Mkuu labda aje raisi kichaa, ila serikali haihami Dar, sio leo wala kesho, itafungua makao makuu Dodoma, ila shughuli zile zile na huduma zile zile za makao makuu zitapatikana Dar, yan et siku serikali iseme pale magogoni raisi hatakaa tena pafungwe 😂 hapana aiseee
Kuhusu balozi za kimataifa, hizi wanaamua wao wakae wapi, na sidhani kuna balozi itaenda ikajitese kukaa Dodoma iache Dar,
Dar itapungua nguvu ya ushawishi sawa ila bado itakuwa kinara hapa Tz kwa miaka mingi sana ijayo,
Serikali kufanya mkoa wa pwani kuwa mkoa wa kiviwanda hio ndio ilipiga muhuri kuwa Dar haitafuta utawala wake kwa miaka mingi sana ijayo,