Kuna maaskari wengi mno wako polisi, jeshi, hata usalama ambao watoto wao au watoto wa ndugu zao hawana ajira au wadogo zao hawana ajira.
Hii movement ya watu wasio kuwa na ajira ndio maana hata ccm wanaiogopa. Maana inawaathiri hata watoto watu wa vyombo vya dola. Je kutokana na Ukosefu wa ajira wa watoto wao wakiamua kukataa kutumika kuiba kura, ccm watakuwa wa mwisho kabisa kwenye uchaguzi
Vijana wa Tanzania ni wapumbavu sana .
Wiki mbili zilizopita zoezi la kuhakiki daftari la mpiga kura limefanyika kisanii kwa malengo maovu ya mchengerwa,tume , CCM na serikali yake .
Vijana wakakaa kimya eti hawahangaiki na siasa .Wazee wa vijijini na mijini wenye makazi ,wastaafu ,wasanii wa Singeli na Machawa pamoja na marehemu wanaandikishwa Fasta kwa siku tano zoezi likafungwa . Mamilioni ya watu walioko hai na wasio na anuani maalumu hawakuandikishwa kutokana na muda kuwa mfupi .
Vijana waliopaswa kuhamasishana na kupinga zoezi hilo kufanyika kwa muda mfupi wakadhani kuwaserikali itawaletea ajira majumbani kwao wakidhani nao ni ukoo mmoja na Abdul.
Wakasahau kuwa nguvu ya CCM ipo kwenye janja janja wakati wa kujiandikisha .
Iko hivi CCM inajua wazi kuwa daftari la mpiga kura haliko sawa kwasababu kuna watu wengi waliokufa . Lakini pia vijana wengi hawajiandikishi au kuhusisha taarifa zao. Matokeo yake CCM inatumia idadi ya wanachama wake wanaofukia mil.12( pamoja na wanachama waliokufa ) kupata ushindi wa kimbunga .
Vijana wapo zaidi ya mil .28 ,hawa walijiandikisha CCM itashindwa vibaya mno kila Sehemu kuanzia udiwani mpaka urais . Hata wizi wa kura utashindikana maana itabidi waibe kura mpaka kufikia mil. 60 ndio washinde kwa angalau 52%.Jambo ambalo haliwezekani.
Vijana wakijiandikisha wote hata Rushwa anazotoa Mama yule zitashindikana maana ni vigumu kuhonga watu zaidi ya mil . 35 . Rushwa za pikipiki zingefeli maana watu elfu 17 ni wachache sana .
Kama vijana wote wangejuandikisha CCM isingetufanyia uhuni wanaofanya .
Ni wazi kuwa vijana wengi wasiojiandikisha ni waoga na wanaodhani kuwa siasa muda wowote inaweza kuwaletea matatizo hata ya kusingiziwa . Hivyo wanaamua kujitenga na siasa mpaka kupiga kura wanawaachia Machawa . Matokeo yake ni kuwa na serikali inayotegemea kuchaguliwa na kundi la watu wasiokua na shida ya ajira wala pesa . Pesa sasa zinatumika kuhonga wetu badala ya kujenga viwanda vinavyotoa ajira .
Wanatoa rushwa badala ya kutoa mitaji kwa Vijana wasomi wenye ujuzi ili wazalishe.
Wanatoa rushwa badala ya kupunguza bei za bajaji na pikipiki ili vijana waweze kupata faida na kuajiri wengine.
Wanatoa rushwa badala ya kupunguza bei ya pembejeo za kilimo kama matrekta na mbegu na madawa ili Wafanyabiashara wauze kwa bei ya ushindani badala ya huu ufisadi wa wizara kuhadaa umma na kupiga pesa za Ruzuku .
Hivi Ruzuku ya Mbolea inamnufaishaje mkulima wa kijijini anayetumia mbolea ya Samadi na kutegemea rutuba ya ardhi yetu tuliyopewa na Mungu mwenyewe. ?
Wao wanatuuzia mbegu za kutengeneza zilizoweza kuzaa bila madawa halafu wanatuuzia mbolea kwa Hadaa kuwa ina Ruzuku ya serikali .
Nchi yenye Ng'ombe ,kuku ,mbuzi , na watu mamilioni halafu inashindwa kupata mbolea ya asili ni nchi yenye watawala na mipango ya hovyo kabisa.
Madampo yanajaa uchafu na mbolea za ng'ombe na pampasi za mbolea safi kabisa halafu wanatumia mabilioni ya pesa kuagiza mbolea kutoa Ulaya kifisadi badala ya kuagiza viwanda vya kukusanya taka na kujitengenezea mbolea safi ya asili isiyo na madawa mangi .
Vijana wamelala ndio maana hawa wazee akina Wasira wanawakejeli na kulitumia jeshi la polisi kuwatisha . Na kwa sababu ya ugumu wa maisha basi polisi nao wanawaza familia zao na kuamua kuwafurahisha wazee waliohujumu nchi hii kwa kiwango kikubwa sana na kuwapandikiza watu wao ili waendelee kulinda mali zao.
Ni wazi kuwa Samia hakubaliki Mbinguni na dunia kuitawala Tanganyika kwa mgongo wa Tanzania . Sio kwao Oman wala Zanzibar anapoweza kuchaguliwa kuwa amiri jeshi mkuu na kuwatawala wanaume mil.30 .Lakini alipogundua kuwa Watanganyika wanapenda rushwa na ubinafsi basi amejikuta kwenye rushwa ili sasa watawala kwa manufaa ya kundi linalokula kwa urefu wa kamba yake. Anajua wazi kabisa kuwa wa Munjibu wa vitabu vyote vya dini zote na mapokezi na mila zote za viumbe vyote wa porini na wa kufugwa na pia mwenyezi Mungu hata Mizimu haimkubali kuendelea kuwa mtawala wa Nchi huu yenye watu mil.65.
Matokeo yake anatumia rushwa rushwa rushwa kuhakikisha anatawala kwa pesa kupitia chama cha mafisadi .
Wale mafisadi wanaofadhili watawala ili wapate fedha za Rushwa wananufaika kwa kukwepa kodi au kuuziwa kila kitu wanachokitaka .
Sasa inapotokea nchi inaelekea kupata Rais mzalendo basi Mafisadi wanaanza kuficha pesa zao au kufadhili vikundi vya kigaidi au wauaji na watekaji ili kuvuruga nchi maana siku zote mafisadi wanapoona sheria zinawabana kwao ni hasara kubwa sana na maumivu makubwa.
Tukirudi kwenye zoezi la kujiandikisha ni wazi kuwa uhuni unaanzia kwenye daftari la mpiga kura .
CCM wanapoona waliojiandikisha ni wachache basi ni wazi kuwa hata pakiwa na tume huru kutoka Marekani watashinda kwa kura halali kabisa .
Hatima ya nchi yoyote duniani ipo chini ya vijana .
Lakini kwa Tanganyika vijana wengi wamejawa na ubinafsi .Kila mmoja anawaza kuwa akishapata mlo wa siku basi hakuna tena suala la kuwa na serikali yenye kujenga mifumo bora ya kijamii ,kisiasa na kiuchumi ili pawe na ajira kwa wengi .
Tanganyika vijana wamelala wanasubiri wachaguliwe viongozi na wabibi na wababu wa kule vijijini ambao hawaoni shida wanapoona kijana wao hana ajira . Zaidi wanapoona mtoto wao hana ajira wanaenda kwa mganga na kuloga kila mtu asipata ajira wawe sawa.
Wazee wasiojua kuwa Serikali imefeli kabisa.
Serikali ya watu madhalimu inafurahia kuona vijana wapumbavu wanapoongezeka na wakati
mwingine kwa dharau kubwa wanatwa wavivu wasiotaka kujiajiri.
Kilichobaki sasa ni kumwachia Mungu aliyetuweka kwenye Taifa hili ili aamue kama yanayofanyika ndiyo mapenzi yake au ni mafisadi wanaweka mifumo yao na watawala wa kuwanufaisha wao huku mamilioni ya wanyonge wakiumizwa makusudi ?
Mungu atajibu kwa moto na siku sio nyingi CCM watasambaratika na chama kufa na kupotea kabisa kama Miji na tawala za babiloni , farao na biashara ya watumwa ilivyopotea duniani