Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Babu babu sasa kimyaa au mission accomplished?
 
alishapata mkwanja wa kumtosha, kasepa mzima mzima.
 
Ushabiki wa kidini tu, hawana lolote hao. Mbona ya Ntwara kwa Subira anayesema anapaewa maarifa makaburini hawamsemi, huyo babu anayepiga sala kwa wote na kuwapa dawa ana dhambi gani wanayoiona kwa macho yao yenye hila? Watu watakwenda Samunge, watakunywa dawa na wenye imani watapona, ila wenye kwenda kumjaribu babu watanawa lakini hawatakula. Acheni Mungu aitwe Mungu peke yake. Wivu wa nini na tiba ya babu?
 
Babu bado anatibu, sema wateja wake wengi si watanzania... Ni utalii kiaina
 
ukweli utabaki palepale, kuwa siyo kila uonekanapo Msalaba panafaa kufanyia ibada na kutolea sadaka. Mungu hawezi kujipinga mwenyewe!. Imeandikwa kuwa Mungu huangalia neno lake ili apate kulitimiza!. Pia Mungu anasema Kupitia Zaburi ya kuwa ameikuza ahadi yake kuliko neno lake. Mungu hawezi kujipinga Mwenyewe pale aliposema Enendeni ulimwenguni kote mkaihubili injili na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wangu, katika kitabu cha Marko 16:kuanzia mstali 16 anasema na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watanena kwa lugha, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya, watakanyaga nyoka hatawadhuru, watakunywa kitu cha kufisha nao hawata kufa.



1. Mungu hajasema Mtafungua hospitali na kuwatibu watu kwa hela wenyeji 500 na wageni dola moja (Mungu wa mbinguni anasema mmepata bure, toeni bure).


2. Mungu wa mbinguni anasema enendeni ulimwenguni kote (siyo kubaki sehemu moja) kubaki sehemu moja hilo siyo agizo la Mungu wa mbinguni labda la mungu mwingine.



3. Mungu hakusema ponyeni watu lakini wabaki na imani zao (yesu anasema myafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu --wanafunzi wa kristo).


4. Mungu wa mbinguni hana mipaka yeye popote pale yupo na kwakiasi kilekile ameahidi wawapo wawili watatu kwa ajili ya neno langu nami nipo. majini hayana uwezo wakuwa kila mahala, jini moja likiwa kigamboni, manayake halipo ubungo. ila na ubungo yatukuwapo majini lakini siyo lile la kigamboni hivyo nguvu zisizo za Mungu zinamipaka akiondoka loliondo tu uganga hana.





5. Yesu ndiye mwanzilishi wa imani yetu, tunaangalia alifanya nini ili nasi tufuate, je Yesu aliweka kituo wapi cha kutolea huduma? na kama hakuweka Yeye kaitoa wapi?.





6. Mungu hawezi kuwa na kikombe maalumu cha kuchotea dawa na ambacho hatakiwi kukishika mtu mwingine mpaka analala nacho, ikiwa ni Mungu kampa kazi hiyo isingeambatana na masharti ya kiganga kama hayo.





7. Mungu wetu siyo wa kusababisha environmental degradation kiasi cha kila siku kuvuna miti mingi kama afanyavyo. kuna maono mbalimbali katika kutenda kazi ya BWANA jambo la muhimu ni kwamba siyo kila mtu ataponyeshwa na maono ya mtu wa kwanza kwa kusema wote wataponeshwa kwa kunywa kikombe.





8. Biblia inasema mwenyenacho ataongezewa bali asiyenacho hatakile kidogo atanyanganywa asiyemwamini yesu hata ile imani ndogo aliyonayo atanyanganywa.




9. Biblia inaagiza ya kuwa usipomwamini Yesu umekwisha kuhukumiwa na aliyempokea yesu hatapita hukumuni.


10. Yohana 17:1-6 ukisoma hapa utajuwa yakuwa Yesu ni nani na anamamlaka gani juu ya wenye mwili.kwa mawazo yangu huyo ni mganga wa jadi aliyekamilika kabisa.



kumbuka kitu chochote ulijino huwa kinachakachuliwa, na huwezi kuchakachua kitu feki kwa hili ninaujasili wa kusema Yesu kristo ndiyo jina pekee tulilopewa wanadamu kutupeleka Mbinguni na siyo Dini ya mtu. Hatakama Mtu alisema msiponiamini, aminini dini yangu wanadamu wenye malengo ya kwenda mbinguni hawatakiwi kuamini dini ya mtu. ukijuwa hata mashetani na majini yana dini usingependa hata kusema dini yangu.


Great Spiritual Analysisi,Jf Oyeeeeeeeeeee,Babu wa Loliondo na Nguvu zake za Kuzimu Ziiiiiiiiiiiiiiiii!!
 
Leo nimesikia kwenye vyombo vya habari babu analalamika kuhujumiwa na watu ndio maana foleni imepungua sana kwake.
 
Kwa mujibu wa makala ya gazeti la Raia Mwema,kamat ya bunge ya huduma za jamii imeitaka TFDA ifungie dawa/huduma hiyo ya babu.
 
Babu siku hizi ana nyumba mpya + solar power,usafiri nk.Mambo yake mazuri.Anasema watu wamepungua sana kwa sababu wanapotoshwa.
 
Nilitegemea kipindi hiki cha mgomo wa madaktari,babu angechukua chati.
 
Hosea 4:6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwakuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwakuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nami nitawasahau watoto wako.

Yohana 8:31-32 Basi Yesu aliwaambia wale wayahudi waliomwamini Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli,tena mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru.

Ayubu 5:3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara nikayalaani maskani yake

Mithali 3:5 Mtumaini bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako.
Zaburi 119: 99 ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote maana shuhuda zao ndizo nizifikilizo.

nimuhimu sana kusoma Biblia na kuomba uongozi wa Roho mtakatifu ili uweze kuielewa. kumbuka Neno la Mungu linasema kumcha bwana ni chanzo cha maarifa.
 
Hosea 4:6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwakuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwakuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nami nitawasahau watoto wako.

Yohana 8:31-32 Basi Yesu aliwaambia wale wayahudi waliomwamini Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli,tena mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru.

Ayubu 5:3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara nikayalaani maskani yake

Mithali 3:5 Mtumaini bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako.
Zaburi 119: 99 ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote maana shuhuda zao ndizo nizifikilizo.

nimuhimu sana kusoma Biblia na kuomba uongozi wa Roho mtakatifu ili uweze kuielewa. kumbuka Neno la Mungu linasema kumcha bwana ni chanzo cha maarifa.

Asante kwa neno mkuu.
 
Back
Top Bottom