Barca ina maana gani? Dar in maana gani: Ama Ronaldinho kwa Ronaldo ina maana Gani? Ama Jair kwa Jairzinho ina maana gani? Unajua nickname wewe? Nimetumia mifano ile ili uelewe nini kinachoendelea hapo. Watumie Greens wao Waingereza?
Barca kwa Barcelona inalink kwa jina hilo tu. Katika Espagnol halina maana yoyote nje ya Barcelona. Ndivyo ilivyo Yanga. Maana yake inlink kwa jina Young tu. Ukikuta majina kama Ernestito utalaumu watu wewe kwa nini hamumuiti Ernesti!
Kwa kuongezea, miaka hiyo timu hizi mbili Young Africans na Sunderland zilijipa miji. Yanga wakachukua Kuala Lumpur, Malaysia na Sunderland wakajitwalia Abidjan, Ivory Coast. Sunderland wakishinda utasikia mashabiki wakishangilia; "Abidjan oyeee! Lumpa ziiii!".Young Africans wakishindia utasikia "Lumpa oyeee! Abidjan ziiii!" Lumpa ikawa jinsi walivyoutamka na kuandika mji wao Kuala Lumpur. Sunderland waliwaita Young Africans kiutani "Makuala hao" kutokana na jina la Kuala Lumpur ama "Lumpa". Mashabiki wakiulizana hata shuleni tuliposoma:"Wee timu gani bwana?" Mtu alijibu ama Lumpa ama Abidjan".
Linganisha na Cavaliers wa NBA huitwa "Cavs"; Juventus na "Juve", Paul Gascoigne na "Gazza", Ramadhani na "Rama", Bakari na "Beka". Kwa mfano tu. Khalikh na "Likky". Juve ina maana gani? Likky ina maana gani? Cavs ina maana gani? Gazza ina maana gani? Au kwa sababu Waswahili wamejipatia nickname yao wewe hutaki kuelewa mpaka iwe Barca ndiyo nikname? Yanga ni nickname ya Young. Wameswahilisha Young. Wako sawa tu.