Hizi english Medium zimejikita kuwaridhisha wazazi wa wanafunzi kuliko kutoa elimu

Kwa Mfano shule ipi / zipi?
 
Kwa class I Hadi III Huwa tunayachezea sana. Hadi Huwa tunafuta majibu yasiyosahihi, tunaweka ya ukweli ili madogo wapate kuanzia tisini. Mzazi akiiona atafurahia na kuongeza moto wa kusaka pesa ili alipe ada.


Kwetu mtu Huwa havuki 15.5 ya 123 hata wanafunzi wakiwa 57 Huwa tunawadabi ili wazaz wapumbavu wafurahie.

Wakifika la nne Huwa tunawaseti kimkakati wapate A tupu.
 
Inaonekana wewe siyo mwalimu maana hata namna ya kupanga nafasi hujui kabisa
 
Na necta je ?
 
Wakishaandika mwanafunzi amekua wa mwisho wewe mtoa maada utaridhika ? Iwe hivo unavosema wanafanya au hawafanyi, cha msingi usikwepe jukumu la msingi la mzazi Kwa mtoto wake, kumfuatilia matokeo yake na karatasi kiujumla ...ukijiridhisha nenda katoe Comments shuleni sio kwenye social networks...lakini usisahau una machaguo ya shule zaidi ya elfu za kumpeleka mwanao...
 
Nimeshangaa sana mwanangu kashika nafasi ya 15, lakini nikimpa hiyo mitihani aliyopata hawezi kujibu hata moja. Hapa sielewk nifanyaje! Mwanangu haelewi kabisa mambo ya shule, sijajua tatizo ni nini!
 
Acha kupoteza hela wewe kamata mtoto wako nenda kamtupe kayumba
Nimeshangaa sana mwanangu kashika nafasi ya 15, lakini nikimpa hiyo mitihani aliyopata hawezi kujibu hata moja. Hapa sielewk nifanyaje! Mwanangu haelewi kabisa mambo ya shule, sijajua tatizo ni nini!
 
Mna hela za kuchezea nyie wacheni muendelee kupigwa hivyo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…