Hizi ajali zinaisha lini kila taarifa ya habari vifo toka juzi mda huu chunya kimeita

Hizi ajali zinaisha lini kila taarifa ya habari vifo toka juzi mda huu chunya kimeita

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Yaani tulishazoea haya mambo Desemba muda wa kufunga mahesabu

Lakini naona kama yameanza mapema jamani

Mimi toka majuzi taarifa ya habari ni vifo na ajali tu

Muda huu kuna ajali Chunya, tutawajuza

1725608071895.jpg
 
Tumepokea ajali ya bus la Kampuni ya AN Classic iliyotokea eneo la Kawetele Wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya.

Taarifa zaidi tuendelee kufuatilia vyombo vya habari.

#EndeshaSalamaFikaSalama
#usalamabarabaraninijukumuletusote
 
Ty
 

Attachments

  • 1725608361410.jpg
    1725608361410.jpg
    384.6 KB · Views: 3
Tumepokea ajali ya bus la Kampuni ya AN Classic iliyotokea eneo la Kawetele Wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya.

Taarifa zaidi tuendelee kufuatilia vyombo vya habari.

#EndeshaSalamaFikaSalama
#usalamabarabaraninijukumuletusote
Barabara pia inachangia
 
Ajali ya basi la abiria la Kampuni Baraka Classic imetokea Alfajiri ya leo eneo la kati ya Vigwaza na Kibaha wakati inatoka Dodoma kuelekea Mtwara.

3 days ago

siwambii mpande ndege

#EndeshaSalamaFikaSalama
#usalamabarabaraninijukumuletusote
 

Attachments

  • 1725608449186.jpg
    1725608449186.jpg
    373.1 KB · Views: 4
5 days ago
#HABARI: Wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Endasaki, iliyopo wilayani Hanang mkoani Manyara pamoja na Dereva wao wamefariki dunia, huku wanafunzi 30 wakijeruhiwa baada ya gari aina ya Costa lililokua limewabeba, kugongana uso kwa uso na Lori katika kijiji cha Gajal, walipokua wakisafiri kuelekea Arusha baada ya shule kufungwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Makarani Ahmed, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo.

#EndeshaSalamaFikaSalama
#usalamabarabaraninijukumuletusote
#RSW2024Doroma
 

Attachments

  • 1725608509092.jpg
    1725608509092.jpg
    302.6 KB · Views: 6
22 aug
 

Attachments

  • 1725608617184.jpg
    1725608617184.jpg
    156.8 KB · Views: 3
  • 1725608612775.jpg
    1725608612775.jpg
    122 KB · Views: 4
Ajali ya Bus la Kampuni ya Mtoto Gema na basi dogo la Mahakama.

#EndeshaSalamaFikaSalama
Usalama barabarani ni Jukumu letu sote.
 
Tumepokea taarifa ya ajali ya basi la Kampuni Super Baraka ya Dar Dodoma iliyotokea eneo la Vigwaza mkoa wa Pwani. Kwa taarifa zaidi tuendelee kufuatilia vyombo vya habari..

#EndeshaSalamaFikaSalama
Usalama barabarani ni Jukumu letu sote
 
Akili za madereva wa Tanzania ni shida
 
22 Aug
Ajali ya bus la Ngasere kwenye daraja la kuingia mzunguko wa Bahi Road ukitokea Majengo mkoani Dodoma.

#EndeshaSalamaFikaSalama
Usalama barabarani ni Jukumu letu sote.
 

Attachments

  • 1725608767123.jpg
    1725608767123.jpg
    198 KB · Views: 3
Ajali y bus la Kampuni ya Mtoto Gema na basi dogo la Mahakama huko Mwanza eneo la Kafumu.

Aug hizo zotee

#EndeshaSalamaFikaSalama
Usalama barabarani ni Jukumu letu sote
 

Attachments

  • 1725608802187.jpg
    1725608802187.jpg
    277.6 KB · Views: 5
Aug 8
24
Ajali ya bus la Kampuni ya Luwinzo na Lorry eneo la Mikumi.

Usalama barabarani ni Jukumu letu sote
 
Rsa mbarikiwe sana
DEREVA WA BASI
1. Anapakia wazima wa afya njema;
2. Anapakia wagonjwa;
3. Anapakia walio na akili timamu
4. Anapakia wasio na akili timamu
5. Anapakia walevi
6. Anapakia wasio walevi
7. Anapakia wahalifu
8. Anapakia wasio wahalifu
9. Anapakia wastaarabu
10. Anapakia wasio wastaarabu
11. Anapakia wachawi
12. Anapakia wasio wachawi
13. Anapakia wenye imani kwa Mungu
14. Anapakia wasio na imani kwa Mungu
15. Anapakia walemavu
16. Anapakia wasio walemavu
17. Anapakia Wazee, anapakia vijana
18. Anapakia wanawake, anapakia watoto
19. Anapakia wavuta bangi
20. Anapakia wasiovuta bangi
21. Anapakia wenye taaluma mbalimbali
22. Anapakia wasio na taaluma yoyote
23. Nk
Hawa wote wanamtegemea DEREVA awafikishe salama. Dereva amebeba dhamana ya uhai wao. Dereva anatakiwa kuwavumilia na kuwahudumia wote hawa. Anatakiwa atende kazi yake kwa weledi. Naam, wote ni abiria wake.

RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
 
Aug 4
24
Tumepokea taarifa ya ajali ya gari ndogo ambapo mmiliki wa Mabasi ya kampuni ya Sauli Luxury Solomoni Mwalabhila amefariki dunia kwenye ajali hiyo. Tunatoa pole sana kwa Kampuni ya Sauli Luxury.

Pichani ni marehemu enzi za uhai wake.
 
KINACHOTUSUMBUA BARABARANI NI ULIMBUKENI, YAANI MTAZAMO NA KUKOSA UTAMADUNI WA USALAMA BARABARANI.

Kinachogomba kwetu sisi ni Kukosa utamaduni wa Usalama Barabarani. Huu sio utamaduni wetu. Sio utamaduni wa wamiliki au waajiri wetu;
Sio utamaduni wa Mtanzania mmoja mmoja;
Sio utamaduni wa dereva; wala
Sio utamaduni wa abiria.
Ndio maana kila tunachoambiwa kuhusu usalama barabarani tunaona kama tunalazimishwa tu.

Madereva vyuoni hawafundishwi usalama barabarani, bali wanafundishwa alama na michoro ya barabarani na kujua kuliongoza gari. Usalama barabarani ni zaidi ya alama, michoro na kujua kupeleka gari mbele au nyuma.

Kwetu sisi kujua kuendesha gari au kumiliki gari ni ulimbukeni. Wachache sana tumezaliwa tukakuta magari majumbani kwetu. Wengi tunayakutia ukubwani. Kwa hiyo maisha na matamanio yetu yanakuwa kuendesha gari kuliko usalama wenyewe. Kwa ufupi, sisi ni LIMBUKENI.

Ndio maana utaona mtu akijua kuendesha gari anafurahi halali hata usingizi. Akipewa kuendesha gari kama ajira anafurahi kupitiliza hata mkataba haulizi, anachojali yeye ni chombo. Mtu akifanikiwa kumiliki gari, ndo kabisaa. Matangazo kijiji kizima na ndio maana atataka aendeshe gari lake mwenyewe kutoka Dar hadi Kijijini akawaoneshe wazazi wake.

Tusipoendesha gari kwa kukimbiza sana tunaona kama hatujaendesha vile. Tunaona kama watu wanatudharau hatujui kuendesha. Dereva hataki dereva mwingine akae mbele yake kwani huo ni udhaifuu. Hata kama hawajaagana safari na huyo mwenzake atahakikisha hapitwi.

Tena madereva wa mabasi ni LIMBUKENI zaidi. Wee utajua tu kutokana na stori zao Kijiwe Nongwa au Mti majungu pale au kwenye basi, utasikia dah ile chuma kali kishenzi. Dah! Yaani hii mashine moto wa kuotea mbali, hili jiko hugusi hiliii. Yaani wee tukitoka hapa tuelekee Mwanza, hunipiti hata dakika 1 tu. Kwa ufupi Mwendo ni ufahari, Ovateki ya gari moja au zaidi ni ufahari.

Ndio maana madereva wa mabasi utaongea nao saa hizi hapa. Watakusikiliza, watakuelewa vizurii, ngoja wapande kwenye siti zao washike usukani utaona aisee. Kila mlichozungumza wakiwa chini wamesimama, wamesahau kabisaa. Utadhani sio wale waliokuwa wakiitikia ndio, ndio, ndio. Ndio maana utaona dereva akipigiwa miluzi au kushangiliwa anavyochanganyikiwa. Anapandisha mori, anajiona bonge la shujaa, anataka hata mwanae mdogo au mkewe nyumbani angekuwepo aone jinsi huko njiani alivyotengeneza heshima. Akiona ameendesha hamumsifu, hadi anaweza kwenda kwa mganga kujiuliza kuna nini mbona jamaa hawanishangilii kabisa na kupiga gia kote hukuu?

Hivyo, tuna kazi kubwa sana ya kujenga Utamaduni wa usalama barabarani, utamaduni ambao watu tangu wakiwa wadogo wataona hili ni jukumu letu sote. Wataona magari ni kitu cha kawaida sana. Wataona kujua kuendesha ni kama kupata ujuzi mwingine wowote. Wataondoa mtazamo kwamba kupitwa na gari nyingine ni udhaifu, watafahamu kwamba barabarani magari yanatofautiana spidi, na kila gari dereva wake ana ratiba yake tofauti na ya kwake.

RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.
 
July 30
 

Attachments

  • 1725609044142.jpg
    1725609044142.jpg
    241.5 KB · Views: 3
Poleni Wote
Waliofariki Wapumzike Kwa Amani
Majeruhi Wapone Harakaa Sana
 
Bus la AN Classic T 682 EGU, lililokua linaelekea Tabora kutokea Dar es Salaam limepata ajali eneo linafahamika kwa jina la Chaya.

Jul hioo
Usalama barabarani ni Jukumu letu sote.
 
JUL 22
24
Taarifa ya ajali ya basi la abiria la ZUBE TRANS, lililokua linatokea Mwanza kuelekea Dar kugongana na lori lililokua limebeba soda eneo la Keminyanga Wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo alfajiri.

Usalama barabarani ni Jukumu letu sote
 
Back
Top Bottom