😉😉😉
 
Swali moja. Kati ya mteja aliyepiga Simu kuweka oda na aliyekuja dukani physically kuweka oda yupi wa kumpa kipaumbele cha kwanza???
Muombe msamaha mteja aliyepo dukani endelea na simu atakuelewa, kuna simu zinazolalamikiwa nadhani umezielewa
 
Kabisa mkuu wateja wengine wana majaribu tu, ukitaka umtreat kila mteja atakavyo utaichukia biashara yako.

Kitu kinauzwa buku na hiyo bei ya chini ila yeye akija atasema pale kwa Michael tunanunuaga jero, unaona kabisa hili ni karibu sasa si aache akanunue huko ila ajabu ananunua hapohapo na akienda hiko kwa Michael atamtambia kua unaona wenzio wanauza vitu bei chee.
 
k Kaka wateja wetu wa kibongo bongo ni changamoto sana,..akikuungisha mara tatu tu,..kasheshe inaanza,....mimi naweka utaratibu wa ofisi, mteja akishindwa basi....
 
Maduka yako mengi kwanini ujihangaishe kumlazimishie mtu pesa zako ulizotafuta kwa shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…