Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Babu babu sasa kimyaa au mission accomplished?
 
alishapata mkwanja wa kumtosha, kasepa mzima mzima.
 
Ushabiki wa kidini tu, hawana lolote hao. Mbona ya Ntwara kwa Subira anayesema anapaewa maarifa makaburini hawamsemi, huyo babu anayepiga sala kwa wote na kuwapa dawa ana dhambi gani wanayoiona kwa macho yao yenye hila? Watu watakwenda Samunge, watakunywa dawa na wenye imani watapona, ila wenye kwenda kumjaribu babu watanawa lakini hawatakula. Acheni Mungu aitwe Mungu peke yake. Wivu wa nini na tiba ya babu?
 
Babu bado anatibu, sema wateja wake wengi si watanzania... Ni utalii kiaina
 


Great Spiritual Analysisi,Jf Oyeeeeeeeeeee,Babu wa Loliondo na Nguvu zake za Kuzimu Ziiiiiiiiiiiiiiiii!!
 
Leo nimesikia kwenye vyombo vya habari babu analalamika kuhujumiwa na watu ndio maana foleni imepungua sana kwake.
 
Kwa mujibu wa makala ya gazeti la Raia Mwema,kamat ya bunge ya huduma za jamii imeitaka TFDA ifungie dawa/huduma hiyo ya babu.
 
Babu siku hizi ana nyumba mpya + solar power,usafiri nk.Mambo yake mazuri.Anasema watu wamepungua sana kwa sababu wanapotoshwa.
 
Nilitegemea kipindi hiki cha mgomo wa madaktari,babu angechukua chati.
 
Hosea 4:6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwakuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwakuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nami nitawasahau watoto wako.

Yohana 8:31-32 Basi Yesu aliwaambia wale wayahudi waliomwamini Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli,tena mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru.

Ayubu 5:3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara nikayalaani maskani yake

Mithali 3:5 Mtumaini bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako.
Zaburi 119: 99 ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote maana shuhuda zao ndizo nizifikilizo.

nimuhimu sana kusoma Biblia na kuomba uongozi wa Roho mtakatifu ili uweze kuielewa. kumbuka Neno la Mungu linasema kumcha bwana ni chanzo cha maarifa.
 

Asante kwa neno mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…