Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Hii tabia ya wateja wenye nyodo hasa niliona mgahawani. Nilitoka kwenda kula, couple moja imekaa pembeni yangu.

Wakaagiza chakula, kilipofika mwanaume akaagiza kitu kimoja. Mhudumu akafikisha mwanamke naye akaagiza soda, soda ikaletwa mwanamke akaagiza tena sijui nini. Mhudumu akaleta tena mwanaume akaagiza maji. Hivyo vinaagizwa kimojakimoja. Nikawaangalia nikaona hawajawahi fanya biashara, hawawezi jiongeza kwamba wanamchosha mhudumu na wanatengeneza foleni ya huduma. Hapo akilini wana akili maandazi za "mteja ni Mflame".
 
Wako mchanganyiko
  1. Kuna wamiliki wenye akili na tabia kama za waajiriwa
  2. Kuna waajiriwa wenye tabia na akili kama za wamiliki
 
Hivyo ndivyo wanavyosemaga wakivurugana na mhudumu mwingine hatimae kuja kwako, utasikia fulani pale ana nyodo bora wewe unaongea vizuri

Ngoja kesho umnyime mkopo ataenda kwa mwingine huku akikupondea wewe

Halafu huyo huyo anaewasifia voda leo utamsikia kesho akiwaponda kwa huduma mbovu mtu akishaitwa mteja ni mla unga aliekamilika
 
nilishawahi kuandika hapa huwa sikaribishi mteja kweny duka langu,huwa sishobikei mteja kwny ofisi yangu.

wateja zangu wananijua nawajua mteja mpya akija mara ya kwanza lazima atarudi tena nasema ni lazima atarudi kwasabb nawapa huduma sahihi,

sijawahi kubembeleza mteja na siwez kubembeleza mteja.

mteja mimi ndy wananibembeleza kwasbb wanahitaji huduma yangu.

mimi huwa na dili na wateja classic ndy maana huwa nasema kabisa mteja ambaye ni msomi,sijui wanajiita watumishi wa serikali ndy pasua kichwa kwsbb pesa zao ni za bajeti unakuta anataka kukupangia jinsi ya kumhudumia na kijihela chake cha mwisho wa mwezi anacholipwa na serikali sijui taasisi.

mimi huwa na dili na wale wateja ambao ni wafanyabiashara kama mimi. hawa wateja wa kusubiri mwisho wa mwezi ni pasua kichwa inshort mimi huwa sidili nao kwasbb pesa zao bajeti
inshort huwa nawaambia kama huridhiki na huduma yangu acha ajira fungua duka lako uwe unajihudumia mwenyewe bila buguza.
 
Swali moja. Kati ya mteja aliyepiga Simu kuweka oda na aliyekuja dukani physically kuweka oda yupi wa kumpa kipaumbele cha kwanza???
Iko hivi, mara nyingi mteja anayepiga simu ni ama yuko mbali especially kama ni mara yake ya kwanza hivyo hawezi kuwa na imani kama mteja aliyepo physically. Au kama ni wa kudumu wa karibu mmekwishazoeana hatumii muda mwingi kuongea anaweka order amemaliza umekata simu.

Wote hao sifa yao ni moja, hawana muda au uwezo wa kuja kwako hivyo vilevile hawana muda wa kukata simu na kupiga tena. Na hauna muda wa kufanya bargain, kisha ukate simu, kisha uanze upya mjadala.

Mteja aliyepo dukani hata kama ni mgeni, mnajadili kitu mnakiona anakagua. Hana details nyingi za sijui lipa namba au delivery tena ikitokea anajua bei unaweza mpa huduma akalipia bila wewe kutamka neno hata moja.

Huwezi kuta tajiri anafanya complications sababu probably aliwahi fanya biashara. Njaa kali ndio hujifanya wanajua sana kinadharia, sababu kwa vitendo hawajui. Mtu ambaye aliwahi kukaa hata dukani kutazama operations hawezi lalamika sekunde kadhaa kutumika kwa simu.
 
Mkuu hio ya kurukwa huwa tunaepusha kelele ofisini,
Anakuja mtu anaropoka mafuta ya buku mafuta ya buku hadi anapoteza usikivu, unampimia tu kisha unaendelea kuhudumia wengine kwa ustaarabu,

Point zingine tutaendelea kujirekebisha
Hawajawahi fanya biashara, hawana experience wanatumia hisia.

Sometimes unakuta mtu labda mchoma chips kaja dukani kununua mafuta. Hapo kuna mteja ananunua vitu kibao vya nyumbani, mhudumu anamtoa mapema huyu wa chips sababu ni kitu kimoja na pia anazingatia uharaka wake kwenye huduma yake kule. Mteja aliyekutwa anavimba.
 
Hakunaga wateja wajuaji kama wateja wanaodai "niuzie tu kwa bei hii mimi nitakuletea na wateja wengine".

Kwanza huwa wana tabia ya kulalia bei (excuse yake anakuletea wateja wengi ambao of course hana). Hawa huwa sio loyal customers, akitokea competitor mwenye lower price wanakimbizana uko bila kujali quality na hizo kelele za customer services wanazimeza. Uko waendako hata watukanwe watanunua, mradi ni bei ya chini.

Mteja wa kutegemewa ni yule anayesimama yeye kama yeye, understanding hata issue ya return na warranty anajua haki zake na limit zake, halalii bei, na cha ajabu bila hata kampeni wala shinikizo hawa ndio huleta wateja wengine walionyooka kama wao.
 
Ingelikuwa hivyo Njombe na Makete vingekuwa mbali sn. Kwa taarifa hakuna sehemu za hovyo kihuduma km kule kwao Njombe na Makete. Wakinga unaowaona Dar wamechangamshwa na Hali halisi w ya ushindani na mchanganyiko walioukuta DSM. Kwao ni hovyo kabisa.
Kuna watu walitaka kujenga lami hadi kwao wakazuiliwa na wenye mamlaka kwa hiyo kaa kimya TU usivyovijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…