Hivyo ndivyo vijana wa kazi wa Kitanzania wanavyoturudisha nyuma na kututia hasara kubwa

Usinikumbushe,yaani nilikuta kifua kinajaa ghafla kama nashindwa kupumua flani hivi,nikafanikiwa kuishusha,angetokea mapema basi ningepiga tukio dunia ingeweka katika kumbukumbu
Hakika mkuu mimi jasho lilinivaa ghafla yaani kama yupo karibu na nina bastola kwisha habari yake.
 
Mkuu ni ngumu sana asee kusimamia mwenyewe na kwa namna hii hatuwezi piga hatua kabisa.
imagine family ipo Dar miradi yako iko mwanza utajigawa vipi? je kama una miradi zaidi ya2 utajigawa vipi?

Tatizo ni sisi wenyewe wa Tz hatuhurumiani tumejaa wivu na husda na unafiki.
 
Hata mimi. Hivi kuna rafiki yangu naye yupo katika process ya kuwekeza katika kupiga story akaniambia katika usimamizi wa kazi zake atamuweka ndg yake mtoto wa mama yake mkubwa nimemshauri usithubutu kabisa japo kamfagilia sana yule ndg katoka chuo anajua kila kitu nimemwambia heri hata mtu baki ukikoswa warudi au mtu yeyote wa nje.
 
Umenena vyema mkuu uwekezaji wowote unahitaji man power ili upige hatua hata uwe mama ntilie una migawaha 4 lazima utakuwa na watu tu. TUKO PAMOJA MKUU NA AHSANTE SANA.
 
Usimsahau mwamba wa kuitwa 20% bila bangi angekuwa mbali sana.
 
Kupata watu sahihi wa kufanya nao kazi tabu sana mkuu.

Tanzania tuna vijana wa hovyo sana mkuu, inatakiwa tuwe makini.

Jipange tena upya, kipindi hiki uwe muangalifu zaidi, Pole sana.
Ahsante sana mkuu siwezi kataa tamaa hata siku moja sema nawasikitia sana vijana wenzangu kama huyu niliye eleza hapo uhakika wa kupata hata laki1 moja ya mpingo kwa sasa na ana family maisha magumu nyumba mbaya hadi huruma. Tulipovuna nikampa m6 za hela bila kuzisimamia mimi angezitapanya. mke aliniambia usimpe njoo nae mnunue mabati chakula nk na nikafanya hivyo.

kwa sasa hawezi pata hiyo hela. Ahsante sana mkuu
 
Wakute sasa kwenye Simba na Yanga jitihada zaoπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Huyu jamaa siku inacheza simba usimwabie kitu kabisa kuhusu shamba sana sana omba mechi iwe usiku hapo kazi
atafanya lakini mawazo yake yote mpiran. itokee mechi inachezwa saa10 jioni shambani sahau kabisa na usitegemee tena anaenda mapema kuwahi viti vya mbele kwenye banda umiza. Ni ukichaa haswa.
 
Nawajua vizuri.....nikisha ona mfuasi wa hizi team tayari najua hapa kuna viwango vidogo vya akili
 
Umaskini Kaka huwa unaanzia kichwani.

Pamoja na kwamba umembeba sana lakini bado habebeki.

Niliwahi kuishi Zanzibar kipindi fulani nikakutana na mzee mmoja amechoka mbaya. Wenyeji wakaniambia ni Kaka Yake Rais Wa Zanzibar wakati huo Dr Ali Mohamed Shein.
Yule mzee alikuwa kachoka anauza urojo.
Nikauliza imekuwaje Kaka yake Rais anakuwa na maisha magumj hivi? Yaani ndugu yakw ameshindwa jinsi ya kumnyanyua? Watu wanamlaum sana Rais Mstaafu Shein.

Lakini Deep Down ni kuwa huenda Shein alishajaribu mbinu zote za kumnyanyua lakini ikawa habebeki.

Ndio kama Hawa.

Ndugu wa Prof Kabudi ni Choka Mbaya kama ndugu wa Prof Kapuya.

Unaweza kuwalaum kwanini wanajipenda wao tu. Kumbe ndugu wenyewe ni wenye akili kama za huyo Mfanya kazi wako.

Kuna Ndugu uking'ang'ania kuwasaidia watakurudisha nyuma na wewe utakuwa maskini kama wao
 
Umeniumiza Kaka
Pole Sana ,usiku mwema na Sasa siwezi kuongezea chochote zaidi ya kusema kidonda ni kibichi mno umekitonesha Kaka 😭😭
Pole sana asee mimi ilinichukua siku kadhaa bila kumwambia wife. katika kupta mtandaoni ndo nikaona hiyo video jamaa kapita mlemle nilimopitia mimi kasoro mtaji tu.

Nivyema mkuu ukatumbia hapa nasi tupate mawili m,atatu ama manne tujifunze pia.
 
Pole sana asee mimi ilinichukua siku kadhaa bila kumwambia wife. katika kupta mtandaoni ndo nikaona hiyo video jamaa kapita mlemle nilimopitia mimi kasoro mtaji tu.

Nivyema mkuu ukatumbia hapa nasi tupate mawili m,atatu ama manne tujifunze pia.
Kwasasa siwezi Kaka ,hata nikisema niandike nitaijaza simu machozi au keyboard machozi .
Wacha nijipe muda ,nikiwa sawa nitasimulia .
 
Ni sahihi kabisa. Nina uhakika jamaa atajuta sana alikuwa hajawahi kuwaza atanunu smart akanunua na saivi hana yaani ni huzuni kubwa. Watu kama ukifanikiwa ndo wanakuwa wa kwanza kukuita wee ni free mason na ole wako upoteze hata mtoto aisee wanapitia hapohapo
 
Hapo makosa yapo kwa mwenye mali. Yeye hayupo kazini na kamtoa kijana wake nani awe na uchungu na mali zake? Aliweka mifumo dhaifu ya kuwezesha upigwaji. Cha mtu mavi.
Mi nadhani ni kwa vijana wa kazi mkuu. Kama unashindwa kusimamia mali ya mtu je ya serkali utaweZa kuwa muadirifu kweli? Imagine hadi mchungaji wake anaye mwamini kashindwa hata kumpa taarifa tu? kazi ipo sana asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…