Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,942
- 18,669
Hahaa dah hadi ukasahau kilichokupeleka ukaanza kuwafuata wanakoenda[emoji13] [emoji13]Kuna warembo fulani mapacha weusi nilikutana nao uhamiaji daah. Aseeh ni wazuri ni weusi wa kun'gaa halafu wazuri hadi nilisahau kilichonipeleka.
Watu weusi wakiwa wwazuri wanakuaga wazuri haswa.
Huko kuwafuata umeongezea wewe.Hahaa dah hadi ukasahau kilichokupeleka ukaanza kuwafuata wanakoenda[emoji13] [emoji13]
Basi deka hata kikorea basi kama umeshindwa kunipa moyoMpaka ukajua kama mapacha ni wazi uliwafuata teh.. mimi huo uzuri niutoe wapi wewe kama unanikubali nikubali kama nilivyo tu
Huyo babako Hana jina la ukoo?Hapo sasa unakuwa unatuonea let's say mi naitwa Josephine na baba yangu anaitwa Goodluck, nifanyeje? Nichukue jina la jirani?
Hakuna sababu wengi wanaona ni ushamba kumbe wao ndo washamba.Sawa mkuu ila huwezi kujua mtu ana sababu gani za kutotumia jina ukoo
Hapana,hawa ni vijana wa kwanza 1985 Na kuendelea.utakuta baba yake anaitwa John Chenge,yeye akiitwa Frank,basi ataishia kuandika Frank John lakini kiuhalisia hakuna Mtanzania peyote mwenyewe majina tupu ya kigeni,kwani hakuna ukoo wa Kitanzania ulio Na jina la kizungu.Aibu mno!
Tena sasa hivi nadhani huo mtindo ndo umeshika kasi sana.
Zamani walau moja ya majina ya mtu lilikuwa lazima liwe lile la ukoo.
Lakini siku hizi sivyo kabisa.
Ukitaka kuliona hilo kwa wingi basi angalia matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa shule za sekondari au angalia orodha ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.
Yaani mtu unayasoma hayo majina hadi unaanza kuona aibu kabisa.
Hapo kwenye majina pananikera sana, unakutana na mtu mzima bila aibu eti anaitwa Peter Paul au Mohammed abdallah, seriously!! Hii ipo zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile Africa. Nigeria ni aibu mtu kuwa na jina la kigeni hata mnigeria azaliwe wapi ataitwa Babatunde, Yemi na majina yao ya asili hali kadhalika South Africa wanatumia sana majina yao, wakenya pia ni sisi tu ndo tumekengeuka.
Kuna mtoto mtanzania toka Mwanza mwaka jana alienda UN kuhutubia anatumia majina mawili yote ya kigeni hadi wale watu walimshangaa. Nilikua naangalia TV ila niliona aibu peke yangu.
Ni wabongo tu ambao wakienda mbele kama anaitwa Musa atajiita Moses, Hashimu Thabiti kawa Hasheem Thabeet. Tumekuwa whitewashed hadi aibu
Naona hiyo picha ya kwanza alikuwa depo kisha ya pili ndiyo baada ya kumaliza depo na kupumzika ss ameng'araHabari zetu warembo na watanashati.
Hii tabia imeota mizizi sasa sijui kwa nini wanawake tunakuwa hivi...tena siku hizi vipodozi vya kubadilisha rangi vinatangazwa hadharani kabisa afadhali siku za nyuma watu walikuwa wanajichubua kwa kujificha.
Hivi ni kweli hivi vipodozi vya kubadilisha ngozi havina madhara kiafya? Kama vina madhara mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuwashughulikia wanaofanya biashara hizi? Kwa kweli nashindwa kuelewa hivi huyu dada ukimuangalia picha yake ya kushoto na kulia kuna tofauti yoyote?
Ipo inayovutia kuliko nyingine? Mimi naona mtu ni yule yule tu nothing more nothing less. Naombeni maoni yenu wadau
View attachment 526690
Duh hapo kwenye majina. Kuna jamaa alikua classmate wangu chuo, ni mpare lakini majina yake sasa...yote matatu ni ya kigeni, kuna siku prof. Alibidi aulize kwani we ni mdanishi...Ndiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.
Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.
Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?
Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?
Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!
Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!
Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.
Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.
Ni ndivyo tulivyo tu.
Huna jina la ukoo kama (Maganga, Mwakipesile, Ngonyani etc)!?Hapo sasa unakuwa unatuonea let's say mi naitwa Josephine na baba yangu anaitwa Goodluck, nifanyeje? Nichukue jina la jirani?
Habari zetu warembo na watanashati.
Hii tabia imeota mizizi sasa sijui kwa nini wanawake tunakuwa hivi...tena siku hizi vipodozi vya kubadilisha rangi vinatangazwa hadharani kabisa afadhali siku za nyuma watu walikuwa wanajichubua kwa kujificha.
Hivi ni kweli hivi vipodozi vya kubadilisha ngozi havina madhara kiafya? Kama vina madhara mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuwashughulikia wanaofanya biashara hizi? Kwa kweli nashindwa kuelewa hivi huyu dada ukimuangalia picha yake ya kushoto na kulia kuna tofauti yoyote?
Ipo inayovutia kuliko nyingine? Mimi naona mtu ni yule yule tu nothing more nothing less. Naombeni maoni yenu wadau
View attachment 526690
Ishu ya jina la ukoo kuna changamoto zake hasa sehemu za vijijini ambapo watu wa ukoo mmoja mnajikusanya. Unaweza kuta kijiji kizima kina Ngonyani watupu kwa hiyo kuepuka saresare ya majina mtu anaamua kutumia jina la kwanza la babaHuna jina la ukoo kama (Maganga, Mwakipesile, Ngonyani etc)!?
Tumia matatu hapo probability ya majina saresare inakua ndogo mno.Ishu ya jina la ukoo kuna changamoto zake hasa sehemu za vijijini ambapo watu wa ukoo mmoja mnajikusanya. Unaweza kuta kijiji kizima kina Ngonyani watupu kwa hiyo kuepuka saresare ya majina mtu anaamua kutumia jina la kwanza la baba