Mkuu haiwezekani kwa sababu hiyo hiyo kuwa tunajaribu kuishi kama wazungu.. huwezxi kubadilisha mazingira ya Serengeti anakoishi Simba ili kumwezesha simba huyo huyo aishi kama Bear wa Vancouver, pamoja na kwamba wanyama wote hawa wana mahitaji sawa ya Kinyama.Shule ya kinadharia haitanishawishi mimi. Kitakachonishawishi ni sisi Miafrika kufanya kweli na kuanza kuishi maisha bora kama mizungu. Longolongo nyingi hazitatui matatizo yoyote.
Haya nendeni kule Mbinga mkajenge shule bora zenye viti na sio wanafunzi kukaa chini kwenye vumbi. Is that too hard?
Sisi kama Simba tutayatengeneza mazingira yetu kutuwezesha sisi Simba kuwinda kwa urahisi ktk mazingira haya haya na sii kuibadilisha Serengeti inaze kuwa na snow ili nasi tunanze kuwinda samaki Salmon.
Siku tutakapo elewa kwamba sisi tunaishi Serengeti na shule yetu itakuwa kujifunza mazingira ya Serengeti, kuwafundisha watoto wetu jinsi ya kuwinda ndani ya mbuga zetu badala ya kupendelea kusoma elimu ya Ulaya inayotufundisha sisi kucheza katika Zoo na sarakasi za Ulaya ni vigumu kuyabadilisha maisha ya Waafrika.
Nimekwisha sema hata Elimu tunayoipata nyumbani ni Elimu tegemezi ya Ulaya kwenye kila kifaa cha kutuchezesha sarakasi ndio maana wasomi wetu wameshindwa hata kutengeneza sindano.. tunashindwa hata kutengeneza Baiskeli ya kurudi nyuma, bajaj zinaagizwa toka India na kadhalika.
Nchi ina joto kali lakini tunashindwa hata kutengeneza Humidfier ya kupunguza joto ndani ya nyumba zetu kitu ambacho kinatengenezwa kirahisi kabisa na motor ndogo ya feni..Badala yake tunajenga nyumba sawa na za Ulaya zenye fire place, sauna na kadhalika. Imean hivi kweli mkuu wangu kuna haja ya kujenga nyumba yenye indoor garage?.. hatuna snow wala hali mbaya ya hewa inayoweza athiri bodi la gari tukiegesha magari yetu nje na pembeni ya nyumba..lakini kwa sababu tu Ulaya wanafanya hivyo basio nasi tunajenga nyumba zetu kama za Ulaya, ceramic tiles hadi living room wenyewe wakisema ni Marble..Haya ndio maendeleo ya mtu mweusi..
Tutakapo weza kupanga vipaumbele vyetu tukasoma na kuelewa nini mahitaji yetu (matatizo) bila shaka tutaweza kuwa na maendeleo yetu.. Maisha bora siui lazima watu wote wale kwa visu na kuvaa suti..Maisha bora sii lazima tule kwa vijiti kama Wachina..
Waziri mkuu Pinda kasema kidogo tu kuhusiana na vazi la suti, Miafrika tumekuja juu vibaya sana hali tukijidai sisi sio Ndivyo Tulivyo - Malimbukeni wa Kuiga.
First we have to accept who we are na kisha kuboresha mazingira yetu ili kumwezesha kila Mtanzania kumudu mahitaji muhimu na yenye manufaa..