Hizi familia hizi zina mengi mazito.

Sasa cha muhimu fanya mambo yako ikiwezekana makazi yako yawe mbali kabisa na makazi yao.

Kama wanaishi mkoa huu wewe hama huo mkoa ukaanze maisha yako... Kama ni ndugu utawapata tu ambao ni majirani au watatoka kwenye kiuno chako
tayari NPO mkoa mwngn kbs na hawajui nipo mkoa upi kikazi na namba zangu hawana Ila kuna dogo mmoja upande WA ma mdogo ni WA kike ananikubali kinyama yaani hata nikipotea vp atapambana mpk anipate uzuri Naye hamkubali Mzee wala shangaz zake. Na anajua fika sina shida na mama ake Ila wabaya ni kina shangazi huyu ndo huwa kidogo tunawasiliana Sana pia yupo dogo WA aunt yng ndiye kufa na kuzkana maana misimamo yetu inaendana kuhusu ndugu.
tatu Nina marafiki zangu wawili hao ni zaidi ya ndugu kbs nilisoma nao advance na chuo mmoja ni pastor mwngn ni advocate sjawahi pata shida hata kidogo wasje aisee.
 
Sijaona kosa lako popote, kama ulishajishusa ukaomba radhi, na mlishakaa kikao kwa kosa la kumalizia hasira kwa dogo, kwa upande wako huna kinyongo songa mbele, jitahidi tu hudhuria sherehe ya mwisho ya Mzee ikiwa atatangulia, mengine ishi wewe, na wanaokutaka songa mbele timua vumbi haswaa
 
Kwani wewe ndo mtoto wa kiume pekee katika hiyo familia ?
 

Focus kwenye mambo yako
 
Mkoa siwezi sema mkuu si unajua. Ila nipo kanda ya ziwa.
Kutonikubali kwao ilikuwa kimaslahi Tu maana Mzee alikuwa njema kiuchumi kuliko ndugu zake wote na walikuwa wanamtegemea Sana sa alipoanza hamishia nguvu kwangu na Mimi nilivyokuwa najaribu kuangalia sn maslahi ya familia Kwanza kuliko wengne ikaanza kuwapa shida ndugu WA Mzee ukizngatia hao akina aunt ndo wakimpindua mama na kufanya house awe mama mwny nyumba.
Kuhusu ma mdogo nadhan hofu yake ilikuwa endapo taendelea kushika hatamu Kwa Mzee uwenda swala la Maza kupinduliwa ningeliibua ikampa shida sn pale kwenye mji wake ikabd awe upande WA WiFi zake wanipindue kama walivyompindua maza
Mzee akikubali wewe kuliko hata mkewe????
Na shangazi zako je???
Kwani Nini wasikukubali wewe uzao wao???
Kwani Sasa upo mkoa gani Mkuu
 

Kuna logic
 
Kwani wewe ndo mtoro wa kiume pekee katika hiyo familia ?
Kiuhalisia Mimi ndiye mtoto WA Kwanza na wakiume kwny familia.
Mzee alipoachana na Maza akapata mke mwngne Naye akapata mtoto WA kiume Ila ni kadogo sn kapo standard one kwasasa na Mzee alishastaafu miaka mitano sasa.
 
Pole sana ndugu yangu
Nikuulze kitu,,kwa baba wewe ni mtoto wa ngapi? Je wanaume mko wangapi kwa baba? Je mama yetu yuko wp kwa sasa?
 
Wewe ni mkorofi jirekebishe na mweshimu baba y'ako na huyo mama mdogo inaonyesha una kabifu kisa mamako, watafte uwe unawasalimia na kuwatumia hata ka hela ka sukari, ushinde ubaya kwa wema na mimi sijaona kosa hapo
 
Huyo Ni baba yako mzazi au baba mdogo wako?
 
Kwenye familia ukishaona sijui Mashangazi au wajomba wana nguvu kuliko baba ujue kuna shida.

Dada yangu anakuaje na nguvu hadi kuleta fitina kwenye familia yangu?
 
Mimi kwa mzee nimetoka Kikwete akigombea awamu ya kwanza. Nilipatembelea tena mwaka 2011 na sijarudi tena. Leo hii sipakumbuki, naweza kwenda endapo tu mke wake atakuwa safari ya mbali. Mambo ya kuhatarisha usalama wangu sitaki
 
Pole sana ndugu yangu
Nikuulze kitu,,kwa baba wewe ni mtoto wa ngapi? Je wanaume mko wangapi kwa baba? Je mama yetu yuko wp kwa sasa?
Mi ndiye first born mkuu. Wanaume tuko watatu dogo anayefuata WA tatu ni WA kiume bt Naye ni kama Mzee hamtambui maana shangazi walimwambia Mzee Yule si mtoto wake kwahiyo hatambuliki. WA kiume mwngn ni ma mdogo bado mdogo sn yupo standard one.
 
Pole sana ndugu yangu
Nikuulze kitu,,kwa baba wewe ni mtoto wa ngapi? Je wanaume mko wangapi kwa baba? Je mama yetu yuko wp kwa sasa?
Mtoto WA Kwanza. Mama yupo kwao huko miaka mingi sasa Ila huwa tunawasiliana. Kuna thread niliiweka humu khs namna ilivyotokea khs yeye kuondoka na nn kilifuata
 
Wewe ni mkorofi jirekebishe na mweshimu baba y'ako na huyo mama mdogo inaonyesha una kabifu kisa mamako, watafte uwe unawasalimia na kuwatumia hata ka hela ka sukari, ushinde ubaya kwa wema na mimi sijaona kosa hapo
Sawa
 
Mimi kwa mzee nimetoka Kikwete akigombea awamu ya kwanza. Nilipatembelea tena mwaka 2011 na sijarudi tena. Leo hii sipakumbuki, naweza kwenda endapo tu mke wake atakuwa safari ya mbali. Mambo ya kuhatarisha usalama wangu sitaki
Aisee! pole sana
 
Aisee kama tunafanana mzee ila yangu yamezd.

Hawa wazee wetu pasua sana sema basi tunakausha,binafsi mzee wangu yeye ajawahi kukosea(akubali kushindwa , ubabe, uchoyo, kutokujali familia)na bifu letu limefika hatua kafuta hadi nmba zangu za simu(kuna ndgu alimuomba ili aongee na mimi akasema hana nmba zangu).....

Me naamin huko alipo ananiombea mabaya nishindwe ili nije nimpigie magoti.

Kwa kifupi ndgu mtoa mada na mm sitokanyaga tena home kwa sababu nishamuomba sana msamaha kwa makosa ambayo kimsingi hayapo lakini amekomaa yahn ile ya bila yeye me siwezi kufanya chochote.

Hii hali siipendi hata kidgo na inaniuuma lakin sina jinsi maana yeye ndo anatka iwe ivo.....

Unaenda mwaka huu sijaonana nae wala yeye kunipigia ingawaje me nampigia kumsalimia ila ananijibu mkato tu.(sahivi hatoina simu yangu tena kwake)

Ila mzee bado nakukubali sana maana hapo nilipo ni juhudi zako, pia ulinifanya utoto wangu nijivunie maana sikukosa kotu kwako shida ilianza nilipofaulu form 4.

Wazee badilikeni acheni kujiona Miungu watu kwa watoto zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…