Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
We nawe acha kudeka ...sinimeshabadilisha??Sasa hivi ni KILLE!!
Hivi wewe leo unaongea lugha gani? "Kille" ndo nini sasa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We nawe acha kudeka ...sinimeshabadilisha??Sasa hivi ni KILLE!!
Aiseee...sasa huo ndo ule wivu unaozidi mpaka kero.Yani mtu wa aina hiyo hata Sipiyu akinigongea Thanks na Like JF ananiuliza kwanini fulani kakugongea thanks?Embu kuweni na imani bwana....hata asipokua nao bado anaweza asiwe muaminifu vile vile.Kuwa mdanganyifu ni hulka ya mtu na sio swala la yeye kua na marafiki wa jinsia tofauti au la!!
Sawa, udanganyifu ni hulka ya mtu. Hilo mimi sikatai. Lakini kubali usikubali urafiki wa jinsia tofauti na mwanandoa ipo siku utaleta mzozo ndani ya ndoa.
Na haya mambo ya imani pofu mimi sikubaliani nayo. Cha muhimu ni wewe uliye kwenye ndoa kutokumpa mwenzako hata chembe ya sababu kukudhania kuwa unafanya mambo ambayo hutakiwi kufanya. Na kama kweli hufanyi jambo lolote baya basi na mwenzako naye wala hatakuwa na sababu ya kukushuku.
Bora ukose uaminifu huku mume hajui kuliko kujenga uhusiano na mwanaume mwingine mume anajua.
Kama unajua udanganyifu ni hulka ya mtu basi fahamu pia mazoea huweza kuzaa tabia, na mwishowe usaliti.
Adui hana alama, hata shosti wako wa tangu primary anaweza kukutafunia mumeo.
Sawa, udanganyifu ni hulka ya mtu. Hilo mimi sikatai. Lakini kubali usikubali urafiki wa jinsia tofauti na mwanandoa ipo siku utaleta mzozo ndani ya ndoa.
Na haya mambo ya imani pofu mimi sikubaliani nayo. Cha muhimu ni wewe uliye kwenye ndoa kutokumpa mwenzako hata chembe ya sababu kukudhania kuwa unafanya mambo ambayo hutakiwi kufanya. Na kama kweli hufanyi jambo lolote baya basi na mwenzako naye wala hatakuwa na sababu ya kukushuku.
Huyu Lizzy tumsamehe tu
Si alishasemaga hana hisia za kike, bali anazo za kiume
Yaani hana hisia za wivu, hata akiona mume wake ana cheza dansi na shosti wake wameshikana viunuuuuuuuuu
Nyie nimewagundua ni wabinafsi sana....hamwezi kushindwa kumwambia mke ''marafiki zako wote potezea mbali mimi nakutosha''!!!
Kwahiyo kwa mkeo kua na rafiki wa kiume ni kukupa sababu ya kumhisi vibaya???Kwanini na wewe usiamue kumuamini mpaka pale utakapoona urafiki ule sio urafiki mzuri???
Hahahahhahha
Kuna mipaka bwana...ila sio kumkataza mtu kabisa!!!
Nyie nimewagundua ni wabinafsi sana....hamwezi kushindwa kumwambia mke ''marafiki zako wote potezea mbali mimi nakutosha''!!!
Hivi wewe leo unaongea lugha gani? Kille ndo nini sasa?
Ndo maana ndoa za siku hizi hazidumu kabisa. Mimi babu na bibi yangu bado wako pamoja. Sijawahi kumwona au kumsikia bibi akiongelea rafiki yake wa kiume hata siku moja. Vivyo hivyo kwa babu.
Lakini katika zama hizi ni vigumu sana na ndo maana ndoa nyingi ziko kwenye life support kama bado hazijafa kabisa. Mtu anang'ang'ania marafiki wa jinsia iliyo tofauti na yake huku yuko kwenye ndoa halafu eti anategemea kuwa na ndoa nzuri yenye amani? Kama ni hivyo si muweke wazi tu kuwa ndoa yenu ni ndoa huria (open marriage).
Ni heri kuwa singo kuliko kuwa kwenye ndoa na mtu mwenye marafiki lukuki wa kiume.
Huu ubinafsi ndo utanilindia mke wangu na kuzuia mianya yote ya kutongoza my waifu.
Sitaki mzaha
Lizzy, frankly nikumbushe tena wenzangu wa jinsia zetu kwamba kukubaliwa kua B.F/Mume si kigezo cha kumiliki uhuru wa mwenzio ...ulipomuaproach alikua na marafiki zake na kampani hivyo kumkatiza si uungwana...Muhimu ni kukaa chini na kuelezana pale panapotokea hali inayotia mashaka kwa upande wowote...binafsi whom niliyesign naye domestic agreement nilimkuta social na simlazimishi abehave ki consevative km mimi...thus all!
Now THIS...is my kinda thinking!!
Nyaniizzo na Sipiyu kama nawaona vile mnavyoandika kwa hisia!!Poleni bana ila kumuoa mtu haina maana una hati miliki mpaka umbadili hata kwa yale yasiyo ya lazima!!
mimi napenda kuwepo agreement toka mwanzo
kuwa uki cheat tu,hatua ntakazochukua ni hizi na hizi
and i own a gun by the way lol