Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Hata wamiliki ni hivyo hivyo.

Hata wale wafanyabiashara wanaotegemea kabisa mapato ya leo ili akale.

Juzi tumeita bolt ya bajaji. Akawa hafiki, ramani haisomi kwamba anakuja. Tukampigia simu. Akasema anamalizia kula na kuomba tumngoje kwanza.
Kwaio ulitaka aache kula aje wabebe nyie. Hujui Kama njaa ingeweza kua chanzo Cha yeye / nyie kupata ajali.
 
Kuna wateja ni kero,
Wengi wanaolalamika hapa hawajawai kuhudumia wateja,... angalia wadada wa migahawani, bar au grocery wanavyoteseka na wateja, mtu na kielfu tano chake anajiona mfalme full kufoka na kumpelekesha dada wa watu,....ukishakuwa na experience ya kutosha kwenye biashara waweza mtambua mteja kwa muonekano wake tu anavyoingia dukani,....wateja wa bongo hela hawana kutwa kutanga tanga kwenye biashara za watu kuleta majaribu, akuulize bei aseme una bei sana kwa fulani tunanunua hivi, utamwambia kanunue huko, kesho atarudi tena atakwambia nipe tu hivyo hivyo japo una bei weeeh!, Mara alete mazoea ya kishamba shamba hasa wanawake na vinjaa njaa vyao, mara mteja aanze kukupa darasa la biashara unayoifahamu kwa miaka nenda rudi, hapa ungefanya vile hapa ungeweka hiki,...kwa ufupi kwenye biashara yangu sibembelezi mteja NEVER,....anapotoa kihela chake anaona amekupa msaada saaaana, kana kwamba yeye hakuwa na shida na bidhaa aliyochukua....wateja wa kibongo ni pasua kichwa tu,..... kwenye biashara yangu unakuta utaratibu na wewe mteja fuata utaratibu, ukiona sieleweki baada ya kulalamika nenda kwingine, ukishindwa huko waweza itumia hiyo kama fursa ya wewe kupiga hela kwa kufungua biashara yako yenye utaratibu mzuri uonavyo wewe,..hutaki sikukuita uje, waweza kwenda kwingine....all in all, good customer care ni number one priority kwangu,..
Naungana na wewe mkuu.
 
Hivi hawa wanaoongea na simu wakati mteja anasubiri huduma ni wamiliki wa biashara au wanakuwa ni waajiliwa?

Unaenda mahala wewe kama mteja unakuta huyo anayetakiwa kukuhudumia amepachika simu sikioni yuko kwenye maongezi unakuta hata hayahusiani na biashara.

Huwa najiuliza sana juu ya watu hawa maana sioni kama wana uchungu na hizo biashara.

Hivi hawa wanakuwa ndo wenye hizi biashara au ni vibarua tu maana hawajali wateja kabisa mteja unaweza kusimama tu hapo yeye anaongea na simu au mwingine anakuongelesha wakati hajakata ile simu hana umakini wa wewe uliyepo hapo kama mteja.

Unaweza kuchukia ukaamua kuondoka zako au ukaingia kwenye shop ingine iliyo karibu lakini mwenzio wala hajali anarudi kuendelea na simu zake.

Au hawa ndo michepuko wa boss maana sidhani kama hata waifu mwenye uchungu wa bizness ya familia anaweza akawa hivi.
Huku kusini ndio mtashangaa yan wafanyabiashara hawajali wateja kabisa.
HUku wafanyabiashara wanadharau wateja asee Lindi kiboko
 
Wateja wengine wapuuuzi Sana. Haka ka usemi ka meja ni mfalme kamewapa ujinga watu wengi.
kufanya biashara zetu hizi za uchuuzi kwenye nchi ilyojaa maskini ni taabu sana, yaani wateja ni maskini wa pesa mpaka akili,...🚮🚮
 
Upo sawa na misimamo yako lakini kwangu mm naona ni ujinga tu yaani nimekuja dukani nakuta mdada anaperuzi sijaongea nae ata kumwambia nataka Nini afu nageuka.! nianze kutafuta duka au huduma ambapo mtu mzima atanihudumia huo mda wa kupoteza Sina.
Wewe ni mpumbavu
 
Kuna wateja wanaweka order zao kwa kutumia simu alafu unataka akatiwe usikilizwe wewe na umemkuta…
Swali moja. Kati ya mteja aliyepiga Simu kuweka oda na aliyekuja dukani physically kuweka oda yupi wa kumpa kipaumbele cha kwanza???
 
Mimi nikikuta
🇮🇱 Mhudumu anaongea na simu na anataka kulazimisha kunihudumia huku akiongea na simu

🇮🇱😉 Akiwa anakula hasa hasa ugali halafu anataka kunihudumia

🇮🇱 Anaosha mtoto dukani halafu anataka kunihudumia

🇮🇱Nimetangulia lakini anakuja mtu mwingine anapiga kelele Toka mbali na kinyoosha mkono kutoka hela na muuzaji akiniruka na kuanza kumsikiliza

HUWA NAONDOKA MARA MOJA NA HAPO SIRUDI TENA. Customers care kwa bongo ni tatizo kubwa
Mkuu hio ya kurukwa huwa tunaepusha kelele ofisini,
Anakuja mtu anaropoka mafuta ya buku mafuta ya buku hadi anapoteza usikivu, unampimia tu kisha unaendelea kuhudumia wengine kwa ustaarabu,

Point zingine tutaendelea kujirekebisha
 
Wakati mwingine nyie mnao jifanya mpogo sahihi ni wajinga, vitu vingine unahitaji busara ya kawaida Sana ya Nini ku complect mambo kiasi hiko.?

Huyo unae mtuhumu ana ndugu ana ana marafiki na ana hisia. Pengine unakuta unae mtuhumu kapigiwa na shangazi, dada, mama, kaka na hata rafiki pengine kapigiwa smu mda ambao alikua free, inakua ningumu mtu kumkatia simu ghafla lazima umtegee Kisha um- please sio ghafla kiasi hicho kaka.

Unapo kua na angalau na punje ya busara na hekima jaribu kuangalia hisia za mwenzako sio kila kitu kulalamika tu kama Janamke.

Mfano leo kuna mzee mmoja namfahamu hanaga mishe yeye nikama mji wake mke wake ndo mtafutaji, yeye kawa wale wazee wa mitaani (balozi) sasa Leo saa 3 asubuhi nikamkuta mtaani mie nilikua kwenye harakat zangu bahati mbaya nikawa nimemskia anasema. "Huyu wa saluni hajafungua mpaka saiv ana hela Sana, watu wengine biashara hawazijui wanadhani biashara nizao kumbe niza wananchi bila sisi biashara hazipo".

Nikasema hili lizee kazi kulalamika lenyewe biashara yake iko wapi.? Au hajui Kama kina dharula, yule mzee na wewe mtoa post ni wale wale.
Funga duka uongee na shangazi yako ukimaliza fungua utuhudumie, mwanangu huniambia samahani mama kata simu Nina.mteja nitakutafuta baadae au samahani mama kuna mteja ananipigia na hata akipiga hamuongei maana yuko busy kweli.na wateja. Lowasa (rip) alisema elimu tukaona katudharau, ukiwa na mwangaza hata wa certificate huwezi kumfanyia mteja hicho ulichokiandika, yaani nisubiri mtu amalize kuongea hapana bora nikose kabisa hicho kitu kuliko kukusubiri umalize kuongea
 
Kuondoka ni maamuzi, pia kumbuka humpunguzii Wala kumuongozea chochote.
[emoji44][emoji44][emoji44] baada ya muda unaanza kutuwekea misukule kwenye biashara wakati wewe ndio uliyefukuza wateja kwa taarifa yako akiondoka mmoja kaondoka na wateja zaidi ya kumi na je wameondoka wangapi ulioacha wakaondoka?, zidisha mara kumi
 
Mkuu hio ya kurukwa huwa tunaepusha kelele ofisini,
Anakuja mtu anaropoka mafuta ya buku mafuta ya buku hadi anapoteza usikivu, unampimia tu kisha unaendelea kuhudumia wengine kwa ustaarabu,

Point zingine tutaendelea kujirekebisha
😉😉😉😉😉😉😉
 
Swali moja. Kati ya mteja aliyepiga Simu kuweka oda na aliyekuja dukani physically kuweka oda yupi wa kumpa kipaumbele cha kwanza???
Muombe msamaha mteja aliyepo dukani endelea na simu atakuelewa, kuna simu zinazolalamikiwa nadhani umezielewa
 
Kuna wateja ni kero,
Wengi wanaolalamika hapa hawajawai kuhudumia wateja,... angalia wadada wa migahawani, bar au grocery wanavyoteseka na wateja, mtu na kielfu tano chake anajiona mfalme full kufoka na kumpelekesha dada wa watu,....ukishakuwa na experience ya kutosha kwenye biashara waweza mtambua mteja kwa muonekano wake tu anavyoingia dukani,....wateja wa bongo hela hawana kutwa kutanga tanga kwenye biashara za watu kuleta majaribu, akuulize bei aseme una bei sana kwa fulani tunanunua hivi, utamwambia kanunue huko, kesho atarudi tena atakwambia nipe tu hivyo hivyo japo una bei weeeh!, Mara alete mazoea ya kishamba shamba hasa wanawake na vinjaa njaa vyao, mara mteja aanze kukupa darasa la biashara unayoifahamu kwa miaka nenda rudi, hapa ungefanya vile hapa ungeweka hiki,...kwa ufupi kwenye biashara yangu sibembelezi mteja NEVER,....anapotoa kihela chake anaona amekupa msaada saaaana, kana kwamba yeye hakuwa na shida na bidhaa aliyochukua....wateja wa kibongo ni pasua kichwa tu,..... kwenye biashara yangu unakuta utaratibu na wewe mteja fuata utaratibu, ukiona sieleweki baada ya kulalamika nenda kwingine, ukishindwa huko waweza itumia hiyo kama fursa ya wewe kupiga hela kwa kufungua biashara yako yenye utaratibu mzuri uonavyo wewe,..hutaki sikukuita uje, waweza kwenda kwingine....all in all, good customer care ni number one priority kwangu,..
Kabisa mkuu wateja wengine wana majaribu tu, ukitaka umtreat kila mteja atakavyo utaichukia biashara yako.

Kitu kinauzwa buku na hiyo bei ya chini ila yeye akija atasema pale kwa Michael tunanunuaga jero, unaona kabisa hili ni karibu sasa si aache akanunue huko ila ajabu ananunua hapohapo na akienda hiko kwa Michael atamtambia kua unaona wenzio wanauza vitu bei chee.
 
k

Kaka wateja wetu wa kibongo bongo ni changamoto sana,..akikuungisha mara tatu tu,..kasheshe inaanza,....mimi naweka utaratibu wa ofisi, mteja akishindwa basi....
 
Hivi hawa wanaoongea na simu wakati mteja anasubiri huduma ni wamiliki wa biashara au wanakuwa ni waajiliwa?

Unaenda mahala wewe kama mteja unakuta huyo anayetakiwa kukuhudumia amepachika simu sikioni yuko kwenye maongezi unakuta hata hayahusiani na biashara.

Huwa najiuliza sana juu ya watu hawa maana sioni kama wana uchungu na hizo biashara.

Hivi hawa wanakuwa ndo wenye hizi biashara au ni vibarua tu maana hawajali wateja kabisa mteja unaweza kusimama tu hapo yeye anaongea na simu au mwingine anakuongelesha wakati hajakata ile simu hana umakini wa wewe uliyepo hapo kama mteja.

Unaweza kuchukia ukaamua kuondoka zako au ukaingia kwenye shop ingine iliyo karibu lakini mwenzio wala hajali anarudi kuendelea na simu zake.

Au hawa ndo michepuko wa boss maana sidhani kama hata waifu mwenye uchungu wa bizness ya familia anaweza akawa hivi.
Maduka yako mengi kwanini ujihangaishe kumlazimishie mtu pesa zako ulizotafuta kwa shida
 
Back
Top Bottom