Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Hivi hawa wanaoongea na simu wakati mteja anasubiri huduma ni wamiliki wa biashara au wanakuwa ni waajiliwa?

Unaenda mahala wewe kama mteja unakuta huyo anayetakiwa kukuhudumia amepachika simu sikioni yuko kwenye maongezi unakuta hata hayahusiani na biashara.

Huwa najiuliza sana juu ya watu hawa maana sioni kama wana uchungu na hizo biashara.

Hivi hawa wanakuwa ndo wenye hizi biashara au ni vibarua tu maana hawajali wateja kabisa mteja unaweza kusimama tu hapo yeye anaongea na simu au mwingine anakuongelesha wakati hajakata ile simu hana umakini wa wewe uliyepo hapo kama mteja.

Unaweza kuchukia ukaamua kuondoka zako au ukaingia kwenye shop ingine iliyo karibu lakini mwenzio wala hajali anarudi kuendelea na simu zake.

Au hawa ndo michepuko wa boss maana sidhani kama hata waifu mwenye uchungu wa bizness ya familia anaweza akawa hivi.
 
Mimi nikikuta
🇮🇱 Mhudumu anaongea na simu na anataka kulazimisha kunihudumia huku akiongea na simu

🇮🇱😉 Akiwa anakula hasa hasa ugali halafu anataka kunihudumia

🇮🇱 Anaosha mtoto dukani halafu anataka kunihudumia

🇮🇱Nimetangulia lakini anakuja mtu mwingine anapiga kelele Toka mbali na kinyoosha mkono kutoka hela na muuzaji akiniruka na kuanza kumsikiliza

HUWA NAONDOKA MARA MOJA NA HAPO SIRUDI TENA. Customers care kwa bongo ni tatizo kubwa
 
Kumbe na wewe umeliona hili?
Leo asubuhi nimepita kwenye duka moja nikamkuta jamaa mmoja teenager hivi, nikawa namuuliza bidhaa fulani kama ipo jamaa akawa yupo bize kuongea na mtu wa nje kuhusu mpira, nikamuuliza mpaka mara tatu hata hanijali yupo bize " Nawaambia simba hamfiki popote labda arudi yesu"
Nikaona niondoke zangu labda pale sio dukani ni kijiwe cha kuzungumza mpira.
Kiukweli nimegundua hivi vitu huenda fan, talent au acquired knowledge.
###Mteja ni mfalme!
 
Inasikitisha sana kwakweli, yani kweli unaenda kufungua biashara yako afu bado unafanya mzaha na wateja?
Hao nafkiri asilimia kubwa ni waajiriwa, wana uhakika wa sallary end of the month
Ndo maana inashauriwa unapoanza biashara ikiwa katika hatua za mwanzo (growth stage) inapaswa uwepo hapo kwa zaidi ya 100%, nje ya hapo ujue bado unacheza
 
Zero customer care!, kuna kila haja ya kufundisha watu customer care wiki mbili zilizopita nilienda kwenye mgahawa nikakuta wahudumu wanalumbana mbele ya wateja huku nao wakiwa wamekaanao!!, nilifikiri ile situation nikaona kabisa hapa ni zero!.
nilitaka nimuambie yule mkubwa lkn nikaona nisije kushushuliwa maana unaweza sikia "hebu nawewe kula uende zako mengine hayakuhusu!"🤣
Si unajua tena wabongo tena wadada!.

but customer care ni muhimu kwenye biashara yoyote na muda mwengine inaweza kukupelekea pakubwa bila wewe kujua!, japo mwengine anaweza kudharau!. all in all bosses kuweni na mtindo wakutoa maarifa kwa mnaowaachia biashara zenu nawewe ulieachiwa ama kuajiliwa ni muhimu kuwa kind kwa unaowahudumia.
 
Hivi hawa wanaoongea na simu wakati mteja anasubiri huduma ni wamiliki wa biashara au wanakuwa ni waajiliwa?

Unaenda mahala wewe kama mteja unakuta huyo anayetakiwa kukuhudumia amepachika simu sikioni yuko kwenye maongezi unakuta hata hayahusiani na biashara.

Huwa najiuliza sana juu ya watu hawa maana sioni kama wana uchungu na hizo biashara.

Hivi hawa wanakuwa ndo wenye hizi biashara au ni vibarua tu maana hawajali wateja kabisa mteja unaweza kusimama tu hapo yeye anaongea na simu au mwingine anakuongelesha wakati hajakata ile simu hana umakini wa wewe uliyepo hapo kama mteja.

Unaweza kuchukia ukaamua kuondoka zako au ukaingia kwenye shop ingine iliyo karibu lakini mwenzio wala hajali anarudi kuendelea na simu zake.

Au hawa ndo michepuko wa boss maana sidhani kama hata waifu mwenye uchungu wa bizness ya familia anaweza akawa hivi.
Wengi ni waajiriwa...🙂‍↔️🙂‍↔️🙂‍↔️ Binafsi niliwah kukuta mfanyakaz wangu anaongea na simu wakati mteja anasubiri huduma,, nilimfukuza kama mbwa mda huohuo, na kumwomba msamah mteja wangu!!

Toka siku iyo nikabadilisha nyaraka za makubaliano ya ajira,nikaongeza kipengele Cha kutumia simu mda wa kazi charge yake ni umevunja mkataba mwenyewe!!!

Watanzania haswa wadada ukiwachekea wanakufukuzia wateja asubuhi TU.
 
kongole sana mkuu kwa kujali wateja wako🤝🤝
 
Hivi hawa wanaoongea na simu wakati mteja anasubiri huduma ni wamiliki wa biashara au wanakuwa ni waajiliwa?

Unaenda mahala wewe kama mteja unakuta huyo anayetakiwa kukuhudumia amepachika simu sikioni yuko kwenye maongezi unakuta hata hayahusiani na biashara.

Huwa najiuliza sana juu ya watu hawa maana sioni kama wana uchungu na hizo biashara.

Hivi hawa wanakuwa ndo wenye hizi biashara au ni vibarua tu maana hawajali wateja kabisa mteja unaweza kusimama tu hapo yeye anaongea na simu au mwingine anakuongelesha wakati hajakata ile simu hana umakini wa wewe uliyepo hapo kama mteja.

Unaweza kuchukia ukaamua kuondoka zako au ukaingia kwenye shop ingine iliyo karibu lakini mwenzio wala hajali anarudi kuendelea na simu zake.

Au hawa ndo michepuko wa boss maana sidhani kama hata waifu mwenye uchungu wa bizness ya familia anaweza akawa hivi.
Hizo nyumba ndogo za boss mkuu
 
Wakati mwingine nyie mnao jifanya mpogo sahihi ni wajinga, vitu vingine unahitaji busara ya kawaida Sana ya Nini ku complect mambo kiasi hiko.?

Huyo unae mtuhumu ana ndugu ana ana marafiki na ana hisia. Pengine unakuta unae mtuhumu kapigiwa na shangazi, dada, mama, kaka na hata rafiki pengine kapigiwa smu mda ambao alikua free, inakua ningumu mtu kumkatia simu ghafla lazima umtegee Kisha um- please sio ghafla kiasi hicho kaka.

Unapo kua na angalau na punje ya busara na hekima jaribu kuangalia hisia za mwenzako sio kila kitu kulalamika tu kama Janamke.

Mfano leo kuna mzee mmoja namfahamu hanaga mishe yeye nikama mji wake mke wake ndo mtafutaji, yeye kawa wale wazee wa mitaani (balozi) sasa Leo saa 3 asubuhi nikamkuta mtaani mie nilikua kwenye harakat zangu bahati mbaya nikawa nimemskia anasema. "Huyu wa saluni hajafungua mpaka saiv ana hela Sana, watu wengine biashara hawazijui wanadhani biashara nizao kumbe niza wananchi bila sisi biashara hazipo".

Nikasema hili lizee kazi kulalamika lenyewe biashara yake iko wapi.? Au hajui Kama kina dharula, yule mzee na wewe mtoa post ni wale wale.
 
Mimi nikikuta
[emoji1134] Mhudumu anaongea na simu na anataka kulazimisha kunihudumia huku akiongea na simu

[emoji1134][emoji6] Akiwa anakula hasa hasa ugali halafu anataka kunihudumia

[emoji1134] Anaosha mtoto dukani halafu anataka kunihudumia

[emoji1134]Nimetangulia lakini anakuja mtu mwingine anapiga kelele Toka mbali na kinyoosha mkono kutoka hela na muuzaji akiniruka na kuanza kumsikiliza

HUWA NAONDOKA MARA MOJA NA HAPO SIRUDI TENA. Customers care kwa bongo ni tatizo kubwa
Kuondoka ni maamuzi, pia kumbuka humpunguzii Wala kumuongozea chochote.
 
Back
Top Bottom