Ni aibu mkuu. Naona pia Jayden na Sean yamekuja kwa Kasi sana hapa katikati
Wamarekani weusi miaka ya 70 hadi early 90s walipoanza kuamka na kutaka kurudisha tamaduni zao walizopoteza walianza kwanza kwa kubadili majina yao, hapo Ndo unakutana na weusi wanaitwa Kanye, Talib Kweli, Tay Nyerere Zonday, Kenyatta, Kenya, Malaika, Kwanzaa nk. Kuna wengine walianza hadi kujifunza lugha za Africa hasa Swahili na lugha za Africa Magharibi
Wamarekani weusi hawakuwa na uamuzi wa kubadili majina yao walibadilishwa kwa lazima kipindi cha utumwa ila sisi leo tunayakimbia kwa hiari na in a few years to come tutaanza kuitwa Yee, Cheng, Yung majina ya kichina since China is taking over.