Hiyo Tanzania ambayo akina Mandela walikuwa wanaikimbilia, leo ndio inazalisha wakimbizi wa kisiasa

Hiyo Tanzania ambayo akina Mandela walikuwa wanaikimbilia, leo ndio inazalisha wakimbizi wa kisiasa

MK254, uwe unajua au hujui, ukweli ni kwamba Mandela alifika nchini kwa harakati za kupambana na Kaburu. Leo Wapinzani(Chadema) wanapambana kumrudisha Bepali/Kaburu ni Kaburu tu hakuna jina jingine la kuwapa ni Makaburu tu. Sasa wanakimbia nchi kwasababu hawataki kupambana na Bepali/Kaburu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Kambona alikimbia nchi hii. Watz hatucheki na vibaraka wa wazungu hata siku moja lazima wakimbie wenyewe!
Mbona mnakuwanga obsessed na mabeberu ama baba yenu Magu ndio amewafunza hivyo
 
Hakuna wakimbizi hapo hao wametafuna pesa za Chadema wameona zimeisha sasa wanaziwinda pesa za mabeberu

Namshukuru Mungu kwa kuniongoza kuiha ma Chadema siku aliyoondoka DK Slaa
 
Kwa comment hizi za baadhi ya watz ni bora tu Jiwe aendelee kuwabana zaidi, hadi akili ziwarudie. Akiweza awaamrishe wote wavae uniform kama za shule ya msingi na machifu na maDC wawe wanatembeza kichapo daily. Maanake haingii akilini kwamba mtu aliye na akili timamu atasema kwamba jamaa anaacha mali, marafiki na jamaa zake nyuma. Kisha anaandamana na mke na watoto wake pia, hadi nchi jirani kama 'maigizo'.

Bro, yaani wewe utadhani ndiyo mara yako ya kwanza kusikia wanasiasa wakiongea jambo!!!
Hela hana, na kwake hamna maisha nje ya siasa. Embu fuatilia alikuwa akifanya kazi gani kabla ya ubunge. Wafuatilie na wenzake kazi walizokuwa wakifanya.
 
Offcourse, wa upinzani ndio wanasiasa. Wale wa CCM ambao huwa unawasifia humu kila uchao ni malaika.
 
Hapa naona 2025 Kenya itakuwa na GDP ya $140 billion na Tanzania bado haitakuwa imefika $70 billion.
 
Hapa naona 2025 Kenya itakuwa na GDP ya $140 billion na Tanzania bado haitakuwa imefika $70 billion.

Hujawahua vizuri mabeberu.

Saa hii nimeona wanawapea Kenya kuingiza horticulture UK.
 
Siku mkijua usanii wa upinzani Tanzania mtabaki midomo wazi!
Hakuna wa kuwakimbiza. Mbona Lissu alikuwa anasema harudi Tz sababu ya usalama wake. Ulipofika msimu wa uchaguzi mbona karudi na hakuna aliyemgusa? Tena wakati wa kampeni anatukana tu na kumkejeli Magu, lakini hakuna aliyemgusa. Baada ya matokea ndiyo akajitia kuitisha maandamano ya "kupindua serikali" na wala hakika support. Ikabidi ajikimbize ubalozi angalau kulazimisha katishiwa kuuawa!
 
Offcourse, wa upinzani ndio wanasiasa. Wale wa CCM ambao huwa unawasifia humu kila uchao ni malaika.

Yule mwingine nimemuona anasindikizwa na mabeberu kwenda airport ili apande ndege aende ubeberuni.
😃😀😁
 
Kwa comment hizi za baadhi ya watz ni bora tu Jiwe aendelee kuwabana zaidi, hadi akili ziwarudie. Akiweza awaamrishe wote wavae uniform kama za shule ya msingi na machifu na maDC wawe wanatembeza kichapo daily. Maanake haingii akilini kwamba mtu aliye na akili timamu atasema kwamba jamaa anaacha mali, marafiki na jamaa zake nyuma. Kisha anaandamana na mke na watoto wake pia, hadi nchi jirani kama 'maigizo'.
Ulitaka comments ziweje
 
Screenshot_20201110-223457~2.png
 
Wapinzani wa bongo wamekuwa kama roma aliyejiteka kisha kusingizia maisha yake yapo hatarini ili apate hifadhi ya kuishi los angeles
 
Hizo fair fair ndo zimeturudisha nyuma sana, kujifanya sisi tuna roho nzuri Sasa ni kazi tu na mtu hii kasi ikimshinda akimbie nchi
 
Hizo fair fair ndo zimeturudisha nyuma sana, kujifanya sisi tuna roho nzuri Sasa ni kazi tu na mtu hii kasi ikimshinda akimbie nchi

Hongereni kwa hiyo kazi ya mwendo kasi...
Wapeni pole familia za hawa

2613391_Khamis.jpg
 
Tatizo naona vijana wengi wasioijua historia wamejitosa kwenye mitandao wamejawa na kejeli na kebehi, hawafahamu hii issue ilivyo ya hovyoo kwa nchi yenu.

Hasa vijana wenzetu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM , mwalimu wao mkubwa ni jamaa mmoja Cyprian Musiba anayewaharibu kupitia YouTube, magazeti yake na TV online . Jamaa amewaharibu hata vijana wenzetu wengine wafuata mkumbo wavivu kuingia intaneti, maktaba au kusoma vitabu wapate kilicho cha kweli.
 
Halafu huyu jamaa nimemkubali sana kwa kweli, bonge la jasiri, Tanzania mngekua na watu watano wenye ujasiri wa huyu jembe aisei mngekua mbali sana. Mtu unapigwa marisasi 38 ila unarudi huko huko na kugombea urais, unatikisa nchi yote hadi wazee wa system wanapanic na kusindika bila aibu mpaka wanapitiliza.
Huyo ni jabali la Afrika, vijana kwenye bara hili wana mengi ya kujifunza kutoka kwake, vizuri nimeona amealikwa kote kote kuzungumza, aendelee hata kama mumemnyima haki yake huko ila nina uhakika mamilioni ya watu wanaomfatilia habari zake watapata hamasa kimaisha.
 
Back
Top Bottom