Hivi zile story tulizokuwa tunasoma shuleni bibi unamsaidia mzigo wa kuni kufika kwake anakupa zawadi hazipo?

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Kwema wakuu habari zenu?

Nimejaribu kuwaza tu Tulipokuwa tunasoma au kuhadithiwa shuleni, hizo story kwenye maisha ya kawaida haya tunayoishi huwa havitokei kabisa

Nimeona kuuliza maana mpaka kuandika huu uzi ni mambo mengi nafikilia natamani niwe natembea njiani nikutane na Bibi Mzee akiwa na kuni kichwani na fimbo mkononi akiwa anatembea taratibu, nimwambie bibi nikusaidie Mzigo

Niuchukue tuongozane mpaka nyumbani kwake akifika anishukuru na kunipa zawadi ya kioo ama pete aniambie, " Mjukuu wangu Asante kwa kunisaidia na roho yako nzuri nakupa zawadi hiyo itakusaidia chochote kile ukiombacho kwa kutumia pete hii au kioo hiki utapata" basi nami ntaondoka na baada ya siku kadhaa nakuwa tajiri

Najaribu kuwaza tu maana Maisha yanavyopiga mpaka watu tunawaza njia za short court, nauliza tu hizo story hazipo kwenye real life au ndo tulisoma tu shuleni ikawa imetoka🤪🤦😁
 
Mabibi wa sasa hivi ukijitusu kumsaidia ukifika kwake ataomba umsaidie kuosha na vyombo na kumsafishia nyumba halafu ukimaliza wakati wa kuaga anakuomba hela.....
Umenichekesha 🤣😂 da! Unasema anaomba hadi na hela du!
 
Hawa hawa mabibi wa kisasa hata hizo stori haziwahusu, sipati picha kizazi chetu hiki ndo kije kuwa mabibi na mababu... wajukuu wetu watakuwa na mizimu ya hovyo kabisa isiyo na lolote!
 
Hawa hawa mabibi wa kisasa hata hizo stori haziwahusu, sipati picha kizazi chetu hiki ndo kije kuwa mabibi na mababu... wajukuu wetu watakuwa na mizimu ya hovyo kabisa isiyo na lolote!
Kwanini Mkuu😅
 
Mabibi wa sasa hivi ukijitusu kumsaidia ukifika kwake ataomba umsaidie kuosha na vyombo na kumsafishia nyumba halafu ukimaliza wakati wa kuaga anakuomba hela.....
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…