Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

ukweli utabaki palepale, kuwa siyo kila uonekanapo Msalaba panafaa kufanyia ibada na kutolea sadaka. Mungu hawezi kujipinga mwenyewe!. Imeandikwa kuwa Mungu huangalia neno lake ili apate kulitimiza!. Pia Mungu anasema Kupitia Zaburi ya kuwa ameikuza ahadi yake kuliko neno lake. Mungu hawezi kujipinga Mwenyewe pale aliposema Enendeni ulimwenguni kote mkaihubili injili na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wangu, katika kitabu cha Marko 16:kuanzia mstali 16 anasema na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watanena kwa lugha, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya, watakanyaga nyoka hatawadhuru, watakunywa kitu cha kufisha nao hawata kufa.



1. Mungu hajasema Mtafungua hospitali na kuwatibu watu kwa hela wenyeji 500 na wageni dola moja (Mungu wa mbinguni anasema mmepata bure, toeni bure).


2. Mungu wa mbinguni anasema enendeni ulimwenguni kote (siyo kubaki sehemu moja) kubaki sehemu moja hilo siyo agizo la Mungu wa mbinguni labda la mungu mwingine.



3. Mungu hakusema ponyeni watu lakini wabaki na imani zao (yesu anasema myafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu --wanafunzi wa kristo).


4. Mungu wa mbinguni hana mipaka yeye popote pale yupo na kwakiasi kilekile ameahidi wawapo wawili watatu kwa ajili ya neno langu nami nipo. majini hayana uwezo wakuwa kila mahala, jini moja likiwa kigamboni, manayake halipo ubungo. ila na ubungo yatukuwapo majini lakini siyo lile la kigamboni hivyo nguvu zisizo za Mungu zinamipaka akiondoka loliondo tu uganga hana.





5. Yesu ndiye mwanzilishi wa imani yetu, tunaangalia alifanya nini ili nasi tufuate, je Yesu aliweka kituo wapi cha kutolea huduma? na kama hakuweka Yeye kaitoa wapi?.





6. Mungu hawezi kuwa na kikombe maalumu cha kuchotea dawa na ambacho hatakiwi kukishika mtu mwingine mpaka analala nacho, ikiwa ni Mungu kampa kazi hiyo isingeambatana na masharti ya kiganga kama hayo.





7. Mungu wetu siyo wa kusababisha environmental degradation kiasi cha kila siku kuvuna miti mingi kama afanyavyo. kuna maono mbalimbali katika kutenda kazi ya BWANA jambo la muhimu ni kwamba siyo kila mtu ataponyeshwa na maono ya mtu wa kwanza kwa kusema wote wataponeshwa kwa kunywa kikombe.





8. Biblia inasema mwenyenacho ataongezewa bali asiyenacho hatakile kidogo atanyanganywa asiyemwamini yesu hata ile imani ndogo aliyonayo atanyanganywa.




9. Biblia inaagiza ya kuwa usipomwamini Yesu umekwisha kuhukumiwa na aliyempokea yesu hatapita hukumuni.


10. Yohana 17:1-6 ukisoma hapa utajuwa yakuwa Yesu ni nani na anamamlaka gani juu ya wenye mwili.kwa mawazo yangu huyo ni mganga wa jadi aliyekamilika kabisa.



kumbuka kitu chochote ulijino huwa kinachakachuliwa, na huwezi kuchakachua kitu feki kwa hili ninaujasili wa kusema Yesu kristo ndiyo jina pekee tulilopewa wanadamu kutupeleka Mbinguni na siyo Dini ya mtu. Hatakama Mtu alisema msiponiamini, aminini dini yangu wanadamu wenye malengo ya kwenda mbinguni hawatakiwi kuamini dini ya mtu. ukijuwa hata mashetani na majini yana dini usingependa hata kusema dini yangu.
 
Je na wale watu 200 waliojitolea kwaajili ya tafiti kama dawa hiyo inaponya imekuaje? Mbona wizara ya afya haitupatii majibu?
 
Je na wale watu 200 waliojitolea kwaajili ya tafiti kama dawa hiyo inaponya imekuaje? Mbona wizara ya afya haitupatii majibu?

majibu gani sasa unataka! je kukaa kimya siyo majibu?. hapo mtu mwenye akili anajuwa nini kinachoendelea!.

kumbuka ya kuwa hata hao watafiti walikunywa!, je kama dawa inasababisha watu wawe vichaa sijui watasemaje!
 
Babu vipi bado ananywesha na watu wanapona?
 
jANA NILIKUWA NAANGALIA CHANEL YA KENYA CITIZEN TV ,WAZIRI WA AFYA KASEMA NO CURE IN LOLIONDO DEADLY DRUGS WAAKAONESHA NA MAKABURI KIBAO KWA WALE WALIOKUNYWA DAWA YA BABU WAAKACHA ZA HOSPITAL
 
Kuishi kwa kumtegemea babu nako tabu eeh.
 
ukienda loliondo unamkuta babu yuko hapo nje mwenyewe!.... (joke)
 
Loliondo Kikombe bado kipo na kuna magari si chini ya 200 kila siku ila mengi ni kutoka Nchi jirani hasa kenya, Uganda, Rwanda na nimeona watu toka hata Zambia. Nilikuwa huko Ijumaa.

Dah! Watu kama nyinyi ni janga kwa taifa!
 
Niliongea na diwani wa kata ya Samunge ambaye tulikutana safarini tukiwa tumekaa seat moja, akaniambia takwimu za kwenye kata yake zinaonyesha kati ya watu 10 wanaojulikana kuwa wana Ukimwi na wanatumia ARVs kwenye vituo rasmi, nane wamepona baada ya kunywa dawa ya Babu na wamethibitisha hilo kwa vipimo. Lakini wawili kati ya hao hawajapona na wanaendelea kutumia ARVs. Pia kwa magonjwa kama Kisukari na hata asthma kuna waliopona baada ya tiba ya Babu na wengine hawakupona. Ndugu yangu mmoja aliyekuwa anasumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu alikunywa dawa Februari mwaka huu, na amepona kabisa. Ufanyike utafiti kuangalia kwa nini wengine wanapona na wengine hawaponi. Mie nadhani tatizo lipo kwenye dozi. Huenda hawa ambao hawajapona wangepata vikombe vya ziada wangepona. Sijui.
 
Na Ashe Hassan


Mtoto Subira Ally (12), Mkazi wa Kijiji cha Malema, Kata ya Maratani, wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara ameonekana kumpindua Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile (pichani) kwa kupata wateja wengi ambao wanakwenda kutibiwa.

Kupinduliwa kwa Babu kumetafsiriwa na watu baada ya kuonekana sasa nyumbani kwake Kijiji cha Samunge hakipati wageni wengi kama ilivyo Kijiji cha Malema anakokaa Subira ambako wageni kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani hufurika kila kukicha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, mtoto Subira alisema kuwa siku moja , Aprili mwaka huu akiwa amelala alioteshwa ndoto iliyokuwa ikimuelekeza kuwa anatakiwa atoe tiba kwa njia ya kikombe kwa kutumia mzizi wa mti uitwao Mkong’oto unaopatikana hapo nyumbani kwao, hivyo kumjulisha mama yake mkubwa anayeishi naye.

“Niliambiwa kuwa dawa hiyo itakuwa inatibu Ukimwi, kisukari, kuponya vipofu, viziwi, na wote ambao miili yao itakuwa imekufa ganzi au kupooza,” alisema Subira.

Aliongeza kuwa dawa hiyo ya kikombe alioteshwa kuwa iwe ikinunuliwa kwa gharama ya shilingi 500. Alipoulizwa ni watu wangapi ambao amewatibu tangu alipoanza kazi hiyo alisema ni wengi sana.

“Wagonjwa ni wengi sana ambao wamepata kikombe na wanaendelea kufika hapa nyumbani,” alisema huku akiwa na mama yake mkubwa aliyefahamika kwa jina moja la Binti Ismail.

WAGENI TOKA NJE YA NCHI

Subira alisema licha ya kutibu wananchi wa Tanzania, amekuwa akipokea wageni wengine kutoka nje ya nchi kama vile Msumbiji na Malawi.

Aliongeza kuwa licha ya wagonjwa wengi kutoka Tanzania bara, amepokea wengine kutoka Visiwani Zanzibar na anakumbuka mmoja alikuwa na matatizo ya miguu ambayo ilikuwa imekufa ganzi kwa miaka mitano. “Sasa mgonjwa huyo wa Zanzibar ganzi imekwisha na anatembea vizuri, amemshukuru sana Mungu.” Mama mkubwa wa binti huyo, aliyefahamika kwa jina la Binti Ismaili alithibitisha mwanaye kuoteshwa na kutoa tiba hiyo.

MASHUHUDA

Naye mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Sharifa mkazi wa Tandika Mikoroshini jijini Dar es Salaam aliyezungumza na mwandishi wetu hivi karibuni alisema kuwa, alikuwa muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi lakini baada ya kutumia dawa ya mtoto huyo na kwenda kupima ameonekana hana virusi vya maradhi hayo.

“Baada ya kutumia dawa ya Mkong’oto nimepona,nilikwenda kupima katika Hospitali ya Maratani mkoani Mtwara na kuthibitishiwa na daktari aliyenipima aitwae Dk.Namihambi kuwa sina virusi. Nangoja kupima mara ya pili kwa uhakika zaidi,” alisema.

Aidha, baba mmoja ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa alikuwa na ugonjwa wa Ukimwi lakini sasa hana baada ya kupimwa katika Hospitali ya Mkomaindo, Masasi.

WAZIRI WA AFYA ALICHOSEMA

Mara baada ya Babu Masapile kutangaza kuoteshwa kutoa tiba ya magonjwa sugu, watu wengi wameibuka kutoa tiba hiyo na wananchi kufurika kupata kikombe.

Hata hivyo, wiki iliyopita gazeti hili lilimkariri Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda akisema kuwa katika tafiti za kitaalamu dawa za mitishamba hazijathibitishwa kutibu Ukimwi.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati anazindua Kituo cha Matibabu ya Wagonjwa wa Ukimwi na Mafunzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Dk. Mponda alisema wagonjwa wa Ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV) na akawataka waende kwenye vituo vya afya kupewa.“Wagonjwa wanaokwenda kupata tiba asili waache kwa kuwa bado zinafanyiwa utafiti,” alisisitiza Waziri Mponda.

Akili kumkichwa....hakika watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa...Mtoto Subira akihojiwa Live na Wapo Radio juu ya Tiba yake na Historia yake alisema yeye anamjua Babu wa Loliondo na huwa wanakutana naye Baharini....Mwandishia akamuuliza wewe umesoma mpaka darasa la ngapi Subira akajibu Mimi nasoma darasa la Tano shule ya Makaburini......mwandishi akahoji tena shule hiii ipo wapi....Subira akajibu shule hii ipo makaburini kule wanakozikwa watu.....mwandishi akahoji tena wewe unaenda shule saa ngapi Subira akajibu huwa naenda shule kuanzia saa tatu usiku....Mwandishi anauliza tena saa tatu usiku huogopi makaburini peke yako...Subira anajibu siogopi...just imagine Mtoto wa miaka 12....Shule anayosoma ni ya makaburini ...Elimu ya kuruani makaburini...haya ni maneno yake mwenyewe.......na akasema yeye na Babu wa Loliondo wanafahamiana......Sasa kazi kwenu.....Full mapepo hii ndiyo Tiba......
 
Akili kumkichwa....hakika watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa...Mtoto Subira akihojiwa Live na Wapo Radio juu ya Tiba yake na Historia yake alisema yeye anamjua Babu wa Loliondo na huwa wanakutana naye Baharini....Mwandishia akamuuliza wewe umesoma mpaka darasa la ngapi Subira akajibu Mimi nasoma darasa la Tano shule ya Makaburini......mwandishi akahoji tena shule hiii ipo wapi....Subira akajibu shule hii ipo makaburini kule wanakozikwa watu.....mwandishi akahoji tena wewe unaenda shule saa ngapi Subira akajibu huwa naenda shule kuanzia saa tatu usiku....Mwandishi anauliza tena saa tatu usiku huogopi makaburini peke yako...Subira anajibu siogopi...just imagine Mtoto wa miaka 12....Shule anayosoma ni ya makaburini ...Elimu ya kuruani makaburini...haya ni maneno yake mwenyewe.......na akasema yeye na Babu wa Loliondo wanafahamiana......Sasa kazi kwenu.....Full mapepo hii ndiyo Tiba......
Zaidi ya hatari.
 
eee bana eee, kusoma tu hayo ya mtoto yanatia woga.
 
Back
Top Bottom