Hivi Wizara ya Afya bado ipo?

Hivi Wizara ya Afya bado ipo?

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Hivi Wizara ya Afya bado ipo? maana imekuwa kimya sana kama vile kila kitu kiko sawa.

Mimi binafsi ninachokiona kwenye wizara hii ya afya ni kama ka mgomo baridi vile,

Nikisikiliza kwenye mitandao ya kijamii naona wanasiasa ambao hawana timu za kuchezea msimu huu wa 2020/2025 wakizusha tafrani na kudai matangazo. hawa unaweza kuwaelewa kwamba wanatafuta usajiri pengine sijui.

Lakini kwa wizara ya afya najiuliza kuna nini?

Mara kadhaa nimesikiliza viongozi wa nchi hii wakisema "kuna matatizo ya upumuaji" na kuongeza "watanzania tuchukue tahadhari" na tutumie njia zetu za hapa kupambana na haya.

Kwangu mimi msimamo huu wa serikali maagizo tosha kwa wizara ya afya kufanya kampeni kabambe za kuhamasisha wananchi kujikinga na matatizo haya ya kupumua na kupambana kwa kutumia dawa zetu.

Msimamo wa serikali haijalishi kila mtanzania anaukubali au haukubali, haijalishi kama jamii za kimataifa zinaukubali au haziukubali

Kitu kikubwa kinachotizamwa ni matokeo na matokeo hayatokani na matamko ya serikali bali ile kazi inayoanzia wizara ya afya na kusambaa kwa kila Mtanzania.

Ila kwa kile ninachokiona ni kama Wizara ya Afya kuna watu hakubaliani na msimamo wa serikali pengine na wameamua kukaa kimya ili kuiprove wrong serikali yetu, nalazimika kuwaza hivyo.

Wizara ya afya ndiyo ya kuzima kelele au kutishana tunakokusikia mitaani na sio matamko ya serikali.

Hawa ni kuelimisha watu matatizo haya ya upumuaji yanasambaa kwa njia gani na kusisitiza watu kujikinga na hasa hili ndilo lenye nguvu.

Kuna maelekezo mengi mitandaoni ambayo wizara ingetolea ufafanuzi

Kuna orodha ya madawa sijui aspirin junior, sijui azuma, sijui amoclave, n.k

Hivi matumizi sahihi ya hizi dawa ni yapi? maana kinachoendelea mitaani ni kichwa kikigonga mtu anakimbia ananunua Aspirin junior na kumeza. Wafamasia hawatuelezi habari za kutosha maana ukienda wanakuandikia tumia 1 x 1 kwa mda gani sijui.

Je, dawa hizi unaweza kuchanganya ipi na ipi? hatujui, mtu unaweza kumeza zote kumbe inatakiwa aina kama mbili au tatu.

Je, kama nimepewa vidonge vitatu vya azuma, nikameza na bado naendelea kujisikia vibaya nikanunue nyingine au niache niendelee na dawa nyingine.

Hapa ninachokiona ni matumizi ya holela ya dawa mitaani na hili linaweza kuleta athari nyingine.

Pengine Pale juu Wizara ya Afya tunahitaji mtu ambaye sio daktari kwa taaluma ili aweze kubalansi vizuri maagizo ya kisiasa na ushauri wa wataalamu.

Maana inaonekana Daktari akipewa maagizo kwanza anaanza kuyapima maagizo kwa kutumia taalauma yake.
 
Jikinge wewe Kama wewe mkuu! Kila mtu sio wizara sio Nani kaufyata, hata yale (mavitambaa "in mfalme juha's voice ) wale wakubwa wanaogopa kuyavaa, hapa wanatetea ugali wao,,pia kuyavaa(according to wao wanaona Ni usaliti )

Anyway , 5 Tena
 
Wizara ni mtu yupo.

1613735277752.png



1613735322485.png
 
Jikinge wewe Kama wewe mkuu !!! Kila mtu sio wizara sio Nani kaufyata,,,, hata yale (mavitambaa """"in mfalme juha's voice ) wale wakubwa wanaogopa kuyavaa, hapa wanatetea ugali wao,,pia kuyavaa(according to wao wanaona Ni usaliti ))

Anyway , 5 Tena

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kujikinga wewe peke yako (individual masking) na kujikinga wewe na wengine wote kwa pamoja (Mass masking)!

Unapojikinga wewe peke yako wakati wote waliokuzunguka hawajajikinga bado unakuwa upo katika hatari kubwa ya kupata Corona!!

Ndo maana inashauriwa wote tujikinge kwa kuvaa mask ili tuwe salama zaidi na kupunguza kuambukizana.
 
 
Jikinge wewe Kama wewe mkuu! Kila mtu sio wizara sio Nani kaufyata, hata yale (mavitambaa "in mfalme juha's voice ) wale wakubwa wanaogopa kuyavaa, hapa wanatetea ugali wao,,pia kuyavaa(according to wao wanaona Ni usaliti )

Anyway , 5 Tena
Mimi ninachoona kwenye wizara ya afya ni lack of leadership basi na ndiyo maana nikasea tunahitaji waziri asiye dakitari, ambaye atajua kubalansi maagizo ya kisiasa na utaalamu kutoka kwa wataalamu.

kila mmoja aone yake yametimizwa.
 
Wala Usilaumu wizara, wanaenda na mdundo wa mpiga ngoma, ili vibarua vyao vidumu. Utaenda kinyume utatumbuliwa ukijifanya mzalendo, au unasimamia taaluma.

Wanafanya kile bwana mkubwa anataka. Bwana mkubwa amejitoa fahamu halafu wewe ujifanye unazo utapata tabu.

Nape ni somo zuri la kimadaraka na kimamlaka. Rais anakoseaje mbele ya Waziri wake.

Maisha haya huhitaji kuwa really Bali smart.
 
Mimi ninachoona kwenye wizara ya afya ni lack of leadership basi na ndiyo maana nikasea tunahitaji waziri asiye dakitari, ambaye atajua kubalansi maagizo ya kisiasa na utaalamu kutoka kwa wataalamu.

kila mmoja aone yake yametimizwa.
Ni wizara pekee ambayo mume wa waziri anafahamika kuliko katibu mkuu wa wizara...
 
Back
Top Bottom